SCENE 13: -
(Siku ya pili baada ya Jeremy
kuwatishia wazazi wake, baba yake anaamua kwenda chuoni kwa kina Miriam ili
aongee nae mawili matatu kuhusu Jeremy, anapofika anapiga simu yake)
Baba:
simu imeita muda mrefu sana si cha ajabu yuko darasani na ana kazi (anakata na kutaka kuanza kuondoka, lakini
kabla hajapiga hatuai)
Miriam:(anamuita)
baba
Baba:(anageuka) mwanangu
Miriam:(kwa heshima kubwa) shikamoo baba
Baba:
marahaba mama kwema?
Miriam:
kwema
Baba:(anarudi na kukaa kwenye kimbweta
kinachotumika na wanafunzi kujisomea)
Miriam:
(nae anakaa pembeni yake) nimeona
missed calls zako nikaona nitoke nje nije nijibu…nimetoka tu ndo nikakuona
Baba:
ndio mwanangu nilikuwa na shida na wewe
Miriam:
shida gani baba? na je unahisi mimi nitakusaidia
Baba:
sio nahisi mwanangu najua kabisa utanisaidia kwa asilimia 100
Miriam:(anacheka kidogo) nambie
sasa…nakusikiliza baba
Baba:
una mahusiano na Jeremy?
Miriam:(anashtuka) hapana baba…nani
amekuambia?
Baba:
hamna aliyeniambia nakuuliza tu mama
Miriam:
hapana baba Jeremy ni shemeji yangu alikuja nyumbani kumchumbia dada yangu na
ninaheshimu hilo
Baba:
sawa…kama huna mahusiano nae naomba uwe na mahusiano nae
Miriam:(anashangaa) baba...
Baba:
ndo hivyo…. nakuomba lakini kama unaniheshimu mimi kama baba yako
Miriam:
nakuheshimu sana baba lakini siwezi kuingilia uchumba wa dada yangu…
Baba:
usijali utakuwa tu unajifanyisha tu mbele ya Jeremy
Miriam:
hapana baba…hakuna kujifanyisha
Baba:
Miriam nakuomba mwanangu, unajua mimi nina mtoto mmoja tu, akifa mimi sitakuwa
tena na mrithi
Miriam:
hapana unachoomba ni kitu ambacho hakiwezekani sio kitu rahisi kabisa
Baba:
mwanangu anakupenda sana na anataka kuwa na wewe alitaka mpaka kujiua kisa wewe
mpokee Miriam hata kwa kujifanya unampenda huko mbeleni tutajua
Miriam:
siku dada yangu akijua itakuwa mwisho wangu, hata wazazi hawataelewa
Baba:
najua hawataelewa ila naomba mwanangu…ikiwezekana nitakuwa nakulipa basi…nisaidie
Miriam…mtulize tu afanye kazi zake jamani kila siku amekuwa ni mtu wa kulia na
kutofanya kazi mwenzio ni mfanyabiashara na asipokuwa makini basi biashara zake
zitayumba mama,msaidie huyu mzee aliyoko mbele yako
Miriam:
lakini baba
Baba:
hapana usiseme chochote kile, kaa utafakari…hautakuwa unafanya kitu kibaya
sana…mkubali tu…hata kama wewe hutaki…yeye atajua umemkubali atatulia na
kufanya kazi zake bila tatizo lolote na lile wazo lake la kujiua litaisha
Miriam:
alitaka kujiua?
Baba:
ndio…hiyo ni baada ya kumkatalia asiwe na wewe ndo akaamua kutaka
kujiua…kiukweli sisi na mali zetu zote hizi tuna mtoto mmoja tu…yaani akifa
jamani sijui tu itakuwaje
Miriam:(anakaa kimya huku kama kuna kitu anafikiria)
Baba:
wewe fikiria tu mama lakini nipe jibu la uhakika nikamwambie
Miriam:
tatizo wazazi wangu…
Baba:
hawana shida bwana
Miriam:na
dada yangu je?
Baba:
hatajua kama una mahusiano na Jeremy we ukifika muda Fulani unamuacha tu na
kusema kuwa humuwezi
Miriam:
hapana baba kwanza hiyo sasa ndo itakuwa mbaya sana bora hata nimkatae ajue
kabisa kuwa simtaki kuliko kuja kumkataa mbeleni…kaa tu ufikurie
Baba:
jamani Miriam usiwe na roho hiyo jamani, nisaidie mimi baba yake Jeremy
Miriam:
haya ni maisha baba…ni maisha ya watu watatu unataka kuyachezea
Baba:
I don’t care…ninachojali ni maisha ya mwanangu…
Miriam:
vipi kuhusu dada yangu?
Baba:
mwanangu anamheshimu sana dada yako na sio kwamba anampenda…anakupenda wewe na
yupo tayari kwa lolote ili awe na wewe…sasa mimi nakuomba unisidie jamani Miriam
hutaki jamani?
Miriam:
sio kwamba sitaki…
Baba:
okay…ukweli ni kwamba Jeremy wala hampendi Ariana…je unataka Ariana aolewe na
mwanaume asiyempenda unadhani mwisho wa siku itakuwaje?
Miriam:
watapendana tu…kwani wakati mnaleta habari nyumbani kuwa Jeremy anataka kumuoa
Ariana mlikuwa mnafikiria nini?
Baba:
wala Jeremy alikuwa hatumii akili alitaka tu kuoa apate mwenza wa kuishi na
kumuangalizia biashara zake wakati amesafiri kwenda ulaya na kadhalika…
Miriam:
ameshamuona Ariana si amuoe
Baba:
alikupenda tangu siku ya kwanza anakuona…hata mimi nilimuona amejutia haraka
alizofanya
Miriam:
maji yakishamwagika hayazoleki…hata ikiwaje hayazoleki, mlikuja nyumbani kumuoa
Ariana muoeni mimi naomba mniache msije mkanigombanisha na ndugu zangu
Baba:
kaa ufikirie kisha utamjibu yeye
Miriam:
nenda tu ukamjibu kuwa Miriam kasema hapana
Baba:
wewe unaogopa nini?
Miriam:
sitaki tu…
Baba:
aisee (huku ananyanyuka) basi sawa
mama…mimi naenda mwanangu ila kama una lolote utanipigia au utampgia
yeye…asante kwa muda wako mwanangu na Mungu akubariki
Miriam:
amina baba, karibu tena
Baba:(anaondoka huku anaonekana hana raha)
Miriam:
iam sorry yaani siwezi
Vanessa:(anakuja aliposimama) wewe mbona unaongea
peke yako?
Miriam:
yaani acha tu rafiki yangu…huyu Jeremy anataka kuniletea matatizo
Vanessa:
yapi tena?
Miriam:
amemtuma baba yake aje aniambie ananipenda
Vanessa:na
wewe ukamjibuje
Miriam:
unadhani ningemjibuje? huku wewe unajua kuwa Jeremy mimi ni shemeji yangu
mtarajiwa
Vanessa:ni
kweli humpendi?
Miriam:
sio kwamba simpendi nampenda kama shemeji yangu tu
Vanessa:(anaguna) yaani hii ipo serious…mpaka
baba mtu kaja kumuombea ujue ipo serious
Miriam:
halafu anasema kuwa nijifanye tu nisiwe serious
Vanessa:
kisa?
Miriam:
eti Jeremy alitaka kujiua kisa mimi!!!
Vanessa:
wewe Miriam embu mkubali mtoto wa watu hata kwa kujionyesha tu bwana
Miriam:(anaguna) are you sure hiyo haitakuwa
tatizo?
Vanessa:
nani atamwambia Ariana?
Miriam:
hakuna siri kwenye hii dunia
Vanessa:
ukiitunza vizuri inakuwa siri kubwa sana tu, mimi sitamwambia mtu na nina
uhakika hata wazazi wake hawatamwambia mtu itakuwa ni siri yetu tu
Miriam:
wewe Vanessa…unamjua dada Ariana
Vanessa:
wewe usimuwaze…we angalia kumpa Amani kaka wa watu
Miriam:
yaani wewe una kichaa kweli yaani nikishampa Amani
Vanessa:
halafu unampenda moja kwa moja tunakula harusi
Miriam:
hicho ndicho nachoogopa mwenzio
Vanessa:
haitakuwa mbaya…kwahiyo utamjibu?
Miriam:
sawa…ila tu akinihakikishia kuwa itakuwa ni siri
Vanessa:
hayo ndo maneno…kwanza Ariana na Jeremy wanalingana haipendezi mwanamke na
mwanamume walingane
(Wanacheka
kisha wanarudi darasani)
0 Comments