MUNGU MKUU 22


 

SCENE 22: -

(Asubuhi ya kesho yake, kuna gari zuri sana linafika nyumbani kwa kina Miriam, ndani ya gari hilo kuna dereva mwanamke, na Vanessa)

Miriam: wow, gari zuri sana

Vanessa: ingia twende mwenzangu wasije wakatoka wakanipa maswali hapa nikashindwa kuyajibu

Miriam: tulia mtoto… (analishangaa gari) yaani Jeremy ana mambo huyu(anacheka)

Vanessa: jamani...twendeni nyie

Dereva:(anacheka) si anakupenda…mwenzio anakupenda kweli mwenyewe anasema wewe ndo mkewe

Vanessa: jamani twendeni

Miriam: okay twendeni

(Wanapanda gari)

Keddy: (anatokea ndani) hamjambo?

Vanessa: eeh makubwa…yamenikuta

Vanessa: hatujambo mama shikamoo

Dereva: shikamoo

Keddy: marahaba, hamjambo (anawaangalia kisha anaangalia gari) gari zuri sana…halafu linaonekana la thamani…la nani?

Miriam:(anadakia) la Vanessa…

Keddy:(kwa mshangao) la Vanessa?

Vanessa: huyu Miriam bwana hili gari ni la dada yangu…sasa ameona awe anatupa lifti ya kwenda chuo…ili tupunguze gharama za nauli

Dereva: ndio ni langu nawaonea huruma ndo nimeona niwe nawapa lifti kwa kipindi nikiwepo

Keddy: wewe unafanya kazi wapi? Maana dah!!! Gari la thamani sana hili

Dereva: mimi nipo Nairobi nafanya kazi huko

Keddy: wewe ni dada yake kabisa?

Dereva: mimi ni mtoto wa mama yake mdogo

Vanessa: eeh ma mdogo…(anajichekesha)

Keddy: basi sawa haina shida...nendeni chuo mtachelewa

Vanessa: haya...Mama…baadae

Keddy: baadae

Miriam: bye mama

Keddy: bye baby

(Wanaondoka)

Vanessa:(anashusha pumzi) yaani wewe na mumeo mtakuja kuniletea balaa wallahi

Miriam:  embu tulia huko kwanza yameisha jamani ee (anacheka)

Dereva:(anacheka)

Vanessa: yaani Jeremy aliponiambia nije nidanganye alikuwa anasema kirahisi kweli

Miriam: sehemu ngumu ni ile mwanzoni ila sasa kila kitu kipo sawa…mama amejua kuwa wewe ndo mwenye gari

(Wanacheka)

Vanessa: sio mimi gari ni la dada yangu…umesahau?

Miriam: oh yes…nilikuwa nimesahau

Dereva: usishau maana mama yako anaonekana ana maswali jamani…(anaguna)

Miriam:(anacheka)

(Simu ya Miriam inaita)

Miriam:(anapokea) baby

Vanessa: eeh…mwambie nimetoka jasho atume hela ya soda

Miriam:(anacheka) jamani

Jeremy: mambo…

Miriam: poa…shikamoo

Jeremy: marahaba…ni matumaini yangu mpo njiani mnaenda chuo

Miriam: yes…baby nimeona gari daddy asante ni zuri

Jeremy: usijali just for you my love…umelipenda?

Miriam: vibaya sana

Jeremy: tell me about it babe, mama au ma mdogo wameliona?

Miriam: wewe mama ameliona tumejiumauma wewe (anacheka) ila tumeeleweka

Jeremy: sasa je ulikuwa unaogopa…kifuatacho ndoa

Miriam:(anashangaa) He--- jamani ...unataka niuliwe mimi eti?

Jeremy: hufi bwana wataelewa

Vanessa: mwambie nataka hela ya soda nimetoka jasho sana

Miriam:(anacheka) msikie Vanessa… (anampa simu Vanessa)

Vanessa: baby ake…hela ya soda ndugu yangu maana sio kwa jasho

Jeremy: utaona mpesa imethibitishwa hapo...

Vanessa: asante baby akeeee

Jeremy: (anacheka) mwehu wewe (anacheka tena) haya poa…

Vanessa: shika simu yako (anamrudishia simu Miriam)

Miriam: nambie

Jeremy: I love you…do you love me?

Miriam: yes

Vanessa: yes, nini si useme I love you too

Miriam:na wewe ni Mbeya…

Vanessa:(anacheka)

Jeremy: tell me baby…

Vanessa: mwambie

Miriam:(anacheka kwa aibu)

Vanessa: mwambie sasa

Miriam: yes, baby I love you

(Wanafurahi)

Jeremy: asante baby...leo siku yangu itakuwa nzuri sana natumaini na yako itakuwa nzuri kama yangu

Miriam: lazima iwe nzuri

Jeremy: we are soulmates baby...na sijui kwanini sikukuona mapema hata njiani nije nikuchumbie badala ya dada yako…

Miriam: umeanza sasa kuleta stori za Ariana baby unajua nikisikia Ariana najisikia vibaya maana nampenda sana dada yangu na dada yangu anakupenda sana wewe jamani…tusiwe tunamuongelea tukimuongelea tu najishisi kuachana na wewe

Jeremy: basi poa nisamehe…sitaki kukuudhi…

Vanessa: wacha we…huko kudeka vipi?

Miriam:(anacheka) ila Vanessa nini lakini?

Jeremy: tukutane lunch…sasa hivi una gari sitaki kuwa nakuja chuoni mara kwa mara

Miriam: palepale pa jana?

Jeremy: yes…

Miriam: ok

(Wanakata simu na safari ya kuelekea kwenda chuo inaendelea)

Post a Comment

0 Comments