MUNGU MKUU 24


 

SCENE 24: -

SIKU YA TOUR: -

(Asubuhi nyingine njema mbele ya macho ya watu na Mungu wa mbinguni aliyeifanya hivyo, wanachuo mbalimbali wamefika chuoni tayari kwa ajili ya kuondoka kuelekea tour kwa ajili ya masomo yao. Jeremy na Miriam wanafika mahali hapo pia)

Jeremy: baby nitakumisi sana unajua

Miriam:(anatabasamu) narudi kesho tu hapa…

Jeremy: siku moja bila wewe kiukweli kabisa sitaweza…

Miriam: come down baby…simu zipo nitakuwa nawasiliana na wewe kila mara don’t worry

Jeremy: simu tu haitoshi baby…nimezoea kukuona kila siku na kila saa

(Wanacheka)

Miriam: wewe tulia tu bwana nikirudi tu nakuja kwako halafu ndo naenda nyumbani ingawa (kuna kitu anafikiria ghafla)

Jeremy: nini tena? Mbona umekuwa myonge ghafla?

Miriam: nakosea sana Jeremy yaani nakosea kuwa na wewe

Jeremy: umeanza baby mbona hata Ariana ameshakubaliana na uhusiano wetu kwani nyumbani jana ulipoenda walikuambiaje?

Miriam: hawakusema chochote ingawa ma mdogo Mary anatuhisi na huwa ananiambia nikuache

Jeremy: oh (anamshika kidevu) sasa najua kwanini unakuwa na mawazo unamsikiliza sana ma mdogo

Miriam:ma mdogo ananipenda sana nimepewa hadithi kuwa alininyonyesha nilipokuwa mchanga

Jeremy: kwanini sasa yeye akunyonyeshe?

Miriam: mama yangu hakuwa na maziwa ya kutosha na ma mdogo alikuwa ametoka kujifungua wakati huo

Jeremy: mtoto akaenda wapi?

Miriam: alikuwa si riziki

Jeremy: maskini basi ndo maana anakupenda anaona wewe ni mwanae kabisa

Miriam: sasa hataki hata kidogo kusikia nina mahusiano na wewe

Jeremy: ah atazoea tu kwani sisi tulipanga kupendana si imetokea tu?

Miriam: najua imetokea tu ila huoni kuwa ni kosa?

Jeremy: huwa unaniudhi hapo hapo mke wangu yaani wewe unawaangalia sana hao ishi maisha yako

Miriam: unanifundisha vibaya (anacheka) sitakiwi kuwa na wewe

Jeremy: nitakusubiri mpaka utakapokuwa tayari nitakuja kwenu kukuchumbia nitakuoa na kuzaa na wewe vitoto virembo kama wewe vyenye tabia ya upole kama wewe

Miriam :( anacheka)

Jeremy :( anatabasamu)

(Rafiki mmoja wa Miriam anawaona)

Rafiki: wewe shuka humo huendi?

Miriam :( anashusha kioo) wewe nakuja

Rafiki: oh, kumbe upo na daddy?

Jeremy :( anashangaa kidogo) daddy???

Miriam: oh (Kwa Jeremy) wewe sio daddy wewe ni my boyfriend

Jeremy: daddy si sponser?

Miriam: baby anakutania jamani

Jeremy: oh… (Anatabasamu) niliogopa kweli nikaona ee naonwa sponser huku mi naona nimeshapata mke

(Miriam na rafiki yake wanaangua kicheko)

Miriam: jamani ee (anacheka)

Rafiki: Vanessa Leo yuko wapi?

Miriam: haji Leo hana hela

Rafiki: sasa wewe (kwa Miriam) si twende au?

Jeremy: bye baby (anambusu shavuni)

Miriam: bye honey

Jeremy:(anatoa kitita cha pesa na kumkabidhi) enjoy…(anatabasamu)

Rafiki: ukiitwa sponsa unakataa

Jeremy:ni wajibu wangu kumtunza nisipomtunza mimi nani atamtunza?

Rafiki: kweli mwaya wanasema abiria chunga mzigo wako

(Wanacheka)

Miriam:(anakumbuka kitu) je nikimuita Vanessa nimlipie nitakuwa nimechelewa?

Rafiki: utakuwa hujachelewa mlipie tu

Miriam: nitafanya hivyo… (anatoka kwenye gari) bye baby

Jeremy: bye take care mpenzi wangu (anabusu viganja vyake kisha anampeperushia)

 Miriam:(anambusu)

(Jeremy anaondoka)

Rafiki: mpenzi wako anakupenda kweli jamani hadi raha

Miriam: kawaida tu mbona

Rafiki: nasikia amekununulia gari na yuko mbioni kukununulia nyumba

Miriam: yaani nyie wambea…wewe nani amekuambia?

Rafiki: jamani mbona hiyo inasikika sana tu

Miriam: najua itakuwa Vanessa huyo yaani na yeye ni mdaku

Rafiki: jamani rafiki yangu mimi si rafiki yako naanzaje kukosa kujua mambo yako?

Miriam: Naila jamani una mamlaka ya kujua mambo yangu wala sijasema hutakiwi kujua…unatakiwa kujua sana tu

Naila:(anatabasamu) ndo hivyo rafiki yangu tunajua kabisa kuwa jamaa ana mpango wa kukuoa na kuishi na wewe

Miriam:(anacheka) Naila bado nasoma siwezi kuchanganya hayo mawazo kwanza…

Naila: ah wewe nae mbona watu kibao wanasoma huku wapo kwenye ndoa zao na wako kawaida na maisha yanaendelea tu kama kawaida

Miriam: eti mimi naona ni mbaya hiyo naona haijatulia hata kidogo

Naila: acha ushamba bwana…unless Kama unataka kuzini…au tayari mmeshaanza?

Miriam: Jeremy ameniambia kuwa atanisubiri

Naila: sasa hawezi kukusubiri kwa muda mrefu sana yeye ni mwanamume

Miriam: najua

Naila: ndo uolewe kabla haijawa vituko

Miriam: nitaolewa kwanza tumalize mambo yaliyopo hapo…wewe si unajua Jeremy alikuwa ni shemeji yangu alikuja nyumbani kwa ajili ya kumuoa dada yangu ndo akatokea kunipenda mimi kwanza nataka kwanza tumalize utata kwa wazazi kwanza halafu ndo mipango mingine ifate

Naila: nakuelewa shoga yangu ila una kazi

Miriam: acha tu ndugu yangu sijui litakuja kuishaje

Naila: kila kitu kitakaa vizuri usijali(anatabasamu)

(Dereva anapanda gari kisha anapiga honi kuita wanafunzi waingie kweye basi kwa ajili ya kuanza safari)

Naila: shoga twende tukawahi siti

Miriam: twende shoga yangu, ila Vanessa hajaja bado ingawa nimempigia simu

Naila: twende bwana...atatukuta

(Wanaelekea kupanda basi)

Dereva: mpo tayari (anaangalia nyuma kisha anawasha gari na kuliondoa)

Post a Comment

0 Comments