SCENE 42: -
NYUMBANI KWA BIANCA: -
MCHANA HUOHUO: -
(Liliana anaingia nyumbani kwao
huku Analia kwa uchungu sana)
Bianca:
(anamuona) Liliana…?
Liliana:
mama (analia sana)
Bianca:
vipi mwanangu (anaacha kumwagilizia maua
yake) njoo mama shida nini mwanangu mrembo? Mbona unalia?
Liliana:
(anamsogelea) Robert mama
Bianca:
kafanyaje yule mwanaume?
Liliana:
(anafuta machozi) ameniumiza
sana…kwanza ameniambia kuwa ni mume wa mtu ana mke na watoto
Bianca:
that bastard (anakasirika sana)
Liliana:
cha pili ameniambia kuwa ameathirika na Virusi vya UKIMWI
Bianca:
Jesus…(anasikitika) don’t worry child
utaishi mwanangu utaishi mwanangu nakwambia kweli kabisa kuwa utaishi
Liliana:
maisha yangu yameisha
Bianca:
No ndo kwanza yanaanza mama…
Liliana:
(analia sana)
Bianca:
nyamaza mwanangu kwani wewe hujasikiaga kuwa kuna watu wanaishi na VVU kwa
Zaidi ya miaka hata 30?
Liliana:
(analia sana) mama
Bianca:
achana nae
Liliana:
(Analia sana)
Bianca:
twende ndani mwanangu…hutakiwi kuwa na stress…
Liliana:
mama Robert ameniambia kuwa hataki mtoto tena ana watoto watatu wanatosha
Bianca:
achana nae
Liliana:
bora angenilea mimi na mtoto
Bianca:
nipo mimi…nitakulea mwanangu
Liliana:
mama
Bianca:
achana nae
Liliana:
ameniumiza sana mama
Bianca:
muache mama
Liliana:
ameniambia kuwa anakupenda sana anataka kukuoa
Bianca:
yule ni mshenzi amekuambia hivyo?
Liliana:
ndio mama
Bianca:
ni mjinga siwezi kuwa karibu na mtu aliyemuumiza mwanangu kwa vyovyote vile
Liliana:
oh mama
Bianca:
yule hana akili kama kukuacha si angekuacha kwa uzuri tu kuliko kukufanyia
alivyokufanyia hana akili mjinga sana yule
Liliana:
kwahiyo mama hutamkubali
Bianca:
child, mimi sio mama mbaya naomba uelewe hilo mimi ni mama ninayekupenda kwa
dhati kabisa mama
Liliana:
(anafuta machozi)
Bianca:
hata ingekuwa hivyo Robert hanivutii hata kidogo so relax my child
Liliana:
(anashusha pumzi kuonyesha kuridhika kwa
jibu hilo)
Liliana:
kwahiyo mama nitajikuta namsahau Robert na haya yote yatakuwa mapito?
Bianca:
yes, child…pole kwa haya yote mwanangu ni mapito yataisha tu…usijali utatulia
tu
(Anna anafika walipo)
Liliana:
oh cousin… (Anamkumbatia)
Anna:
nini wewe una shida gani?
Liliana:
nina stress
Bianca:
(kwa Liliana) mama
Liliana:
abee mama?
Bianca:
nimekuambiaje?
Liliana:
basi mama sitaongea tena mama
Bianca:
(kwa tabasamu tulivu anamgeukia Anna)
karibu mama
Anna:
asante aunt
Bianca:
baba yako yuko wapi?
Liliana:
(anacheka) mama nilijua tu
utamuulizia
Bianca:
(anacheka kwa aibu kidogo) namuulizia
tu kama nitakavyouulizia Bella (kwa Anna)
eti Bella yuko wapi?
(Wanacheka)
Anna:
atakuja baadae
Bianca:
(anacheka)
Anna:
hata hivyo sio mbaya sana baba na aunt ni wachumba
Bianca:
(anacheka kwa aibu)
Liliana:
nakumbuka hilo (anatabasamu) tuanze
maandalizi ya harusi
Bianca:
ni mapema sana bwana
Anna:
wala hata sio mapema
Liliana:
eti mapema…mama tuna miezi mitatu bado hatujafanya chochote sio shopping sio
mpango wowote
Anna:
wewe wasiwasi wako nini?
Bianca:
si ndo hapo…embu naombeni mniache mzee mie
Liliana:
eti mzee mama wewe sio mzee wewe ni forever 16
Bianca:
hata mimi naona
(Wanacheka)
Bianca:
(anamuangalia Liliana) afadhali
unacheka mwanangu
Ana:
kwani shida nini maana nauliza hata huniambii
Bianca:
ah achana na hayo
Anna;
(kwa Liliana) cousin?
Liliana:
sijisikii kuongea sasa hivi cousin nitakuambia
Anna:
okay sitawauliza tena ukijisikia kuniambia utaniambia
Liliana:
usijali binamu by the way twende ndani tukale nina njaa
Bianca:
(anacheka)
Liliana:
mama? mbona unacheka?
Bianca:
nimefurahi tu…unapenda kula sana
Liliana:
(anacheka huku anaingia ndani)
Anna:
(anamfuata ndani)
Bianca:
ah mimi sitaendelea kukaa nje naingia ndani nikale mie
Mbise:
nitamalizia kumwagilizia
Bianca:
asante Mbise
Mbise:
(anaendelea kumwagilizia maua)
Bianca:
(anaingia ndani)
0 Comments