SCENE
28: -
USIKU
WAKE: -
(Majira
ya saa nne usiku Ariana anafika nyumbani kwao akiwa ni mtu mwenye furaha sana,
anapofika anawakuta wazazi wake wana wasiwasi sana)
Ariana:
shikamooni
(Wanamuitikia)
Ariana:
mbona hamna Amani kuna shida gani?
Mary: Miriam
hajarudi mpaka sasa hivi
Ariana
:( anacheka) za mwizi arobaini
Keddy:
una maana gani?
Ariana:
mnaniona mimi ndo mtenda dhambi wa nyumba hii (anajitupa kwenye sofa)
kumbe mtenda dhambi yupo amejivika ngozi ya kondoo kumbe ni mbwa mwitu katika
kundi la kondoo
Ken:
bado sijakuelewa embu ongea vizuri acha kuongea kwa mafumbo sipendi mafumbo
yenu
Ariana:
Miriam ana mwanaume
Ken:(kwa
mshangao) Mwanaume?
Ariana:
ndio ana mwanamume
Ken:
ameanza lini? na huyo mwanaume ni wa wapi?
Ariana:ni
Jeremy
(Wote
wanashangaa)
Mary:
Mungu wangu huyu mtoto
Ken:
Jeremy huyu mchumba wako?
Ariana:
ndio…anatoroka chuoni anaenda kwa Jeremy kila siku
Ken:(anashikwa
na hasira) Jeremy na Miriam wametusaliti sana hawa watoto…yaani sitaki
kumuona Miriam
Mary:
shemeji jamani…Miriam hana kosa kila mara Jeremy alikuwa anamlazimisha
Keddy:
ina maana ulikuwa unajua?
Mary:
nilikuwa nahisi tu dada
Ken:
kwanini hukumkataza huyu mwanaume?
Keddy:
jamani hawa watoto
Ken:
amenitia aibu sana huyu mtoto sikutegemea tena shemeji yake?
Keddy:(anamtuliza
mume wake) tulia baba…tulia
Ken:
naomba simu yangu mama Ariana...nitamtukana huyu kijana na sitaki tena aje
nyumbani kwangu…na mwanangu sitaki amuoe tena
Ariana:
baba mimi bado nampenda
Mary:(anashangaa)
we Ariana
Ariana:
ndio ma mdogo au nikuite mama Miriam
(Ken
na keddy wanapigwa butwaa)
Keddy:
mama Miriam kivipi?
Ariana:(anacheka)
jamani mbona mimi t undo wa kusema ukweli? Leo eeh (kwa mama yake) ndio mama ma
mdogo ni mama mzazi wa Miriam
Ken:(anashangaa)
Mary kwanini? yaani sielewi ilikuwaje?
Mary:(anabaki
mdomo wazi anakosa la kusema)
Keddy:
umenisaliti hata mimi Mary jamani? mimi si dada yako? mbona nilikupa nafasi
nzuri tu ya kuwa karibu na mimi
Mary:(anabaki
kimya)
Ken:
yaani ilikuwaje mpaka Miriam akafika mlangoni kwetu na wewe kuwa msaidizi wetu
wa kazi?
Keddy:
nakumbuka tulikutana na wewe wakati tunatoka kutoa taarifa juu ya kupatikana
kwa Miriam
Ken:
nakumbuka tulitaka kumgonga
Keddy:(anafikiria
kitu Fulani) na ndo maana ulikuwa unampenda sana Miriam...
Mary:(kimya
huku machozi yanamtoka kwa fujo)
Keddy:
kwanini Mary ulificha yote hayo? ungeniambia basi hata mimi iwe siri yangu tu
jamani ukaona umwambie Ariana
Mary:
ilitokea tu nimemwambia Ariana hata mimi nilipanga kukuambia wewe
Keddy:
ikawaje?
Mary:
nikaona sijui nini…nilihisi nikisema mwanangu atakosa sehemu ya kuishi
Keddy:
kwahiyo unataka kuniambia kuwa Miriam ni mwanao?
Mary:
ndio ni mwanangu dada (Analia)ni mwanangu wa kumzaa mwenyewe…ni maajabu
na ukuu wa Mungu alipata familia…
Ken:
mambo mengi kwa wakati mmoja mara huyo mwanao amemsaliti mwanangu (anajitupa
kwenye sofa kama mtu aliyechoka sana) nimechoka haki ya nani
Ariana:(anacheka
chinchini)
Keddy:
ukweli huu umenishangaza kwakweli...(anaguna)tumekaa na wewe miaka 18
hata kusema Mary
Mary:
nilikuwa nahofia mwanangu angekosa malezi mazuri nisameheni sana nimekosa
naombeni mnisamehe (anafuta machozi) naomba muendelee kumpenda mwanangu
kama mwanzo
Ariana:(anajisemea
moyoni) mwanao hayupo tena duniani yaani hapa wakati wowote kutakuwa na
habari kuwa mwanao amekutwa kafa (anacheka moyoni) oh nimeua ndege
wawili kwa jiwe moja Mary na Miriam out na hivi huyu Mary alikuwa hana akili
sijui ataishije?
Mary: nisameheni…kipindi
hicho sikuwa na uwezo wowote wa kumlea mtoto mwanaume aliyenipa mimba
hakunitaka tena, nyumbani nilikuwa nimefukuzwa…ningefanya nini…nikaona nije
nimuweke hapo nje kwenu na Mungu akawa mwema mkamuona na kumchukua mmelea kama
mtoto wenu kabisa…nimekuwa hapa nimeona upendo mnaomuonyesha Miriam…naomba
msimtupe nifukuzeni mimi msimfukuze
Ken:
Miriam amekosea kuwa na shemeji yake ila pamoja na yote Miriam ni mtoto wetu
tumemjua kwa miaka 18 sasa…tunampenda na wala hatutamfukuza pamoja na kutukosea
Mary:(anafuta
machozi) asanteni sana Mungu awabariki sana jamani…eeh Mungu unaendelea
kuonyesha jinsi ulivyo Mkuu, asanteni sana
Ken:
usijali ila kama kuna siri nyingine tuambie mapema…tu
Mary:
hakuna siri nyingine shemeji
Keddy:(anatabasamu)
usijali… kuwa na amani yataisha au yameisha
Ariana:(anajisemea
moyoni) yaani mimi nimekuja kusema hivi ili wazazi wangu wakasirike
wamfukuze huyu Mary badala yake wamemsamehe kirahisi hivi(anafyonza)I can’t
believe it…yaani kirahisi hata wazazi hawajatia neno sana na wala hawajashangaa...
(Anaguna)
Mary:
asanteni Sana ndugu zangu kwa kunisamehe kwa hili
Keddy:
usijali halikuwa kosa lako ni matatizo tu…
Ken:
sasa nyie endeleeni kuongea mimi namfuata Miriam kwa huyo Jeremy
Keddy:
ngoja nikusindikize mume wangu
Ken:
twende
(Wanaondoka)
Mary :( kwa
upole) mwanangu…mbona umeamua kuwaambia wazazi wako kuhusu Miriam?
Ariana :(
Kwa ujeuri) niliamua tu kwani kuna tatizo?
Mary: (anatabasamu
kidogo) unajua kwanini nilikuambia…? Nia yangu ilikuwa ni hiyohiyo uje
uwaambie maana nilishidwa kuwaambia nashukuru umenisaidia sana
Ariana
:( anafyonza) embu nitolee upuuzi wako hapa… (Anafyonza) halafu
usiniite Mimi mwanao…siwezi kuwa mwanao Mimi huna hadhi ya kuwa mama yangu
Mary :( anatabasamu)
sijui umechukua roho ya nani? (kwa upole) usipobadilika una hali mbaya
sana mwanangu…sijui utabaki na nani
Ariana:
nimekuambia usiniite Mimi mwanao husikii? (Anaondoka kwa hasira)
0 Comments