MUNGU MKUU 12

 


SCENE 12: -

(Jeremy amekaa nyumbani kwake akiwa peke yake na anaonekana ana mawazo mengi sana, ameshika simu yake kama mtu anayesubiri kupokea ujumbe Fulani, wakati amekaa amezuba na anaonekana ana mawazo mengi, mama yake anaingia)

Mama :( anamshika bega) baba…

Jeremy :( anashtuka)

Mama: mbona sikuelewi?

Jeremy: shikamoo mama

Mama: marahaba

Jeremy: hunielewi kivipi mama?

Mama: watumishi wako wanasema siku hizi huendi ofisini na watumishi wa nyumbani kwako nao wanasema una mawazo mengi sana baba…vipi kila kitu kipo sawa?

Jeremy :( kimya)

Mama: au unafirisika mwanangu?

Jeremy: bora ningekuwa nafirisika ningeomba hata mkopo niokoe biashara yangu

Mama: kwahiyo nini tatizo baba?

Jeremy: iam in love mama

Mama: hilo wote tunajua…je mchumba wako anakusumbua?

Jeremy: sio yeye…

Mama:ni nani?

Jeremy: mdogo wake

Mama:(anashtuka) wewe Jeremy

Jeremy: yes, mama nampenda Miriam kupita kiasi, siwezi kuwa na mwanamke mwingine

Mama: huruhusiwi kuwa na huyo mtoto

Jeremy: kwanini mama?

Mama: sababu wewe ni mchumba wa dada yake

Jeremy:(anaongea kinyonge) lakini simpendi Ariana mama

Mama: hapana mwanangu wewe muoe tu Ariana

Jeremy: mama, No…sitaki halafu mbaya Zaidi (anataka kulia) Miriam kabadilisha simu…. namba yake haipatikani

Mama: what’s wrong my son…yaani unataka kulia kisa mtoto kama Miriam?

Jeremy: mama please help me mama yangu nakuomba…mimi ni mtoto wako nisaidie mama yangu

Mama: hapana najua wewe ni mwanangu...ila siwezi kukusaidia labda kama ingekuwa hujamchumbia Ariana hapo ningekusaidia

Jeremy: mama nitajiua I swear!!! Sikutanii

Mama: umekuwaje Jeremy embu tulia…lala kidogo tuliza akili yako halafu (anamnusa) mbona kama vile umekunywa pombe…. yaani umelewa wewe mtoto jamani loh, umeanza lini kunywa pombe Jeremy?

Jeremy: nimeanza leo mama nataka nipunguze na kusahau maumivu yote niliyo nayo mama…nisipompata Miriam najiua…I swear

Mama: wewe mtoto utaniletea matatizo ngoja nimpigie baba yako sasa hivi

Jeremy: niambie mama utanisaidia au hunisaidii (anachukua bastola anajiwekea kichwani) nitajiua sasa hivi

Mama: Mungu wangu (simu inaita inapokelewa) baba Jeremy naomba uje haraka Sana nyumbani kwa mtoto wetu

Baba: kuna nini…nakuja mke wangu

Mama :( anakata simu) tulia mwanangu…

Jeremy: utanisaidia au nife?

Mama: baba jamani embu acha masihala

Jeremy: unaona natania?

Mama: jamani baba

(Wakati wanaendelea kujibizana baba Jeremy anafika)

Baba: kuna nini? (Anamuona mwanae kajiwekea bastola) wewe mtoto tatizo nini?

Mama: huyu mtoto anataka kutuletea matatizo

Baba: yapi?

Mama: anamtaka mdogo wake Ariana

Baba: kivipi, kwanini?

Jeremy: nahesabu mpaka kumi…nikiwa sina jibu najilipua haki ya Mungu tena

Baba: jamani

Jeremy: moja…

Mama: baba Jeremy tufanyeje?

Baba:(anatumia ukali) embu acha ujinga Jeremy…shusha hiyo bastola mara moja

Jeremy: mbili

Baba: nimekuambia shusha hiyo bastola

Jeremy: tatu…

Baba: mimi si baba yako na unaniheshimu?

Jeremy: nne…

Mama: Jeremy…Jeremy baba, yule ni mtoto mdogo miaka 18 tu jamani, hayupo tayari kuwa mke wa mtu

Jeremy: tano

Baba:(anawaza kitu)

Jeremy: sita…

Baba: Jeremy unadhani tutafanyaje? unadhani ile familia itatuelewaje?

Jeremy: saba… (anaiweka sawa bastola)

Baba: sawa baba tutakusaidia

Jeremy:(anaacha kuhesabu na kuwaangalia) kivipi

Baba: ila iwe siri mwanangu…mtakuwa wote kisiri sawa eeh…nitaenda mimi mwenyewe kuongea na Miriam atanielewa tu haya shusha bastola mwanangu mzuri…eeh baba yangu tulia mwanangu mzuri jamani

Jeremy: kweli au unaniambia tu ili nishushe bastola

Baba: nimekuahidi mimi baba yako

Jeremy:(anashusha bastola) sawa…utaenda lini?

Baba: hata kesho please relax baba

Jeremy: sawa

Mama: sawa mwanangu utakuwa nae

Jeremy: poa…kama mnanidanganya mtakuta maiti yangu

Mama: hatukudanganyi

Jeremy:(anaingia chumbani kwake)

Mama: huyu mtoto anataka kutuletea shida jamani loh!!!!!

Baba: sijui itakuwaje…mzee Ken hatonielewa kabisaaaa…. yaani mimi najuta

Mama: kwahiyo utaenda?

Jeremy:(yupo kwa ndani anawasikiliza)

Baba: itabidi nikaongee na Miriam…wawe tu hata kwa muda wakati tunafikiria cha kufanya ila Ariana na wazazi wao wasijue chochote

Mama: huyu mtoto katukomesha loh!!!kazini haendi anakunywa tu pombe…

Baba: mwanaume kampenda mwanamke... (anatikisa kichwa) balaa hili jamani

Jeremy:(anatabasamu) ilibidi nitumie njia hii ili niwe na kipenzi changu (anaangalia ile bastola) bastola yenyewe toi(anacheka)nisameheni wazazi wangu…nampenda Miriam kupita kiasi

(Wazazi wanaendelea kuongea, huku Jeremy akiendelea kuwasikiliza)

Post a Comment

0 Comments