SCENE 49: -
NYUMBANI KWA ROBERT: -
USIKU: -
(Robert anatoka nje ya nyumba
yake kwa lengo la kwenda sehemu Fulani maana amebeba ufunguo wa gari na
anaelekea gari lake, wakati anapiga hatua anahisi kuna mtu anamuangalia kwa
mbali)
Robert:
(anageuka nyuma) nani?
Mtu:
(kakaa kimya)
Robert:
nani?
(Kimya)
Robert:
(anapiga hatua)
Mtu:
(anapiga hatua kumfuata)
Robert:
nani?
Mtu:
(anajitokeza na sio mwingine bali ni
Liliana)
Robert:
you?
Liliana:
(anatabasamu)
Robert:
unafanya nini hapa wewe mwanaharamu
Liliana:
mwanaharamu ni wewe Robert (anacheka)
usidhani nakuogopa yaani nitakuchoma visu kwanza ndo nikuchomee humu ndani
Robert:
(anacheka sana) Oh My God yaani
Liliana bado una mawazo ya kijinga? Eti kuniua mimi? Ona uliposimama yaani
unaniogopa sana
Liliana:
(anamsogelea) you think so? (anatabasamu) usiniambie
Robert:
(anashangaa)
Liliana:
nahesabu siku tu Robert ikifika tu arobaini ya mama yangu nakuua yaani nampa
zawadi hiyo nitakuua kama ulivyomuua mama yangu
Robert:
(kwa ujasiri) usiponiua Liliana
nitakuua mimi Liliana
Liliana:
deal?
Robert:
done
(Wanakaziana macho)
Liliana:
(anatabasamu kwa dharau)
Robert:
(anacheka kwa dharau pia)
Liliana:
nenda ulipokuwa unaenda
Robert:
kila nikikutana na wewe ni lazima mambo yangu yaharibike
Liliana:
yataharibika Zaidi na Zaidi subiria (anacheka
sana) yataharibika utajuta
Robert:
(anachukua simu na kutaka kupiga)
Liliana:
unapigia polisi au wasichana wavivu ambao hawajui kutafuta pesa basi kwa ujinga
huo wanajikuta wanalaghaiwa na wewe na kujiingiza kwenye matatizo?
Robert:
(anaendelea kutafuta namba Fulani)
Liliana:
(anamsogelea Zaidi na kumkazia macho)
unaniogopa?
Robert:
ah wapi
Liliana:
kuna baridi mbona kama unatoka jasho?
Robert:
this is none of your business
Liliana:
ulichogundua ni kwamba mimi ni kifo chako yaani kila kitu chako kinahisi mimi
ni kifo chako ndo maana unatetemeka (anacheka)
Robert:
hunitishi
Liliana:
really?
Robert:
really
Liliana:
haya sawa pigia simu huyo unayetaka aje akusaidie
Robert:
siiti msaada naita dereva wangu
Liliana:
hata huyo ni msaada fikiria tena na tena huwezi kuendesha gari umeniogopa ni
bora uniogope hivihivi my dear maana nitakumaliza
Robert:
nimeshakuambia kwamba hunitishi
Liliana:
na mimi nimekuuliza really
Robert:
nimejibu really
Liliana:
haya bwana…tuendelee kuhesabu siku baba tutafika daddy
Robert:
usiniite daddy
Liliana:
utajijua (anacheka kisha anaondoka)
Robert:
this woman (anabaki na hasira)
Liliana:
nakukera acha nikukere (anacheka sana)
Robert:
ananikera sana sijui katokea wapi
Liliana: (anacheka sana huku anatokomea gizani)
Rpbert:
(anafyonza kisha anaingia kwenye gari) bastard…
0 Comments