SCENE 56: -
NYUMBANI KWA RAPHAEL: -
(Asubuhi na mapema, Liliana anafika
kwa mpenzi wake akiwa ni mtu mwenye wasiwasi sana)
Liliana:
baby
Raphael:
(anaonekana amezidiwa na ugonjwa Fulani)
Liliana:
(anakaa pembeni yake) baby ni nini?
Au hunywi dawa tena? Usichoke haya ni maisha yetu
Raphael:
(anacheka) no baby nilitaka uwahi
kuja my love najua ningekuita kawaida ungekawia kuja au usingekuja kabisa
Liliana:
baby I don’t understand
Rapahel:
baby it has been four years my love
Liliana:
(anaonekana kutoelewa kitu)
Raphael:
(anacheka) baby...it has been four
years my love
Liliana:
yeah baby
Raphael:
na ndani ya muda wote huo umekuwa mtu mzuri sana yaani best girlfriend
Liliana:
(anatabasamu) hata wewe umekuwa best
boyfriend and best daddy to my child
Raphael:
our child my love
Liliana:
yes, our child
(Wanacheka)
Raphael:
asante kwa kuwa mwenza mzuri mwenye upendo wa dhati na muelewa
Liliana:
wewe ndo asante kwa kuwa mvumilivu umenivumilia nilipokuwa gerezani mpaka
nikatoka bado tu umenionyesha upendo
Raphael:
No baby wewe ndo umenionyesha upendo pamoja na kwamba jamii halikulichukulia
suala la mimi na wewe kuwa wapenzi but still ulichagua kuwa na mimi…asante sana
Liliana nakupenda sana
Liliana:
nami nakupenda Zaidi Raphael wangu
(Wanatabasamu)
Raphael:
hivyo basi kwa kusema haya yote (ananyanyuka
anatoa mkebe mfukoni kisha anapiga goti) Liliana
Liliana:
(anatabasamu) yes baby (anaweka mikono mdomo ishara ya kushangaa)
Raphael:
will you be my wife?
Liliana:
seriously baby? (anatabasamu)
Raphael:
yes, baby will you marry me?
Liliana:
oh my God baby yes (anamkubatia)
Raphael:
(anamvalisha Pete ile yenye urembo mzuri
na yenye thamani sana) she said yes
(Ndugu zao wanakuja kutokea
vyumbani)
Anna:
wacha weeee raha sio raha
Wote:
(wanaitikia) Rahaaaaa
Raphael:
(anatabasamu)
Liliana:
(anashangaa) mlikuwepo?
Anna:
tunakosaje kwa mfano?
Liliana:
(anacheka)
Bella:
ofcourse lazima tuwepo
Raphael:
(Anafurahi sana) asante sana Liliana
kwa kukubali kuwa mke wangu
Liliana:
(anatabasamu)
Raphael:
(kwa watu) haya muanze kujiandaa na
harusi sitataka ichelewe
Michael:
dogo relax unapania sana
Raphael:
sio kweli bwana
Lydia:
imekuwa so soon
Gabriel:
mama umeanza waache bwana najua wewe bado hukubali kwasababu Liliana aliwahi
kuwa mpenzi wa baba mzazi wa Raphael but mama this is love na ikija imekuja na
tunatakiwa kukubaliana nalo
Lydia:
unaongea sana Gabriel kwani mimi nimekuambia sitaki waoane?
(Wanacheka)
Gabriel:
sasa ulimaanisha nini uliposema kuwa imekuwa ghafla sana?
Lydia:
I mean hajamuacha mwanadada akae hata mwezi adange kidogo
(Wote wanaangua kicheko)
Lydia:
anataka kumfunga mapema (anacheka kwa
nguvu)
(Wote wanaangua kicheko)
Raphael:
jamani mama
Lydia:
njoo mziwanda wangu hongera baba kwa kuchumbia (anamkumbatia)
Raphael:
Asante mama yangu (anamkumbatia kisha anambusu kwenye paji la uso)
Michael:
na kisha tusherekee
(Watu wanasherekea kwa kucheza
muziki na kadhalika)
Gabriel:
hakuna bia?
Lydia:
na wewe utaacha lini pombe wewe mtoto (kwa
Anna) naomba umuokoe mwanangu
Anna:
(anacheka kwa aibu)
Liliana:
mambo hayo
Gabriel:
(anacheka kwa aibu pia)
Lydia:
unadhani sijawaona? Au unadhani sijui kinachoendelea kati yenu?
Gabriel:
ni Michael na Bella mama
Lydia:
hata nyie
Raphael:
(anashangaa) mazito
Lydia:
na ndo maana mling’ang’ania kubaki huku mnadhani sijui?
Liliana:
what?
Raphael:
ndugu wanaoa ndugu
Lydia:
mnaendeleza ukoo…pambaneni
(Wanacheka)
Lydia:
ndo vizuri lakini hatujatupana
(Wanacheka)
Michael:
DJ weka mambo (anaangalia huku na huku)
alaaah!! Kumbe hakuna cha Dj wala baba yake DJ ngoja niwe mimi
Lydia:
utakuwa umetusaidia sana mwanangu
Michael:
(anaenda kuchukua vinywaji kwenye friji
kisha anawasha muziki)
Anna:
watu weeeweeeee
(Wanaanza kucheza na kufurahia
maisha yao)
Lydia:
(anashusha pumzi) haya ndo maisha
anayotakiwa kuishi Liliana ameteseka toka akiwa mdogo na Zaidi baba wa watoto
wangu alimsababishia maumivu makubwa sana ila pamoja na yote Mungu atabaki kuwa
Mungu
Raphael:
yes, mama
Liliana:
(anafurahi sana)
Raphael:
happy baby?
Liliana:
very happy
Raphael:
(Anambusu mdomoni)
(Sherehe inaendelea huku kila
mmoja wao anaonekana kuwa na furaha isiyo na kifani na mwenye furaha zaidi sio
mwingine bali ni Liliana)
0 Comments