SCENE 2: -
(Asubuhi njema tena ya kupendeza tena Zaidi
imefanywa na bwana, baba muumba mbingu na nchi, Ken na mkewe wanaenda kituo cha
polisi wakiwa wamembeba mtoto mchanga kabisa na anaonekana amezaliwa siku si
nyingi, wanapofika mahala pale kwakuwa wanajulikana na watu wengi wanasalimiana
na watu wengi sana katika kituo hicho, mara baada ya salamu wanaenda moja kwa
moja mpaka kwa mkuu wa kituo hicho)
Mkuu
wa kituo:(anasimama kusalimiana na Ken
pamoja na mkewe) ah...mkurugenzi…habari yako bwana
Ken:
nzuri kabisa za kazi mkuu?
Mkuu:
nzuri za huko kwenu?
Ken:
tunamshukuru Mungu
Mkuu:(kwa mke wa Ken) shemeji? habari yako?
Keddy:
salama shemeji
Mkuu:
tafadhali ketini
(Wanaketi)
Mkuu:(nae anaketi maana muda wote huo alikuwa amesimama)
ndio niwasaidie nini ndugu zangu? naona mmebebelea mtoto…wa nani?
Ken:
sisi hatujui huyu mtoto tulimkuta jana nje ya nyumba yetu tukamuweka ndani na
tukaambiana tuje tutoe taarifa polisi
Mkuu:
mmefanya vyema sana…kwahiyo hamjui ni wa nani?
Ken:
ndio...hata hatujui ni wa nani?
Mkuu:
sawa kwanini msimuache hapa tutatangaza kwa yeyote aliyepoteza kichanga basi
atamkuta hapa
Keddy:
hapana mkuu…nadhani mama yake alitaka kumuacha kwetu….
Mkuu:
okay…kwanini mmekuja kutoa taarifa
Keddy:
unajua wanadamu tuna mambo mengi anaweza kurudi tena na kusema labda kaibiwa mtoto
na kuleta kizungumkuti ndo maana tunataka kuepukana na hilo
Ken:
tuko tayari kukaa na huyu mtoto mpaka mama yake atakapojitokeza
Mkuu:
sawa…nyie kaeni nae tu mama yake akitokea maana ni lazima atakuja basi akija
basi nitawaambia
Keddy:
sawa hiyo imekaa vizuri
Mkuu:
mtoto gani?
Ken:
wa kike
Keddy:
anaitwa Miriam
Mkuu:
mpaka jina mmeshampa? (anacheka kidogo)
Keddy:
ndio… (anacheka pia)
Mkuu:(anacheka) sasa Ariana amepata mtu wa
kubaki nae nyumbani pindi anapokuwa hayupo shuleni
Ken:si
yeye tu hata sisi tumepata mtoto
Keddy:
njia za Mungu hazichunguziki….
Ken:
kwakweli
Mkuu:(anashusha pumzi) sawa…nyie nendeni
kukiwa na chochote nitawashtua au sio
Ken:
sawa mkuu…
Mkuu:
mtunzeni vyema Miriam
Keddy:
atatunzwa kama Ariana hatokosa chochote katika haya maisha
Mkuu:
vizuri sana
(Ken na mkewe wananyanyuka
kujiandaa kuondoka)
Mkuu:(huku ananyanyuka) sawa malezi mema
Ken:na
wewe kazi njema
(Wanapeana mikono kisha Ken na
mkewe wanaondoka zao na kwenda)
Ken:
tumepata mtoto mke wangu shetani muongo sana walipokutoa kizazi…alitudanganya
na kutuaminisha kuwa hatutapata tena mtoto ila leo tuna mtoto tena mrembo (anatabasamu)
Keddy:
haswa (anapanda kwenye gari kisha anampokea
mume wake mtoto)
Ken:(nae anapanda kwenye gari)
Keddy:
ila umegundua kuwa Ariana hajafurahishwa na ujio wa Miriam
Ken:
shetani Muongo mke wangu anajaribu kukushawishi kuwa mwanao mkubwa hajampenda
mwanao mdogo, ili ukate tamaa nae…wewe mpe muda Ariana ataelewa tu mke wangu
acha kabisa kuwaza mambo yatakayokukosesha Amani
Keddy:
sawa mume wangu nami nakubaliana na wewe honey
Ken:
nina mpenda sana bwana Mungu wangu maana hajawahi kuniacha na hatawahi kufanya
hivyo…
Keddy:
hakika mume wangu
Ken:
amina (anaondoa gari)
(Kuna mwanamke mbele ya gari na sio mwingine
mama mzazi wa Miriam)
Ken:(anashtuka) Yesu wangu
Keddy:
nini baba Ariana…?
Ken:
unajua ningemgonga vibaya huyu dada… (anashuka
kwenye gari) dada vipi mbona unataka kujiua?
Dada:
sina mahali pa kwenda sina wazazi sina chochote naomba mnisaidie…
Keddy:(anashuka) unataka msaada gani?
Dada:
hata niwe msichana wa kazi za ndani…
Ken:
(kwa mkewe) mke wangu sikukwambia
kuwa Mungu anaweza? si tulikuwa tunatafuta msichana wa kazi leo amejileta
mwenyewe
Keddy:
kabisa… (anatabasamu)
Ken:
unaitwa nani?
Dada:
Mary…
Ken:
mama wa Yesu...wow
Keddy:
nakwambia…(anacheka)
Ken:
sawa panda kwenye gari twende nyumbani
(Wote wanapanda kwenye gari,
wanaanza kuondoka)
Mary:
naomba nimbebe mtoto…
Keddy:(anampa)
Mary:(anamchukua kisha anajisemea moyoni)
mwanangu mzuri…hatimaye tena nimekushika nitakulea chini ya uangalizi wa hawa
watu mpaka utakuwa mwanangu…
(Gari linaendelea kwenda na baada
ya dakika kadhaa hatimaye wanafika katika jumba la kifahari la Ken na mkewe)
Ken:
tumefika nyumbani…karibu
Mary:
asante sana
Keddy:
shuka…
(Wanashuka kisha wanaingia ndani)
Keddy:
karibu nyumbani…
Ariana:(anaandika homework)
Keddy:
Ariana…msalimie ma mdogo…kuanzia leo atakuwa anawalea wewe na Miriam
Ariana:(haonyeshi uchangamfu) shikamoo… (huku anaangalia pembeni)
Ken:(anaingia chumbani kwake)
Keddy:(anamuonyesha
Mary, chumba chake cha kulala) humu ndo utakuwa unalala
Mary:
sawa…
Keddy:
hujaja na nguo?
Mary:
ndio
Keddy:
usijali nitakupa zangu ambazo sizivai tena?
Mary:
asante dada
Keddy:(anabaki anatabasamu)
0 Comments