MUNGU MKUU 29


 

SCENE 29: -

USIKU HUOHUO

NYUMBANI KWA JEREMY: -

(Ken na mkewe wanafika nyumbani kwa Jeremy wakiwa wanaonekana kuwa na hasira na hamu ya kumuona Miriam)

Ken:(anapayuka) we Miriam

Jeremy:(anashtuka usingizini) nani tena usiku huu? (ananyanyuka kutoka usingizini anatoka moja kwa moja mpaka nje) baba?

Ken: usiniite baba wewe mtoto mimi sio baba yako unaelewa vizuri

Jeremy: shida nini? (anafikicha macho)

Ken :( Kwa jazba) Miriam yuko wapi?

Jeremy: una maana gani? Miriam hayupo hapa hajawahi kuja usiku hata siku moja

Keddy: baba tunajua mna mahusiano

Jeremy :( anaangalia chini kwa aibu)

Keddy: ndo maana tunaomba kama yupo mwambie aje wala hatutafanya chochote kwa mtoto wetu tutaenda nyumbani tutasahau ujinga wenu na kuendelea na maisha

Jeremy: mama ni kweli mimi na Miriam tunapendana…na ni kweli tupo kwenye mahusiano ila hatujafikia hatua ya kukaa pamoja mpaka usiku wa manane na isitoshe mimi na yeye hatujaongea tangu mchana…

Ken:(anamzaba kofi) huna haya na adabu unadiriki kusema wazi bila uoga kuwa unatembea na mwanangu mdogo baada ya kumchumbia binti yangu mkubwa?

Jeremy: baba hapa tunaongelea moyo baba

Ken: kelele…nitasahau kuwa wewe ni mtoto wa rafiki yangu…nitasahau kwamba wewe ni kijana na wa mzee wa kanisa mwenzangu…mnatutia aibu nyie watoto

Jeremy: baba naomba mtusamehe…ni moyo ndo uliamua kumpenda Miriam, mimi na yeye tulijikuta tunapendana tu pamoja na kupigana kinyume na hisia hizi

Ken: unanitia kichefu chefu embu nipe njia niingie mwenyewe nimtafute mwanangu

Jeremy: kuwa huru baba (anamuachia njia)

Ken:(anaingia ndani)

Keddy:(kwa Jeremy) mwanangu...

Jeremy: naam mama

Keddy: mmefanya vibaya sana mnajua

Jeremy: tunaomba msamaha mama...ila kweli kabisa mimi sijui Miriam alipo yaani tangu mchana namtafuta simpati

Keddy:(anasikitika) sijui atakuwa wapi

Ken:(anapayuka) Miriam...wewe Miriam toka kama umejificha wala sitakufanya chochote mwanangu twende nyumbani

Jeremy:(anaingia alipo Ken) dad...Miriam hayupo hata upayuke vipi hayupo

Ken:(anamnyooshea kidole) wewe mtoto najua mwanangu yupo hapa na chochote kitakachotokea kwa mwanangu wewe ndo utawajibika, naomba kesho nimuone mwanangu...

Jeremy: baba mimi sijui Miriam alipo

Ken: nimeshasema (kwa mkewe) twende mke wangu

(Wanaondoka)

Jeremy:(anabaki ameduwaa)!!!!makubwa haya sasa Miriam kaenda wapi au ndo yupo kwa bwana wake? ila hamna Miriam hayupo hivyo…kuna namna…au kuna kitu kimejificha hapo sikielewi vizuri (anaingia chumbani na kuchukua simu yake) embu ngoja nimpigie simu (anapiga simu)

(Simu haipatikani)

Jeremy: yuko wapi huyu mtoto... (anaonekana kuchanganyikiwa) hana tabia za disco kama dada yake, hanywi pombe, hata kama ndo kaenda kwa bwana ndo alale huko? (anaangalia simu yake) sasa ni saa sita na dakika ishirini na nane...hajarudi nyumbani na wala haijulikani yuko wapi…(anaguna)sijui nimpigie Vanessa au Naila au Ariana? ngoja niwapigie kila mmoja wao kwa wakati wake (anaanza na Vanessa)

(Simu inaita)

Vanessa:(anapokea) hello shem

Jeremy: shem...samahani nimekusumbua

Vanessa:(sauti ya usingizi) usijali…nambie

Jeremy: eti Miriam yuko wapi?

Vanessa:(anaguna) mi mara ya mwisho naongea nae ilikuwa saa 12 aliniambia anaenda kuonana na Ariana...ila baada ya hapo simu yake ikawa inapokelewa na mwanaume

Jeremy:(anashangaa) kumbe alienda kuonana na dada yake? wapi?

Vanessa: mimi aliniambia kwenye sight yao na nyumba yao mpya

Jeremy: nielekeze maana mwenzio nina msala imejulikana kuwa nina mahusiano nae na wazazi wake wamekuja hapa…yaani

Vanessa: muulize Ariana…ndo atakuwa anajua

Jeremy: nielekeze tu hilo jumba lilipo…yaani nitaenda usiku huu huu bila kupoteza muda…halafu baada ya hapo Ariana anatakiwa anijibu maswali yangu bila kukosa

Vanessa:  anyways ngoja nikuelekeze(anamuelekeza)

Jeremy: asante shemeji nimepaelewa

Vanesa: Miriam aliniambia wanatoka mtoko na dada yake na mimi nikajua wamerudi ila nikashangaa tu baada ya hapo simu yake ikawa inapokelewa na mwanaume amelewa na sijui alikuwa disco hata sielewi

Jeremy:(anashusha pumzi) asante sana umeupooza moyo wangu yaani ulikuwa unawaka moto kwa wivu nilijua mpenzi wangu kanisaliti na mwanaume mwingine

Vanessa: kuwa na Amani shemeji Miriam anakupenda wewe peke yake...yaani wewe nay eye ni kitu kimoja usijali mimi naona tu hapo kuna namna maana na dada yake nae ni mtata

Jeremy: wewe unahisi atakuwa amemfanya nini?

Vanessa:(anaguna) yaani siwezi kusema sana ila dada yake ni mtata yule yaani huwa hampendi Miriam

Jeremy: usiniambie

Vanessa: ndo nakwambia sasa shemeji tena nina uhakika hata hajafurahia huo uhusiano wenu

Jeremy:(anaguna) mbona kama alichukulia poa?

Vanessa: moyoni kwa mtu mbali shemeji na moyo wa mtu kichaka

Jeremy:ni kweli kabisa… (anashusha pumzi) asante kwa taarifa ubarikiwe…naenda sasa hivi huko

Vanessa: unaenda peke yako?

Jeremy: naenda na mlinzi wangu

Vanessa:na nyumba unaicha peke yake

Jeremy: right now...usalama wa Miriam ni wa muhimu kuliko nyumba

Vanessa:ni kweli kabisa shemeji

Jeremy: ngoja nikamcheki...nikimpata poa nisipompata tutaanzia hapo...utanisaidia kumpata

Vanessa: usijali daima nipo na nyie

Jeremy: asante shem usiku mwema

Vanessa: usiache kuniambia yaliyojiri

Jeremy: usijali

(Wanakata simu)

Vanessa:(anaendelea kulala)

Jeremy:(anavaa nguo maana alikuwa amevaa nguo za kulalia) ni lazima nimtafute mpenzi wangu sasa hivi...haijalishi nini (anatoka nje akiwa ameshikilia ufunguo wa gari) iam coming my love (anamuita mlinzi) rafiki…

Mlinzi :( anatoka mbio)

Jeremy: naomba unisindikize

Mlinzi: nyumba tunaichaje (anapanda kwenye gari)

Jeremy :( anapanda kwenye gari) wewe twende tu usalama wa malkia wangu ni muhimu kuliko hii nyumba (anawasha gari na kuliondoa)

Post a Comment

0 Comments