SCENE 51: -
NYUMBA NDOGO YA ROBERT: -
(Lydia amekaa na watoto wake wakizungumza
mambo mbalimbali ya maisha ikiwemo ya marehemu Robert)
Lydia:
lililotuleta limeisha sasa turudi Canada
Raphael:
sirudi Canada mama
Lydia:
what do you mean?
Raphael:
namaanisha sirudi Canada
Lydia:
vipi kuhusu kazi yako?
Raphael:
nitapata kazi nyingine huku
Gabriel:
una shida gani kwanini hurudi Canada?
Raphael:
nataka nianze kuishi maisha yangu nimeshakuwa mkubwa nina miaka 26 sasa sitaki
kuwa chini ya mtu yeyote najua mimi ni last born wenu naomba msinibebe hivyo
milele
Michael:
are you in love?
Raphael:
(kimya kidogo)
Lydia:
(kwa hasira) kaka yako anakuuliza
mbona hujibu?
Gabriel:
mama please…yeye sio mtoto tena ana haki ya maamuzi yoyote
Lydia:
najua anayempenda
Michael:
kama unamjua basi ni vizuri
Raphael:
yes, iam in love with Liliana
Lydia:
huwezi kushare na baba yako
Raphael:
nampenda
Lydia:
she is H.I.V positive
Raphael:
hata mimi mama…hata mimi ni muathirika usisahau hilo mama
Lydia:
(anamuangalia kwa hasira) nakuambia
achana na huyo mwanamke
Raphael:
no mama iam so sorry
Lydia:
utamuitaje huyo mwanae Raphael mwanangu huu uhusiano hauwezekani
Raphael:
I will make it possible mama
Lydia:
hatakukubali
Raphael:
I don’t care nitafanya kila kitu mpaka anielewe I will not give up mpaka
nimpate kipenzi cha moyo wangu I love her mama
Lydia:
nendeni mkaandae mabegi iam booking flight tunaondoka
Raphael:
mtaenda without me nanunua nyumba
Michael:
bro, she is in jail now
Raphael:
I will wait for her
Lydia:
seven years?
Raphael:
hata kama ingekuwa kumi
Gabriel:
aisee inasikitisha sasa amekukubali?
Raphael:
I don’t care atanikubali tu nitapambana mpaka nimpate yeye ni kila kitu I want
her to be my wife
Lydia:
be careful young man usione nimenyamaza ukadhani nafurahia
Raphael:
iam so sorry mama ila rudi Canada peke yako au na kaka zangu
Gabriel:
iam not going back either
Lydia:
usiniambie you are also in love
Gabriel:
yes
Lydia:
(anashangaa) na nani?
Gabriel:
with the country
Michael:
iam not going back too
Lydia:
mna matatizo gani?
Gabriel:
baba alitaka tuje huku
Michael:
alitaka kutufata
Gabriel:
mara ya mwisho alisema tuje huku
Lydia:
okay enough… (anakaa kimya) hata mimi
sirudi Canada
(Wanashangilia)
Lydia:
ila upuuzi wako wewe Raphael sijauafiki
Raphael:
I said iam sorry mama
Lydia:
siafiki
Gabriel:
mama Raphael huyu si unamjua? Hakuwahi kuwa na girlfriend sijui alikuwa
anaogopa nini…muachie aenjoi first experience yake
(Michael na Gabriel wanacheka)
Lydia:
it is not funny…unadhani atamuitaje yule mtoto
Gabriel:
wherever mama amuite kaka, ba mdogo vyovyote mama ni sawa tu
Lydia:
no…no..no ana bahati mbaya huyo mara wazazi wake wamekufa haya na huyo Bianca
nae kafa unataka kwenda kufa mwanangu?
Raphael:
sifi mama nitaishi vizuri sana
Lydia:
hapana I don’t trust that girl itakuwa amezaliwa na mikosi
Raphael:
ipi mama?
Lydia:
kila anayemsogelea anakufa…nyie itafakarini hadithi yake
Raphael:
she deserves to be happy mama hata yeye ni mtu
Lydia:
sijakataa kwamba yeye sio mtu
Gabriel:
bali?
Lydia:
sitaki aisogelee familia yangu tena
Michael:
too late mama, last born wako ameshamuangukia
(Wanacheka)
Lydia:
sasa mnacheka nini?
Gabriel:
kesho tukamuone
Lydia:
nani?
Michael:
mkwe wako
Lydia:
over my dead body
Gabriel:
relax
Lydia:
(ananyanyuka na kuondoka kwa hasira)
Raphael:
(anataka kumfuata)
Gabriel:
Rapha muache
Michael:
rudi ukae anahitaji kutulia kwanza we can understand her
Raphael:
(anakaa kimya)
Gabriel:
wewe kama umempenda basi kuwa nae tu fight for her
Michael:
we will support you don’t worry sawa ee
Raphael:
sawa brothers nashukuru sana
Gabriel:
relax sawa ee
Raphael:
(ananyanyuka) ngoja nikapumzike
Gabriel:
okay brother
Raphael:
(anaondoka kuelekea chumbani)
0 Comments