I KILLED MY LOVER 43

 


SCENE 43: -

OFISINI KWA BIANCA: -

(Asubuhi tulivu tena yenye kupendeza machoni kwa Bwana na wanadamu, Bianca akiwa ni mwenye tabasamu tulivu anaingia ofisini kwake akiwa na lengo la kuianza siku yake kama ilivyo kawaida yake)

Mfanya usafi: (anamuona na kwa heshima anamsalimia) aunt

Bianca: hello

Mfanya usafi: shikamoo aunt

Bianca: (kwa upole na upendo) marahaba mama hujambo mwanangu…

Mfanya usafi: sijambo…umependeza sana aunt

Bianca: nashukuru sana

Mfanya usafi: (anatabasamu kidogo kisha anaendelea na kazi zake)

Bianca: (anaelekea ofisini kwake)

Mjomba: (anatokea kwa nyuma yake) bibie

Bianca: (anageuka taratibu huku anatabasamu) oh vipi?

Mjomba: umependeza sana…za asubuhi?

Bianca: salama za mwamko?

Mjomba: za mwamko nzuri mrembo wangu

Bianca: (anatabasamu kwa aibu kidogo)

Mjomba: basi cha kufanya wewe endelea na kazi tutaonana baadae mpenzi

Bianca: (anatabasamu kisha anaelekea ofisini kwake)

Mjomba: (anatabasamu kidogo kisha anaelekea ofisini kwake)

Bianca: (anafika ofisini kwake anaweka mkoba pembeni kisha anakaa kwenye kiti chake cha kuunguka) life is good…mwanangu anatarajia kuniletea mjukuu na mimi natarajia kuolewa na mwanaume nimpendae (anacheka) Liliana amekuwa ni kiumbe cha kuniletea bahati na ninajivunia kuwa mama yake nampenda mwanagu

(Mlango wake unagongwa)

Bianca: pita mlango uko wazi

Robert: (anaingia)

Bianca: (tabasamu linaanza kupotea usoni mwake) Robert?

Robert: yes, my queen…mbona umenuna ghafla hujafurahi kuniona hapa?

Bianca: (anaghazabika sana) Liliana yupo chuoni hayupo hapa

Robert: unajua sijaja kwake nimekuja kwako (anamsogelea)

Bianca: (ananyanyuka na kumkwepa) naomba tuheshimiane

Robert: kwanini unanichukia kiasi hicho?

Bianca: sikuchukii na wala sikuwazii mabaya

Robert: sasa mbona hupokei simu zangu na nikikuomba kuonana na wewe hutaki?

Bianca: Robert ndugu yangu naomba uniache tafadhali

Robert: nimeshaachana na mwanao kama unaona hicho ndo kikwazo…nimemuacha kwani hajakuambia?

Bianca: naomba haya mazungumzo yaishie hapa tafadhali naomba

Robert: sitaondoka mpaka utakaponikubalia Bianca nakupenda sana you are so beautiful lady nisaidie nakupenda nataka kuwa na wewe

Bianca: siwezi kuwa na wewe

Robert: kwanini?

Bianca: kwanza nani amekuonyesha ofisini kwangu?

Robert: hilo sio swali nililokuuliza mbona unanijibu swali juu ya swali?

Bianca: okay naolewa na mchumba wangu hatapendezwa na mimi kuwa na mwanaume mwingine

Robert: nani anakuoa Bianca…haki ya Mungu tena bianca sikudanganyi nitamuacha mke wangu na kukuoa wewe mpenzi wangu

Bianca: jamani sikutaki Robert una nini lakini? Una wazimu?

Robert: ndio nina wazimu (anamkumbatia kwa nguvu)

Bianca: (anamsukuma na kumzaba kibao cha nguvu) tena ukome pumbavu sana

Robert: (anashika shavu) nakupenda sana Bianca ila usingenizaba kofi umekosea sana

Bianca: get out…

Robert: utalipa nakwambia

Bianca: embu toka hapa…utanifanya nini?

Robert: umekosea sana usingefanya hivyo nakwambia

Bianca: ndo utanifanya nini? embu acha kunitishia mimi pesa zako hapa hata mimi nina pesa…na usidhani eti kisa una pesa utapata kila kitu utakachotaka…mimi na mwanangu sio bidhaa kwamba utatubadilisha pale utakapotaka

Robert: sina mpango wa kukubadilisha Bianca

Bianca: naomba utoke ofisini kwangu na isitokee hata siku moja umerudi hapa

Robert: (anamkaribia na kumbusu kwa lazima)

Bianca: (anamsukuma na kumpiga kibao kikubwa Zaidi ya mwanzo)

Robert: (anashikwa hasira mpaka macho yanakuwa mekundu) umerudia tena

Bianca: nitarudia mara nyingi Zaidi kama hutaondoka ofisini kwangu

 Robert: (anamvuta na kumlazimisha kumkumbatia)

Bianca: (kwa kupayuka) security

Mjomba: (anasikia sauti ya Bianca anakimbilia ofisini kwa Bianca) nini?

Robert: ondoka hayakuhusu huu ni ugomvi kati ya wapendanao

Mjomba: wewe si Robert mkwe?

Robert: nilikuwa sasa mimi ni baba yake Liliana

Mjomba: una maana gani?

Robert: mimi na Bianca tunapendana

Bianca: sikutaki na wala sitaki kusikia upuuzi wako

Robert: mbona unamuogopa huyu mzee ni nani yako?

Bianca: huyu ni mchumba wangu na siku sio nyingi tutakuwa wanandoa naomba umheshimu

Robert: Bianca seriously umeenda kumchukua huyu mzee mchafu mchafu unaniacha mimi mwananume nadhifu tena mtanashati nina pesa zangu

Bianca: (anacheka kwa kejeli) eti nadhifu…wewe nadhifu? Basi kama ni hivyo baki na unadhifu wako niachie mimi mzee wangu nimempenda mwenyewe na uchafu wake

Robert: I love you and you know it

Bianca: utaondoka mwenyewe au niite polisi?

Robert: usihangaike nitaondoka mwenyewe sasa ila baadae nitarudi

Bianca: hautakaribishwa

Robert: tutaona…(anaondoka)

 Bianca: (anakaa kwenye kiti)

Mjomba: inabidi ukapumzike

Bianca: hapana nipo sawa

Mjomba: (anamkumbatia mchumba wake kwa upendo) nipo pamoja na wewe mpenzi mpaka mwisho usijali mama nipo na wewe

Bianca: asante mpenzi wangu

(wanakumbatiana)

Mjomba: haya nenda nyumbani bibie (anatabasamu) kapumzike mke wangu

Bianca: (anatabasamu kidogo anabeba mkoba wake na kuondoka zake)

Post a Comment

0 Comments