SCENE 15: -
(Ni usiku, kila kitu kipo kimya
kasoro sauti za wadudu waliao usiku, Jeremy yupo nyumbani kwake, ametulia
anapata kinywaji chake huku anaangalia mpira kupitia runinga yake kubwa iliopo
katika sebule yake ya kifahari)
Jeremy:(anatabasamu kidogo) iam so happy,
finally Miriam ni wangu… (anacheka kidogo)
sitaruhusu kitu chochote kiharibu furaha nayoisikia sasa hivi…sio wazazi wangu,
sio wazazi wa Miriam na sio Ariana (anakunywa
kinywaji kidogo) Ariana anatakiwa akubali kuwa siwezi kumpenda yeye kama
ninavyompenda Miriam (anachukua simu) ngoja
nimpigie kipenzi changu, tangu nilivyomuona asubuhi sijamuona tena(anapiga)
(Simu inaita)
Miriam:(anatoka kuoga, anaichukua simu kisha anaipokea)
hello
Jeremy:(sauti nzito Zaidi) baby? umelala?
Miriam:no
sijalala
Jeremy:
unafanya nini?
Miriam:
ah nipo tu nimetoka kuoga
Jeremy:
okay…mi naangalia mpira hapa, nikaona sio mbaya nikusalimie
Miriam:(anacheka kidogo) asante sana
Jeremy:
nimekumisi sana. sijakuona tangu asubuhi ulipokuja kunipa habari njema
Miriam:(anatabasamu) hata mimi nimekumisi(anajishangaa)
Jeremy:
kweli?
Miriam:
sikudanganyi
Jeremy:
asante honey…nataka nikulipie chuo
Miriam:
No Jeremy…
Jeremy:
kwanini?
Miriam:
kumbuka haya mahusiano ni siri kubwa sana…nadhani nilikuambia
Jeremy:
nakumbuka umeniambia yawe siri lakini je unadhani yatakuwa siri milele?
Miriam:
kwa sasa hivi naomba usinifanyie chochote…
Jeremy:
usinifanyie hivyo Miriam...
Miriam:
tulikubaliana leo asubuhi kuwa itakuwa siri…kumbuka wewe unachukuliwa kuwa ni
mkwe yaani mchumba wa Ariana…maana hata kama umeachana na Ariana bado Ariana
hajatuambia sisi kama familia
Jeremy:
okay…Ariana akiwaambia je utaniruhusu nikulee kama mke wangu mtarajiwa
Miriam:(anakaa kimya)
Jeremy:
naomba jibu...utaniruhusu?
Miriam:
uhusiano wetu, ni forbidden passion
Jeremy:
ukimaanisha nini?
Miriam:
haturuhusiwi kuwa pamoja hata iweje…maana hata baba na mama yangu hawataruhusu
yaani uachane na Ariana halafu uwe na mimi…kwanza haitaleta picha nzuri
Jeremy:
kwahiyo unataka kuniambia haya mahusiano yatakuwa ya siri milele hata ndoa yetu
itakuwa ya siri?
Miriam:
tutajua mbele kwa mbele
Jeremy:
sawa baby ilimradi tu usifikirie kuniacha
Miriam:
sitakuacha milele…nakuahidi
Jeremy:
nakupenda Miriam
Miriam:
nakupenda pia…(anacheka)
Jeremy:(anatabasamu) lala sasa…na mimi nitalala
mpira ukiisha
Miriam:
unaangalia mpira peke yako?
Jeremy:
ndio…
Miriam:
pole…
Jeremy:
ndo maana nataka uje tuwe tunaangalia wote
Miriam:(anacheka sana)
Jeremy:
umefurahi mwenyewe natamani ningekuwa hapo nishangae dimples zako
Miriam:(anatabasamu)
Jeremy:
haya bwana usiku mwema
Miriam:na
kwako pia
(Kwa pamoja wanakata simu)
Miriam:
mimi nimekuwaje? mbona kama nipo serious nampenda Jeremy? au nimempenda Mungu
wangu na baba yake aliniambia nijifanye kumpenda mbona kama nampenda kweli?
nampenda Jeremy…yes nampenda kweli kabisa
(Upande wa Jeremy)
Jeremy:
nitafanya kila kitu kulitunza hili penzi, sitaruhusu mtu yeyote avuruge hili
penzi…sio wewe mwenyewe Miriam maana naona kama unasita kwa mambo Fulani (anajikuta anashangilia mpira ghafla)
GOOOOOOOOOOOOO!!!ushindi mara mbili… (anapiga
makofi) mwanamke niliyemfatilia muda mrefu sasa nipo nae na hawa jamaa
wamenisuuza roho yangu loh!!!mambo ni motoooooooooo
(Upande wa Miriam, anamaliza
kuvaa nguo zake za usiku na kujilaza kitandani)
Mary:(anagonga mlango wa chumbani kwa Miriam)
hodi...
Miriam:
karibu ma mdogo
Mary:(huku anaingia) asante mwanangu…vipi haujalala
(anakaa pembeni yake)
Miriam:
nimetoka kuoga...sasa hivi
Mary:
leo umechelewa kuoga…
Miriam:
ah nimeoga mara mbili …nilikuwa nimelala sasa usingizi ukawa hauji ndo nikaamka
kuoga tena
Mary:
unakosa usingizi mwanangu
Miriam:(anaitikia kwa kichwa ishara ya kukubali)
Mary:
una mawazo gani?
Miriam:
ya masomo yangu…
Mary:
soma mwanangu
Miriam:
nasoma ma mdogo
Mary:(anatabasamu)
Miriam:(anamuangalia usoni) halafu ma mdogo
mbona tunafanana hivi?
Mary:(anashtuka sana)
Miriam:
unajua mimi natakaga kukuuliza sema huwa nakosa muda na nafasi
Mary:(anajichekesha) itakuwa kwa sababu
tunapendana labda
Miriam:
kwahiyo watu mkipendana mnafanana? kwahiyo nitafanana na Jeremy?
Mary:(anashtuka) unasemaje?
Miriam:(anajishtukia) sijasema chochote
Mary:
Jeremy ni nani yako?
Miriam:
kuna kaka anaitwa Jeremy darasani kwetu
Mary:
mnapendana?
Miriam:
huwa tunataniana
Mary:
soma mwanangu sawa mama…lakini pia mheshimu Jeremy ni shemeji yako sawa ee
Miriam:
sawa ma mdogo
Mary:
haya usiku mwema (ananyanyuka na kuondoka
zake)
Miriam:
namheshimu vipi Jeremy huku nafsi yangu imeshampenda…nampenda na wala simuoni
tena kama shemeji yangu, nimeanza kuota kuolewa na Jeremy… (anakaa kimya kidogo)
hivi mimi nina akili kweli...eti jamani nampenda shemeji yangu…kama kumpenda
Jeremy ni kosa niko tayari kuhukumiwa hata kifungo cha maisha...Nampenda Jeremy
(Upande wa Jeremy)
Jeremy: nampenda Miriam…nipo
tayari kwa lolote, iam ready hata nipigwe vibaya na mzee Ken ila tu niwe na
Miriam she is my everything
0 Comments