SCENE 53: -
BAADA YA MIEZI MITATU: -
GEREZANI: -
(Raphael anafika magereza ambapo
imekuwa ni kawaida yake kufika mahali hapo kila siku kumuona Liliana)
Raphael:
(anaketi mara baada ya kumuona Liliana)
unaendeleaje my love?
Liliana:
naendelea vizuri
Raphael:
umeshakunywa dawa baby?
Liliana:
ndio tayari wewe je?
Raphael:
mapema sana
Liliana:
(anatabasamu)
Raphael:
vipi Bianca yuko wapi?
Liliana:
bado amelala
Raphael:
(anacheka kidogo) leo bibie vipi
kalala mpaka sasa hivi
Lilana:
(anacheka) ukorofi tu hana lolote
Raphael:
(anacheka kisha anakaa kimya kwa muda
huku macho yake yanamtazama Liliana)
Liliana:
(anatabasamu) mbona unaiangalia sana?
Raphael:
asante
Liliana:
ya nini?
Raphael:
kila kitu
Liliana:
oh My God Rapha
Raphael:
what? (anatabasamu) asante kwa
kunikubali maana nimetumia miezi miwili kuomba unikubali niwe mpenzi wako
Liliana:
na ulikomaa (anacheka) mimi
nilikuambia ya kwamba siwezi kuwa na wewe maana tayari niliwahi kuwa na baba
yako na pili ni muathirika…lakini hata hukuogopa
Raphel:
unajua funny fact ya mapenzi ni kwamba hayachagui I mean moyo ndo huwa
hauchagui nani wa kumuangukia nilikuangukia tangu siku ya kwanza nakuona pamoja
na kwamba wewe ni muuaji wa baba yangu bado tu nilihitaji kuwa na wewe
Liliana:
(anacheka) yaani wewe
Raphael:
ulipohukumiwa nilimuambia mama yangu juu ya hisia zangu kwako alikataa na wala
sikujali nikakomaa na wewe kwasababu tayari nilikuwa nimekupenda sana sikuwa
nimesikia la mtu kaka zangu tu ndo walikuwa wamenichukulia mimi na ujinga wangu
Liliana:
(anacheka) umenifanya mwenzio nimetukanwa
na mama yako
Raphael:
(anashangaa) usiniambie mama yangu
alikutukana
Liliana:
ila yameisha huwezi kuamini mara ya mwisho kabisa ameniambia kuwa anatuacha tu
tuwe na kwamba amenikubali hata siku nikitoka kifungoni nitakaribishwa nyumbani
kwenu
Raphael:
oh My God (anafurahi sana) nafurahi
sana baby…tutafunga ndoa mapema tu ukitoka
Liliana:
mwaka gani?
Raphael:
hata ikiwa baada ya miaka mia sawa tu
Liliana:
lakini Rapha
Raphael:
I swear
Liliana:
(anacheka kwa aibu)
Raphael:
(anashika mikono ya mpenzi wake na
kuibusu)
Liliana:
asante kwa kunipenda
Raphael:
unanipenda?
Liliana:
(anacheka) nakupenda ndio
Raphael:
ila sio Zaidi yangu
Liliana:
nakupenda sana baby
Raphael:
(anatabasamu) asante mama watoto
wangu
Liliana:
(anacheka)
Raphael:
by the way baby…nimeshafungua ofisi, nimenunua nyumba
Liliana:
ndani ya miezi mitatu hiyo?
Raphael:
nilikuwa na hela kwenye akiba zangu…pesa nyingi tu na pia kwenye urithi wa baba
mama ametugaia so hiyo imenipa nafasi ya kufanya yote hayo
Liliana:
hongera sana
Raphael:
ukitoka tu tutafunga ndoa
Liliana:
baada ya miaka saba?
Raphael:
ndio au nitaomba kama itawezekana nifunge ndoa na wewe ukiwa humu
Liliana:
sidhani kama watakubali
Raphel:
tutawauliza
Liliana:
(anacheka)
Raphael:
by the way nimekuja na chakula chako ukipendacho sana
Liliana:
umejuaje kuwa nina njaa?
Raphael:
nimehisi tu maana hata mimi nina njaa nikaona kabla sijaingia ofisini nipite
hapa nile na wewe kisha niende kazini
Liliana:
(bila kutegemea anambusu mpenzi wake
mdomoni)
Raaphael:
(anashangaa) wow thank you (anambusu pia)
Liliana:
(anacheka)
Raphael:
(anacheka) haya kula darling
Liliana:
(anaanza kula)
Raphael:
(anakula huku anamuangalia mpenzi wake)
Liliana:
wewe mbona unaniangalia sana unataka kunikariri?
Raphael:
hapana nashangaa tu uzuri wako
Liliana:
(anacheka huku anatikisa kichwa)
Raphael:
ni nini baby? Mbona unatikisa kichwa?
Askari:
(anawaangalia kisha anacheka)
Raphael:
(anafurahi sana)
Liliana:
kula uende ofisini
Raphael:
mimi ndo boss nikitaka sitaenda
Liliana:
kwani tayari umeweka na wafanyakazi?
Raphael:
lazima niwe nao kazi zangu sio rahisi kufanya mwenyewe
Liliana:
I can imagine
Raphael:
ndo uimagine sasa
(Wanacheka)
Liliana:
(anamaliza kula) haya mie nimemaliza
naomba na wewe umalizie uende kazini
Raphael:
nimeshamaliza hata hivyo (anakusanya
mifuko waliyotumia)
Liliana:
acha nikatupe (anaenda kutupa)
Raphael:
haya mie naenda nilikuja kukuona tu kidogo kupata kifungua kinywa nawe baadae
nitakuja tupate chakula cha mchana pamoja
Liliana:
asante
(Wanakumbatiana)
Raphael:
(anambusu kisha anaondoka zake)
Liliana: (anarudi gerezani)
0 Comments