SCENE 55: -
BAADA YA MIAKA MINNE: -
NYUMBANI KWA RAPHAEL: -
(Raphael
amewakusanya watu mbalimbali ikiwemo mama yake, kaka zake na baadhi ya marafiki
zake nyumbani kwake wanaonekana kusherekea jambo Fulani)
Raphael:
(amembeba mtoto Bianca ambae amekuwa na
umri wake ni miaka minne) kwanza kabisa namshukuru Mungu kwa kunifikisha
siku hii (anambusu mtoto Bianca)
Lydia:
(anatabasamu)
Rafiki
1: leo kuna nini Rapha? Ni birthday yako?
Gabriel:
(anatabasamu)
Raphael:
(Anacheka) hapana leo sio birthday
yangu
Rafiki
1: ila kuna nini?
(Honi ya gari inasikika kutoka
nje)
Raphael:
wamefika (anamuweka Bianca chini)
Bianca:
(anamkimbilia Michael)
Raphael:
(anaenda kufungua mlango)
(Liliana pamoja na binamu zake
wanaingia)
Lydia:
(anafurahi kumuona Liliana)
wow…karibu mama Bianca
Liliana:
(anatabasamu) asante sana
Anna:
(kwa Raphael) ndo nini kutuacha peke
yetu tumemchukua ameachiwa jamani Mungu ni mkubwa sana
Bella:
sana
Raphael:
samahanini sana sikuwa na nyie ila ilibidi nije nyumbani niandae mazingira ya
kusherekea huu muujiza
Bianca:
(anamkimbilia mama yake)
Liliana:
jamani ka mama kangu (anamkumbatia na
kumbusu)
Gabriel:
(kwa Liliana) karibu shemeji
Liliana:
asante shemeji
Michael:
karibu Liliana
Liliana:
asante sana shemeji
Raphael:
karibu nyumbani my love (anambusu)
Bella:
awwwh jamani
Anna:
mapenzi mazuri sana
Bella:
sana
Liliana:
(anacheka) mmeanza majungu
Bella:
(anacheka)
Raphael:
(anacheka pia) karibu my love…karibu
nyumbani nimefurahi sana
Lydia:
sio peke yako sasa (anacheka) wote
hapa tumefurahi
Michael:
kabisa
Raphael:
(anatabasamu) haya kwa yule
aliyeniuliza leo kuna nini? Jibu hili hapa kwamba mpenzi wangu ameachiwa huru
baada ya kutumikia kifungo kwa miaka minne
Rafiki
1: wow
Rafiki
2: huyu si alikuwa mpenzi wa baba yako? Raphael unachangia mwanamke na baba
yako?
(Wote waliopo hapo wanaishiwa
uchangamfu)
Raphael:
(anakaa kimya)
Rafiki
2: mbona mna mambo ya ajabu hivyo hamuoni aibu yaani (kwa Liliana) hivi huoni aibu kuliwa na baba na mtoto?
Liliana:
(anaangalia chini kwa aibu)
Rafiki
2: (kwa Lydia) unaruhusu vipi mwanao
kuja kuishi na hawara wa mume wako? Au ulikuwa umefurahi? Na pia kumbuka ya
kwamba huyu ni muuaji wa mume wako
Lydia:
kijana umeongea sana nashukuru kwa mchango wa maneno yako sana ila mwisho wa
siku haya ni maisha yetu na maamuzi haya tumeyafanya tukiwa na akili timamu
Raphael:
(anashusha pumzi)
Lydia:
lililotokea lilitokea na hatukuwa na uwezo wa kubadilisha chochote hapo ni sawa
alikuwa ni hawara wa baba yake Raphael kwani yeye sio mtu mpaka asipate nafasi
ya kupendwa na kupenda pia?
Raphael:
mama achana nae tulijua tu yataongelewa haya lakini pamoja na kuongelewa
sitaachana na mpenzi wangu eti kwasababu watu wanataka hivyo…moyo hauchagui pa
kuangukia sikupanga kama nikionana na Liliana nitamtongoza na awe wangu
ilitokea tu
Rafiki
2: uwe na aibu
Raphael:
(anapaza sauti) uwe na aibu wewe
unayeingilia mambo yasiyokuhusu
Rafiki
2: nakusikitikia sana unadhani jamii inakuchukuliaje?
Raphael:
I don’t care watu wanawaza nini au wanafikiria nini nampenda Liliana na
nitamuoa yeye
Lydia:
(kwa rafiki 2) naona hapa hapakufai
kaka unaweza ukajiondokea mwaya hapa ni kwa watenda dhambi
Rafiki
2: naondoka ndio (anaondoka)
Anna:
duh kwani huyu mtu ni wa wapi? Mbona ana gubu
Raphael:
achana nae (kwa Liliana) baby
Liliana:
lakini anachosema ni sawa yuko sahihi
Michael:
shemeji usimsikilize
Liliana:
(anacheka) hapana shemeji (kwa Raphael) mi naona tuishie hapa
Raphael:
no Liliana huwezi kunifanyia hivi mpenzi wangu nimekusubiri miaka minne vipi
kuhusu mipango yetu ya kumlea mtoto wetu pamoja yaani maneno ya mtu asie na
akili yakubadilishe mawazo?
Liliana:
(anakaa kimya)
Gabriel:
shemeji relax waelewe wasielewe ni nyie na maisha yenu jamani tutakuwa
tunafanya mambo yetu kwa kujali watu sawa ulikuwa na mahusiano na baba sasa
hiyo isiwe fimbo ya kukupigia wewe milele relax shemeji yangu
Liliana:
(anafuta machozi)
Raphael:
(anamshika bega) baby karibu nyumbani
Lydia:
yaliyopita si ndwele tugange yajayo
Anna:
kabisa
Liliana:
asanteni sana kwa ushirikiano kweli kabisa Mungu awabariki sana
Michael:
ubarikiwe pia shemeji
Liliana:
jamani lets celebrate
Raphael:
yes, baby
Lydia:
tule, tunywe, tusahau ya nyuma yote yaliyotuumiza yale yote yaliyotuwekea uadui
na tuwaombee wapendwa wetu waliotutangulia wapumzike kwa amani
Wote:
amina
Liliana:
(ananyanyua glasi yenye shampeni) kwa
mambo mazuri yote yanayokuja mbele yetu cheers
Wote:
cheers (wanagonga glasi)
Liliana:
(anaonekana ni mtu mwenye furaha sana)
Raphael:
(anamkumbatia mpenzi wake)
Anna:
aaawwhh love is such beautiful thing
Bella:
sanaaaaa
Liliana:
(anacheka) embu huko
(Wanaendelea kufurahia na
kusherekea kwa kunywa, kula kucheza muziki na michezo mbalimbali, hali ni
shwari kabisa)
0 Comments