SCENE 54: -
USIKU: -
GEREZANI: -
(Usiku mtulivu sana nje kuna
upepo mwanana unavuma huku miti nayo inaukubali upepo ule na taratibu inayumba
kwa madaha huku ikimtukuza Mungu, Liliana amelala usingizi wenye utulivu na hapo
anaota njonzi)
(Ndoto)
Bianca:
(marehemu anakuja namnyanyua Liliana
kichwa na kukiweka kwenye mapaja yake kama kumpakata)
Liliana:
(anamuona) mama? (anafurahi sana)
Bianca:
(anafurahi sana) abee mwanangu
Liliana:
umekuja?
Bianca:
sijaja peke yangu nimekuja na mama yako
Liliana:
mama yangu?
Bianca:
(anatabasamu)
Mama
mzazi: mwanangu
Liliana:
(anafurahi kumuona mama yake)
mmekutana huko?
Mama:
ndio mwanangu na nimemshukuru kwa kukulea vizuri na kukupenda
Liliana:
(anafurahi) nimewakumbuka
Bianca:
pole sana liliana…pole hata kwa hili unalopitia (anaonekana kuwa na huzuni) ni mimi ndo nimekusababishia mpaka leo
upo hapa
Liliana:
(anakaa maana alikuwa amelalia mapaja ya
Bianca) hapana mama nilimuadhibu Robert kwa lile alilokufanyia mama
Mama:
(anatabasamu)
Bianca:
hata hivyo sijaja kulia hapa nimekuja kukuambia ni wakati wako wa kufurahia
maisha Liliana hautawahi kuja kuteseka kama ulivyoteseka maisha yako yote
Liliana:
(anamuangalia mama yake mzazi) nataka
niende na nyie
Bianca:
ili iweje mama? Bianca utamuachia nani? Vipi kuhusu mpenzi wako? Wote hao
wanakuhitaji (anamshika bega) hata
jela hautakaa sana mama utatoka
Liliana:
(anakaa kimya)
Mama:
vipi unawaza nini?
Liliana:
namuwaza Raphael
Bianca:
amefanya nini?
Liliana:
ananipenda kweli
Bianca:
anakupenda kweli na wala sio utani yule kijana ndo sababu ya furaha yako
mwanangu
Liliana:
kwahiyo nimuamini?
Bianca:
kabisa
Mama:
muamini mwanangu wewe na yule kijana mtajenga familia nzuri yenye upendo
utasahau maisha yako ya zamani utasahau uchungu ambao maisha yamekupitisha
mwanangu utakuwa ni mwenye furaha
Liliana:
kweli mama?
Bianca:
kabisa
Mama:
acha kuhuzunika kuwa na furaha maana huu ni mwanzo mama furaha yako iko mbele
inakuja utaifurahi sana
Liliana:
asante mama
Bianca:
tunakupenda sana mwanetu
Liliana:
nawapenda sana mama
(Bianca na mama wanatoweka)
Liliana:
(anashtuka kutoka usingizini)
Mage:
(amelala pembeni yake) vipi mwenzetu
umeota ndoto mbaya?
Liliana:
hapana Mage ile ilikuwa sio ndoto ilikuwa kabisa naongea nao
Mage:
kina nani?
Liliana:
mama zangu
Mage:
mama zako? Kina nani?
Liliana:
mama yangu mzazi na Bianca
Mage:
umewakumbuka tu unawaza sana
Liliana:
hapana walikuja kabisa wamenipa moyo kuwa ni wakati wangu wa kufurahia maisha
Mage:
ni ndoto hiyo
Liliana:
unadhani sitafurahi maisha tena?
Mage:
hapana rafiki yangu sio kwamba hautafurahia maisha nilichomaanisha haiwezekani
mtu aliyekufa akaja tena mkaongea
Liliana:
(anaguna) basi itakuwa ndoto
Mage:
eeh lala
Liliana: (anajifunika shuka huku anajisemea moyoni) iwe ndoto isiwe ndoto
nachojua ni kwamba nimefurahi sana kuwaona tena (anatabasamu)
Kichanga: (kimelala fofofo)
0 Comments