SCENE 50: -
BAADA YA SIKU 40: -
USIKU: -
(Usiku ulio mtulivu kabisa, kila
kitu kimetulia kasoro wadudu wa usiku wanalia kwa sifa kumtukuza Muumba wao,
Liliana akiwa amevaa nguo nyeusi tena amejifunika na kitambaa cheuzi usoni
anaingia nyumbani kwa Robert)
Liliana:
(anafika ndani hapo) ona
linavyojiamini limeacha mlango wazi na nilijua tu kuwa linaachaga mlango wazi
maana lina miadi na wanawake huyu mwanaume kweli hana akili mshenzi sana
Robert:
(amelala chumbani kwake hana habari juu
ya ujio wa Liliana)
Liliana:
(anazima taa zote mpaka za nje) ni
giza kwelikweli hapa sasa naweza kuanza kazi yangu (anatoa kisu na kumuendea Robert anaanza kumchoma kwa nguvu)
Robert:
(anaamka kwa maumivu makubwa) jamani
nani?
Liliana:
(anawasha tochi ya simu yake)
umeniona mimi ni kifo chako…
Robert:
Liliana (anatoa macho) nisamehe
Liliana:
ili uniue? Umesahau kuwa tuliambiana kuwa nisipokuua utaniua? No way baba
lazima ufe (anamchoma kisu mfulululizo)
Robert:
(Analia kwa maumivu makubwa kisha anakata
roho)
Liliana:
(anashusha pumzi kubwa sana sana kisha
anacheka kwa nguvu) yes, I killed my lover…I killed him (anajikuta Analia ghafla) mama this is
for you (anachukua dumu la mafuta kisha
anamimina kila pande ya nyumba ile kisha anatoka anawasha kiberiti na kukitupia
pale halafu kwa mwendo wa kasi sana anaondoka zake)
END OF FLASHBACK: -
(Liliana bado kasimama kizimbani
anasimulia kisa kilichosababisha kumuua aliyekuwa hawara yake)
Liliana:
ndo ilikuwa hivyo ni kweli nilimuua kwasababu ya hasira na uchungu hata hivyo
alinikejeli na kunionyesha kuwa yeye ana nguvu hata serikalini
(watu wananong’ona wengine
wanasikitika)
Raphael:
(anasikitika sana)
Lydia:
(anasikitika pia) yaani alikuwa yupo
radhi aniache ili amuoe Bianca pamoja na shida na dhiki tulizopitia pamoja?
Aisee huyu mwanaume hakutakiwa kubaki kwenye jamii yetu
Gabriel:
daddy was my hero ila baada ya kusikia hii hadithi hapana alifanya vibaya
Michael:
daddy why did you do this umemuumiza mtoto wa watu maskini aliishi kwa shida
sana Mungu akampa mama aliyempenda kwa dhati kwa tamaa zako ukamuua umemkosea
sana mtoto wa watu
Hakimu:
(anashusha pumzi) aisee pole sana
binti kwa hayo uliyopitia ila pamoja na yote Mungu atabaki kuwa Mungu kwa ukuu
wake….
Liliana:
asante sana mheshimiwa…nashukuru sana
Hakimu:
(anakaa kimya kidogo) aisee hadithi
inasisimua sana
Watu:
sana aisee
Liliana:
(amejiinamia kwa huzuni)
Hakimu:
una umri gani?
Liliana:
miaka 24
Hakimu:
bado mdogo sana
Liliana:
(anakaa kimya)
Hakimu:
tuchukue mapumziko kidogo kisha tutarudi kusikiliza hukumu
(Watu wananyanyuka na kwenda nje)
Liliana:
(kwa unyonge anatoka kizimbani na kushuka
walipo binamu zake)
Anna:
Liliana
Liliana:
(machozi yanamtoka) nilifanya yale
kwasababu ya hasira na pia niliona kuwa Robert hakufaa kuishi kwenye jamii ila
kumbe nilikuwa nakosea ningejua ningeiachia sheria ifuate mkondo wake
Bella:
basi binamu usilie yameshatokea
Liliana:
nitapokea hukumu nitakayopewa kwa mikono miwili na ndo ninayostahili
Bella:
(anasikitika sana)
Raphael:
(anamuangalia Liliana sana)
Gabriel:
(kwa sauti ya kunong’ona) dogo
sikuelewi what is wrong are you in love with our father’s killer
Raphael:
umeisikia vizuri hiyo hadithi? Nani aliyemfanya mwenzie afanye hilo?
Gabriel:
(anakaa kimya)
Raphael:
inaonekana hujasikiliza hadithi vizuri ametusimulia kwa upana na tumemsikia na
kumuelewa tumejua kwanini alichoma nyumba na kumuua baba yetu, mama yake
aliuawa kinyama alilipa kisasa
Lydia:
baba yenu alinikosea sana
Michael:
(anasikitika sana) yaani baba
alichofanya kwanza alitukana kisha akataka kutukataa kwakweli dah
Lydia:
ndo hivyo... (anaangalia mlangoni)
naona watu wanarudi
Raphael:
(anamuangalia Liliana)
Gabriel:
basi nenda ukamuangalie vizuri maana naona una dukuduku kweli yaani
Raphael:
(anaenda alipo Liliana) Liliana
habari yako?
Liliana:
(anamgeukia) abee salama… (anampa mkono) nani vile?
Raphael:
Raphael
Liliana:
nambie
Raphael:
ah sina la kusema sana nimekuja kukusalimia tu
Liliana:
nashukuru sana (anatabasamu kidogo)
Hakimu:
(anaingia)
(Watu wanakaa kimya kisha
wanasimama kwa heshima)
Hakimu:
(anakaa)
Watu:
(wanakaa pia)
Hakimu:
habari za muda tena?
Watu:
(wanaitikia)
Anna:
(anaonekana kuwa na wasiwasi sana)
Bella:
(Analia maana anatambua kuwa binamu yake
anafungwa)
Anna:
eeh Mungu…
Hakimu:
basi kutokana na hadithi hiyo ya kuhuzunisha tumejua kwanini binti alifanya
unyama ule (anakaa kimya kidogo) hata
hivyo hakupaswa kujichukulia sheria mkononi angeiamini sheria na ingemsaidia
hivyo anahukumiwa kifungo cha miaka saba jela na kazi ngumu (anagonga meza) basi tumeishia hapa (ananyanyuka na kuondoka)
Anna:
(anaangua kilio)
Raphael:
(anasikitika sana)
Liliana:
(anatabasamu)
Askari:
(anamchukua Liliana) twende binti (anamuangalia kwa huruma) hata hivyo
umeishi maisha magumu sana Mungu akusaidie mwisho wako uwe mzuri uwe na familia
na kadhalika miaka saba sio mingi na pia ukiwa na tabia njema utatoka mapema
Liliana:
sawa
Anna:
Liliana my cousin (anamkubatia huku
Analia sana)
Raphael:
(anakuja walipo Liliana na binamu zake)
iam so sorry
Liliana:
(anatabasamu) it is okay (anamfuata askari magereza)
Gabriel:
maskini…yeye furaha yake iko wapi? (anasikitika
sana)
Raphael:
aisee (anasikitika sana)
Lydia:
(hasemi kitu amekaa kimya tu)
(Watu wanatawanyika huku wengi
wao wanaonekana kuwa na huzuni sana)
0 Comments