MUNGU MKUU 21


 

SCENE 21: -

(Majira ya saa nane mchana, upepo mwanana unavuma, Jeremy na Miriam wamekaa katika mgahawa mmoja wa kifahari wanapata chakula cha mchana huku kila mmoja akifurahia hali ya hewa ya wakati huo)

Jeremy: wow napenda hali hii ya hewa, it’s beautiful (anaachia tabasamu)

Miriam:(huku anakula) of course ni nzuri sana hata mimi napenda sana hali hii (anacheka kidogo)

Jeremy:(anatabasamu) Miriam wewe ni mzuri sana

Miriam:(anacheka kwa aibu kidogo) umeanza kwani tunaongelea uzuri wa nini si wa hali ya hewa?

Jeremy:(anacheka) basi tu nimeona niingize ya urembo wako…kwani nimefanya kosa?

Miriam: okay bwana tuendelee kula...

Jeremy:(anakula kijiko kimoja) nataka nikuoe…

Miriam:(anacheka kidogo) mara hii? mbona mapema

Jeremy: mapema? (anacheka kidogo) hapana sio mapema…bwana mimi tangu nimekuona nimekuwa na wazo la kukuoa kwahiyo sio mapema

Miriam: Jeremy…mimi bado mwanafunzi na isitoshe ndo kwanza nina miaka 18 acha nile ujana kwanza

Jeremy:(anacheka) wewe mtundu...kwani ukiwa mke wangu hutakula ujana?

Miriam:(anacheka) sasa nitakulaje ujana huku nitakuwa mke wa mtu

Jeremy:si tunakula ujana wote hata mimi nataka kula ujana mbona?

Miriam:no baby…tusubiri

Jeremy: honey...mbona wewe kila kitu hutaki? Unajua sikuelewi eeh

Miriam: nimekataa nini tena jeremy?

Jeremy:(anacheka) si umekataa gari?

Miriam: jamani Jeremy...siwezi kupokea gari...unajua nitaulizwa sana nyumbani

Jeremy: unawaambia la Vanessa

Miriam: siwezi kudanganya hivyo maana wanajua maisha yake

Jeremy:si atasema kuwa amepewa na bwana ake

Miriam:(anacheka) yaani wewe…

Jeremy: kwahiyo nitakuletea gari mpenzi

Miriam:mi naogopa Jeremy

Jeremy: usijali nitaongea na vanesa nitamfundisha cha kusema...nataka uwe na gari litakalokuwa linakupeleka popote unapotaka my soulmate, sitaki udhurure njiani kwa miguu wataniibia

Miriam: hapo sasa ndo watu watashangaa…kunipeleka kila napotaka? By the way sidhururi kwa miguu nyumbani kuna gari

Jeremy: najua nataka tu uwe na gari Mirriam la kwako wewe kama wewe

Miriam:(anaguna) anyways, hilo gari liko wapi?

Jeremy: gereji kwangu, nyumbani kwangu

Miriam: Jeremy una utani…si wanajua magari yako

Jeremy:ni jipya--- relax baby usiogope hakuna aliyewahi kuliona…mpaka dereva yupo

Miriam: (anashangaa) wewe Jeremy wewe?

Jeremy: mwanamke…tutasema ni dada yake Vanessa

Miriam: (anatabasamu) haya mimi sina cha kusema umeshaamua…

Jeremy: okay baby…asante kwa kupokea zawadi zangu next itakuwa nyumba

Miriam: (anashangaa) wewe Jeremy?

Jeremy: you are my wife baby…lazima nikupambe na nikutunze

Miriam:(anatabasamu) asante baby

(simu ya Miriam inaita)

Miriam:(anaiagalia simu yake) ma mdogo(anapokea)hello ma mdogo

Jeremy:(anataka kuongea)

Miriam:(anamuwekea kidole mdomoni ishara ya kumnyamazisha)

Mary: Miriam uko wapi si umemaliza masomo yako saa saba sasa hivi ni saa nane na dakika kadhaa…uko wapi?

Miriam:(anashikwa kigugumizi) ah---- ah …nipo nakula na Vanessa…

Mary:mpe simu niongee nae

Miriam:(anashikwa kigugumizi) wewe Vanessa (anaendelea kuongea na simu) ma mdogo Vanessa kaenda chooni

Mary: akirudi nipigie…

Miriam:ma mdogo jamani mbona hivyo? huniamini?

Mary: Miriam nimekuona mara nyingi sana una ukaribu na shemeji yako mchumba wa dada yako Ariana

Miriam: sipo na Jeremy mbona, wasiwasi wako tu ma mdogo

Mary: haya mama kuwa makini usije ukajiingiza kwenye matatizo

Miriam: usijali ma mdogo...

(Wanakata simu)

Jeremy:(anaguna) hivi wewe una mahusiano gani na mfanyakazi wenu yule Mary sijui ndo mnamuita ma mdogo

Miriam: mahusiano kivipi?

Jeremy:mi naona mnafanana kweli

Miriam: halafu watu wengi wameniambia hivyo mi mbona sioni kama nafanana nae? anyway mi sijui nachojua ni kwamba mfanyakazi wetu ila tunampenda kama ndugu basi hivyo tu mengine sijui kwakweli

Jeremy: kama ni hivyo sawa ila fatilia (anacheka)

Miriam: (anacheka) anyways, mi nimeshamaliza kula…naona mwenzangu bado unajivuta

Jeremy: nataka nikae na wewe…muda mrefu…napenda kukuangalia (anacheka)

Miriam:(anacheka kisha anaguna) yaani wewe unajua hatuwezi kufanya hivyo, umeona hapa tu nimeshapigiwa simu ya kuulizwa

Jeremy: yatapita tu baby ipo siku tutakuwa pamoja kwa Amani na uhuru

Miriam: dah sijui itakuwaje siku hiyo…baba ataniua

Jeremy: hapana…nina Imani ataelewa…

Miriam: sijui tu

Jeremy: hivi unajua wazazi wangu mara ya kwanza walichukulia kama kunisaidia tu ili nisijidhuru ila kwa sasa wanasema nikuoe wewe…wanani sapoti

Miriam: bora yako…unajua kwa wazazi wangu bora usingekuja kwa ajili ya kumuoa Ariana

Jeremy: tunapanga ila Mungu ana mipango yake labda Mungu alikuwa ananisukumia kwenu ili nikutane na wewe…Miriam sikupanga kwamba nikija kwenu nikupende wewe…wazazi wangu wanaelewa nina Imani na wazazi wako wataelewa tu tuwajaribu…tuone

Miriam: tujaribu mapema maana hapa tunachofanya ni usaliti na inaniumiza

Jeremy: naelewa my queen…nitamwambia mama na baba wakavunje uchumba wangu na Ariana baada ya hayo basi tutawaambia

Miriam: umeniambia kuwa umevunja uchumba na Ariana

Jeremy: yes, baby nimevunja, kwanini unaniuliza?

Miriam:(anacheka kidogo) unajua aliniambia niongee na wewe kuhusu wewe nay eye kurudiana…halafu badala yake nipo hapa nina mahusiano na wewe kwakweli najisikia vibaya sana unajua

Jeremy: najua...mpenzi mimi na wazazi wangu tunajiuliza tuombe vipi msamaha kwa hili…na jinsi tunavyochelewa ndo mambo yanazidi kuwa magumu...Wazazi wangu wanatamani hata sasa hivi waje kwenu na kusema kuwa nakupenda wewe na sio Ariana ila wanaogopa wazazi wako watasema…pamoja na hayo mimi naamini tukijaribu wataelewa

Miriam: embu tusiyawaze hayo…nipeleke nyumbani kabla mama hajanipigia(ananyanyuka)

Jeremy:(huku ananyanyuka) sasa mtu mwenyewe muoga...nakufikishaje nyumbani

Miriam: unanishushia mbali…

Jeremy: okay...kesho gari lako litakuja (ananyanyuka anamshika mkono Mirriam kisha wanaondoka)

Post a Comment

0 Comments