SCENE 52: -
GEREZANI: -
(Liliana yupo gerezani
akimnyonyesha mwanae anaonekana hana wasiwasi wala huzuni kuhusu hayo yote
yanayotokea kwake)
Mmoja
wa wafungwa: (anakuja alipo) wewe
mpole sana…
Liliana:
(anacheka) ila muuaji
Mfungwa:
hapana sio hivyo bwana ulikuwa na maana yako yule askari ametusimulia yaani
tumekuonea huruma
Liliana:
(anacheka)
Mfungwa:
mwanao mzuri…anaitwa nani?
Liliana:
anaitwa Bianca
Mfungwa:
mama yako wa pili?
Liliana:
(anaitikia kwa kichwa ishara ya kukubali)
Mfungwa:
naitwa Mage
Liliana:
mimi naitwa Liliana au mama Bianca
Mage:
safi sana shoga yangu
Liliana:
(anatabasamu)
Askari:
(anakuja) mama Bianca
Liliana:
abee
Askari:
kuna wageni wako wanakuita
Liliana:
oh sawa (ananyanyuka na kuelekea nje)
(Nje kuna Raphael, Anna, Bella,
Gabriel na Michael)
Liliana:
(anafurahi kuwaona) mmekuja?
Anna:
(anamchukua mtoto kutoka kwa Liliana)
Liliana:
jamani karibuni
Raphael:
(anatabasamu anapomuona Liliana
anatabasamu)
Liliana:
karibuni mkae
(Wanakaa)
Liliana:
(kwa watoto wa Robert) bora mmekuja
nataka niombe msamaha kwa yale yaliyotokea najua mmenichukia sana
Raphael:
(anatabasamu)
Gabriel:
usijali Lily hayo yamepita labda sisi kwa nafasi hii tukuombe radhi kwa yale
yote uliyopitia tena yaliyosababishwa na mzee wetu najua asingefanya hivyo wala
na wewe usingefanya hivyo
Liliana:
(anaonekana kuridhika na jibu la Gabriel)
asante kaka
Gabriel:
Gabriel
Michael:
na mimi naitwa Michael na huyu (anamshika
Raphael bega) mdogo wetu wa mwisho anaitwa Raphael hajaoa wala nini ni
mchapakazi ni mfanyabiashara mzuri pia
Gabriel:
(anacheka) jamaa hili umeulizwa
kwani?
Raphael:
(anacheka kwa aibu)
Liliana:
(anatabasamu) nafurahi kuwafahamu
Raphael:
(anamchukua mtoto kutoka kwa Anna)
Gabriel:
(anamchungulia mtoto) aaaawh katoto
karembo
Liliana:
kama bibi yake
(Wanacheka)
Liliana:
(tabasamu linapotea ghafla)
Raphael:
vipi mbona tabasamu limepotea
Liliana:
bado kidonda kibichi moyoni mwangu namkumbuka sana mama yangu kipenzi mama
aliyenilea kwa upendo mkubwa alinipa kila kitu leo hayupo (Analia)
Bella:
lakini binamu hatujaja ili tuone machozi yako tumekuja ili tuone tabasamu la
matumaini na sio huzuni
Liliana:
(anafuta machozi)
Raphael:
(anatoa kitambaa kutoka mfukoni na
kumpatia Liliana)
Liliana: (anapokea
kisha anajifuta machozi) asante
Anna:
(anamuangalia Raphael) kijana
anaonekana ame…
Liliana:
wala unaangalia vibaya
Bella;
haya yetu macho
(Wanacheka)
Gabriel:
sikujua nyie wadada ni watabiri wazuri wanasema lisemalo lipo kama halipo
linakuja hili sasa sijui lipo au linakuja ndo Raphael utuambie
Liliana:
(anacheka kwa aibu)
Raphael:
(anacheka kwa aibu pia)
Bella:
oyooooo hapa naona mambo mazuri sana
Liliana:
kivipi?
Michael:
anyways tungependa kuangalia mazingira ya magereza hii inavutia sana (kwa Gabriel, Anna na Bella) twendeni
tukatembee kidogo
Kichanga:
(kinalia)
Gabriel:
(kwa Raphael) mpe Liliana mtoto
Liliana:
(anamchukua na kumnyonyesha)
Gabriel:
haya sisi tupo huku
(Wanaondoka na kuwaacha Raphael
na Liliana peke yao)
Raphael:
(anakohoa kidogo)
Liliana:
(anamuangalia)
Raphael:
ah (anashikwa na kigugumizi)
Liliana:
vipi?
Raphael:
najua sio muda muafaka wa kuongea haya mazungumzo ila siwezi kusubiri tena
Liliana:
unazungumzia nini Raphael?
Raphael:
ah naomba uniruhusu niwe baba yake Bianca na baba wa familia yako
Liliana:
(anashtuka kidogo) me?
Raphael:
yes, you Liliana
Liliana:
how is that possible?
Raphael:
what do you mean?
Liliana:
iam your father’s killer
Raphael:
I know lakini pamoja na hayo I want to give you family labda Mungu alitaka
uitengeneze familia mwenyewe
Liliana:
mimi nimlaaniwa kila atakayenisogelea basi ataumia au kufa
Raphael:
hapana sio kweli Liliana naomba nafasi utaona mambo yatakavyokuwa
Liliana:
(anaguna) I don’t know
Raphael:
please think about it I wont rush you
Liliana:
mimi sikufai
Raphael:
nani kasema?
Liliana:
(anatikisa kichwa)
Raphael:
think about it (anambusu kwenye paji la
uso kisha anambusu kichanga halafu anaondoka zake)
Liliana: (anabaki na maswali mengi sana) nini tena hii? Yaani nitembee na
baba mtu na mtoto? Nahisi sio vizuri lakini pia mimi ni muathirika nitamuua
mtoto wa watu (anaendelea kujiuliza
maswali mengi sana)
0 Comments