SCENE 14: -
(Asubuhi ya siku ya pili, Jeremy
amekaa ofisini kwake anaonekana ana mawazo mengi sana, kwa mbali anamuona mtu
kama Miriam anashangaa)
Jeremy:
naota, nawaza au naona kweli? au? yule si Miriam?
Miriam:(anaingia mapokezi na kusalimiana na dada wa mapokezi)
mambo
Dada
wa mapokezi: poa karibu
Miriam:
namuulizia mkurugenzi
Dada:
una appointment nae?
Miriam:
hapana
Dada:(kwa nyodo) kaa hapo nimwambie
(Wakati huo Jeremy anakuja)
Jeremy:(kwa sauti ya chini) Miriam?
Miriam:(anageuka na kuachia tabasamu)
Jeremy:(anajikuta anatabasamu pia)
Dada:
ndo nilikuwa nakupigia nikuambie kuwa kuna dada anakutafuta
Jeremy:(kwa Miriam) karibu Miriam…twende
tukaongee ofisini kwangu mama
(Wanaongozana kuelekea ofisini na
baada ya hatua chache wanafika ofisini kwa Jeremy)
Miriam:(anasimama pembeni)
Jeremy:
karibu keti...mbona umesimama?
(Ofisi ya Jeremy ni ya kifahari,
fenicha zilizomo zinaonekana ni za gharama sana, hata kompyuta na runinga
zilizomo ni za kifahari sana)
Miriam:(anakaa) asante sana
Jeremy:(anacheka) utakunywa nini?
Miriam:
maji tu
Jeremy:
maji na asubuhi yote hii?
Mirriam:
inatosha tu… (anacheka kidogo)
Jeremy:(anatabasamu kidogo kisha ananyanyuka na
kuchukua maji kutoka kwenye friji)
Miriam:(anaiangalia mandhari ya ofisi hiyo)
ofisi yako nzuri sana
Jeremy:(huku anakuja alipo) asante, umeipenda? (anampa maji)
Miriam:(anapokea) ndio nimeipenda sana ni nzuri
sana unajua
Jeremy:(huku anakaa) karibu Miriam
Miriam:
asante sana
(Kimya kinapita huku kila mmoja
wao anatafakari cha kuongea)
Jeremy:(anavunja ukimya) nambie
Miriam:
well, nilipata ujumbe wako, nadhani kwanza kutoka kwako lakini pili kutoka kwa
baba yako
Jeremy….
ndio
Miriam:
nimeona ni sawa tu
Jeremy:
sawa nini?
Miriam:
sawa kwamba mimi na wewe tunaweza kuwa wapenzi
Jeremy:(anapata furaha kubwa na bila kutegemea
ananyanyuka kutoka kwenye kiti chake na kumbeba Miriam) kweli Miriam
Miriam:
yes...kweli
Jeremy:(anambusu
shavuni) asante Miriam, I swear, you have me the happiest man, I love you so
much my queen…
Miriam:(anajaribu
kushuka maana amebebwa)
Jeremy:(bado amembeba na anamnyima nafasi ya kushuka)
usiogope…nakupenda Miriam, sasa nitakuoa utakapokuwa tayari
Miriam:
nishushe watu wanaweza kuja
Jeremy:
sioni vibaya kumwambia kila mtu kuwa wewe ni mke wangu mtarajiwa
Miriam:(anacheka kidogo) okay najua kuwa huoni
vibaya ila naomba nishuke please
Jeremy:
okay darling(anamshusha)
Miriam:(anakaa
kwenye kiti)
Jeremy:(anavuta kiti na kukaa pembeni ya Miriam)
siamini my love kama hatimaye umenikubali…unajua umenisumbua sana…yaani wewe
muone
Miriam:(anacheka) kawaida tu
Jeremy:
I will make you the happiest woman in the world…I will surely marry you
Miriam:(anajisemea moyoni) iam sorry
nakudanganya ila sitaki ujiue Jeremy kisa mimi halafu nionekane mimi ndo chanzo
cha kifo chako, ninaumia kuwa nina msaliti dada yangu
Jeremy:
najua kuna kitu unawaza…na ninajua kuwa unawaza kuhusu dada yako Ariana…labda
sijakuambia kitu…mimi na Ariana tumeachana muda mrefu sana…yaani tangu nimeanza
kukufukuzia, alikubali na kusema kuwa atawaambia wazazi wake
Miriam:
usingemuacha, ungeendelea kuwa nae tu hata kwa kujifanyisha
Jeremy:
siwezi
Miriam:
dada yangu…ataumia sana… (Anaanza
kukasirika)
Jeremy:
no baby usikasirike okay nitarudiana nae Kwa kujifanya tu najua tutakuwa
tunaudhulumu moyo wake ila kwakuwa pia najua hiyo itakuwa raha moyoni mwako
Miriam
:( anajisemea moyoni tena) yaani huu
mchezo sijui utakuja kuishiaje tu
Jeremy:
nini tena?
Miriam:
hamna mbona mimi nipo sawa kabisa?
Jeremy:
yaani naona una mawazo kweli... (Anamsogelea)
please Miriam this is our lives hatutakiwi kuwaza wengine watafikiriaje
Miriam:(katika hali isiyo ya kawaida anamuona Jeremy
ni wa tofauti sana, anaanza kumuangalia vingine)
Jeremy:
I swear nitakupenda na kukutunza sana…nitakupa chochote utakachotaka na mwisho
nitakuoa
Miriam:(anamuangalia usoni huku anajisemea kitu
fulani kichwani mwake) namuonaje? mbona naanza kumpenda? Mungu wangu this
is wrong…
Jeremy:
baby, you don’t have to worry about anything… (anaibusu mikono yake) nakupenda Miriam
na utaona tutakavyokuwa na raha baby…utaenjoi
Miriam:
okay haina shida… (anajisemea moyoni)
mbona najichanganya?
Jeremy:
umekaa kimya najua unamuwaza Ariana sana…ok nitakuwa nae ila I promise
nitatunza penzi letu
Miriam:
okay(ananyanyuka)baadae
Jeremy:
una haraka ila naelewa kuwa unataka kuwahi chuoni…tutakula dinner pamoja au sio
Miriam:
nitakuambia…
Jeremy:(anamshika mkono) mawasiliano ndo nguzo yetu,
najua itakuwa ngumu kwetu, ila naomba tujitahidi kuwasiliana baby
Miriam:
okay
Jeremy:
i love you baby
Miriam:
I love you too (kisha anatoka)
Jeremy :( anabaki anashangilia sana) yes…finally nimempata…ni wangu
sasa..nimepata mke(anajitupa sofani huku
anashangilia kama mwendawazimu)I love her so much…leo nitaenda kwa baba na
mama na kuwaambia kuwa nampenda sana Miriam na tayari tumeshakuwa wapenzi maana
amenikubali na Oh My God!!!au naota?hii itakuwa ndoto…amka Jeremy ni muda wa
kuamka…Oh My God,I can not believe ni kweli…kumbe Mungu unajibu maombi sana
unajua ee(anasimama yaani kwa kifupi
hatuliii)najua nimetumia njia ya udanganyifu kumpata Miriam ila ukweli ni kwamba nampenda
sana huo ndo ukweli,sasa maisha yamekuwa maisha sasa,yamekuwa na maana
kabisaaaaaaaaa…maana nimempata wangu wa ubani…I will take care of her
forever…nitamsomesha,nitamtunza,nitamjengea nyumba,nitamsubiri mpaka
atakapokuwa tayari nitamuoa I swear atakuwa malkia wa himaya yangu..yes(anachukua simu yake na kuingia katika
akaunti ya Miriam ya Instagram na kuanza kuangalia picha zake)wow look at
my girlfriend,she is just so beautiful(anabusu
moja ya picha za Miriam)my wife..(Anarudi
kukaa kwenye kiti chake cha kuzunguka) nitaikuza hii picha na kuiweka hapa
mezani...Kwangu (anatabasamu kidogo)
0 Comments