SCENE
23: -
(Jioni
nyingine njema tena yenye kupendeza machoni pa Mungu na kwa wanadamu, jua
linaanza kuzama na kila kitu kinaonekana kutaka kupata pumziko baada ya siku ndefu,
Ariana anafika katika jumba la kifahari la mfanyabiashara kijana Jeremy)
Ariana:(huku
anashuka kutoka kwenye gari) leo nataka kumpa surprise ya maisha huyu mwanaume
(anachukua boksi kubwa na kuanza kutembea) mpaka asipate tena wazo la
kutaka kuniacha mimi (anaangalia gari ambalo analifahamu) hili si ndo
gari linalomleta Miriam siku hizi linafanya nini huku? (anapiga tena hatua)
eeh (anauelekea mlango na kuufungua akiwa na lengo la kumfurahisha Jeremy)
(Anamkuta
amemkumbatia Miriam)
Ariana: (kwa
mshangao) Jeremy?
Jeremy:(anamuangalia)
Ariana:na
mdogo wangu?
Miriam:(anaogopa
sana)
Jeremy:
Ariana listen, and iam so sorry hata mimi nilijitahidi sana kupigana na hisia
zangu nimeshindwa nampenda sana Miriam ni mwanamke ninayetaka kumuoa
Ariana:(machozi
yanamlenga) this cant be…please tell me it is a dream (analia)
Jeremy:
usitoe machozi Ariana…mbona nilikuandaa kwa hili jamani?
Ariana:
najua uliniandaa mapema sana Jeremy lakini hukuniandaa kwa hili…katika wote
umemchagua Miriam? Jeremy jamani
Jeremy:
iam so sorry Ariana…hata hivyo mbona mahusiano yetu hayakuwa ya karibu sana?
Ariana:(machozi
yanamwagika) Jeremy nakupenda, jamani kwanini lakini?
Jeremy:
sasa kwanini nini? mimi sina jibu la swali lako Ariana tulizungumzia hilo tena
mara nyingi sana
Ariana:
najua ni mara nyingi sana tulizungumzia hilo ila hatukumuongelea Miriam
Miriam:(anaonyesha
wasiwasi)
Ariana:(kwa
Miriam) kama ilivyo kawaida yako umenizunguka Miriam
Miriam:
sio kweli dada…nilijaribu sana…ila...
Ariana:
kimya…kimya sitaki kusikia chochote Miriam… (anafuta machozi kisha anatabsamu)
usijali mdogo wangu unadhani nimekasirika…nimefurahi sana tu kuwa na wewe
umepata boyfriend hongera sana Jeremy is nice guy
Miriam:(anashangaa)
really? Are you sure? (anazidi kushangaa)
Ariana:(anafuta
machozi) nilikuwa tu najifanya kukasirika baada ya kukuta hivi
Jeremy:
are you sure? I mean are you serious?
Ariana:
yes…iam serious
Jeremy:
hujachukia?
Ariana:
nachukia nini sasa huku Miriam ni mdogo wangu akipata kitu kizuri na mimi
nimepata… si ndio baby sister?
Miriam:
dada(anamkumbatia)asante sana dada yangu…nakushukuru sana...
Ariana:
usijali sana mama... (anaweka boksi mezani) enhe mmeshawaambia wazazi?
Jeremy:
wazazi wa pande moja ndo wanajua… (anacheka kidogo) upande mwingine hawajui...ila
tutawaambia
Ariana:
waambieni bwana mapema ili wajue tule wali sie
(Wanacheka)
Jeremy:(kwa
Ariana) yaani siamini kama umekubali shemeji yaani nilivyokuwa nakuwazia ni
tofauti kabisa na ulivyoonyesha
Ariana:
kwanini jamani?
Jeremy:
basi tu nilihisi hivyo kutokana na hali yenyewe… (kwa Miriam) my love
umesikia sasa tupo watatu tutatetea huu uhusiano
Ariana:
mkitaka nitamwambia baba na mama kuwa mnapendana najua watakubali tu...wanampenda
sana Miriam na watamfanyia kila kitu…Miriam is such a lucky girl kila kitu
kizuri anapata yeye upendo wa wazazi na mwanaume mzuri kama wewe Jeremy
Jeremy:
hata usiseme hivyo shemeji mbona hata wewe wazazi wako wanakupenda sana? na pia
huu sio mwisho mimi sikuwa tu mwanaume ambae Mungu amekupangia nimefurahi tu
jinsi ulivyoochia mapema hivyo…sasa namuomba Mungu akusaidie na wewe upate
mwanaume mzuri sana shem na tule ubwabwa kabla ya Miriam
Ariana
:( anaguna) eti eeh
Jeremy:
ndio
Miriam
:( anaonyesha furaha)
Ariana:(anatabasamu)
Jeremy:by
the way (anaangalia boksi) umeleta nini humo embu tufungue ulikuwa umeniletea mimi…
(kwa Miriam) naomba tufungue box shemeji ametuletea zawadi
(Jeremy
na Miriam wanafungua box)
Jeremy:
wow…bonge la keki
Ariana:(anawafuata)
kama nilijua nitawakuta wawili
Jeremy:(anaangalia
ilivyoandikwa) I love you, Jeremy?
Ariana:
sasa hapo iangalie hivi kwamba Miriam ndo amekuletea
Jeremy:
good idea (kwa Miriam) eti unaonaje baby
Ariana:
halafu nimeona gari hapo nje hilo gari huwa linamleta Miriam nyumbani ni la
nani?
Jeremy:ni
la Miriam nilimnunulia
(Maneno
ya Jeremy yanajirudia mara nyingi sana kichwani kwa Ariana)
Miriam:
Jeremy
Jeremy:(anatabasamu)
nini, Ariana yupo upande wetu…ni msiri wetu mpaka pale tutakapoamua kuwaambia
wazazi si eti Ariana?
Ariana:
bila shaka kabisa
Jeremy:(kwa
Miriam) anza kujifunza kuwa mke kalete kisu na sahani tukate keki tule
Ariana:(anaangalia
saa)mi naona niwaache kuna sehemu nawahi(anaondoka bila kusikia chochote)Mungu
wangu(Anatoka nje)wanadhani nimekubali (anatabasamu tabasamu la kiovu)sijakubaliana
nao…Miriam atajuta kwanini aliamua kunisaliti na maisha yake yatakuwa mabaya
kuliko zamani nitamfanyia kitu mbaya mpaka dunia itikisike…pendaneni Miriam na
Jeremy pendaneni sana maana muda wenu wa kupendana unakaribia kuisha..pendaneni
Zaidi na Zaidi…nitakurudia Jeremy…utakuwa wangu peke yangu…(anacheka kiovu)nikimuua
Miriam hata wazazi watakulazimisha kunirudia mimi halafu tutafunga ndoa
nitakuwa malkia wa himaya yako na mali zako zote.. zitakuwa zangu nitaringa mie
(anacheka kisha anaingia kwenye gari lake analiwasha kisha analiondoa)
(Huku
ndani walipo Jeremy na Miriam)
Miriam:
nimeshangaa dada alivyochukulia poa mahusiano yetu
Jeremy:
mimi nimepagawa…
Miriam:
ila sijapenda ulivyo mwambia kuwa lile gari ni langu
Jeremy:
kwani uongo Miriam?
Miriam:
haikuwa kitu kizuri mtu baada ya kupokea mshangao wa maisha umuongezee jambo
lingine
Jeremy:
acha uoga…bwana. enhe ulikuja kuniambia nini? maana dada yako alikuja ndo
kwanza ulikuwa unaingia ndo maana ametukuta tunakumbatiana (anacheka)
Miriam:
kuna tour chuoni nadhani wikiendi hii kuna mengi ya kujifunza ila naona uvivu
kwenda
Jeremy:
kisa?
Miriam:
nitakuwa peke yangu
Jeremy:
Vanessa je?
Miriam:
haendi
Jeremy:
nenda tu baby si ni kujifunza?
Miriam:
ndio
Jeremy:
nenda tu nitakusindikiza mpaka mtakapopandia gari
Miriam:
haya bwana kwakuwa umesema wewe ngoja nitaenda
Jeremy:
that’s like my girl(anatabasamu)
(Wanatabasamu huku wanaendelea kumega keki taratibu)
Jeremy:
I love you(anatabasamu)
0 Comments