MUNGU MKUU 30


 

SCENE 30: -

USIKU HUO HUO (SAA SABA NA ROBO)

JUMBA BOVU: -

(Jeremy na mlinzi wake wanafika katika jumba hilo bovu, wanaangaza kwa kumulika na tochi kila sehemu)

Mlinzi: kuna gizi kweli hapa

Jeremy: hatutaondoka mpaka tumpate Miriam (anatembea tembea na ghafla anakanyaga kitu anamulika na Tochi) Oh My God…Miriam...

Miriam :( anahemea kwa mbali)

Jeremy: baby…wamekufanyaje? Oh My God Asante Sana…Asante sana Vanessa…Miriam… (Anamkumbatia)

Mlinzi :( anamuangalia) anaonekana ana hali mbaya kweli unaonaje tumpeleke hospitali?

Jeremy: yes…tumpeleke

Miriam :( haongei na wala hajitambui)

Mlinzi: wamemuumiza kweli mmh sijui nani kafanya huu unyama

Jeremy :( anaonyesha uoga) naomba uache kusema hivyo rafiki yangu nisaidie…

(Wanasaidiana kumbeba Miriam aliyelala na wala hajitambui)

Mlinzi :( anampima mapigo ya moyo) mbona hana mapigo ya moyo

Jeremy :( anajikuta anachanganyikiwa) Mungu wangu (anapata nguvu ghafla za kumbeba kipenzi chake)

Mlinzi: sasa hapa hospitali gani boss

Jeremy: tutajua mbele ya safari huko… (Anamuweka Miriam kwenye gari kisha anafunga mlango) kaa twende hatuna muda

(Wanapanda gari haraka Jeremy analiondoa gari Hilo, wakiwa ndani ya gari kila mmoja wao anaonekana kuwa na mawazo sana jinsi ya hali ya Miriam ilivyo mbaya)

Mlinzi :( anajisemea moyoni) hali ya shemeji mbaya kweli tunafika nae hospitali kweli?

Jeremy :( anajisemea moyoni) hali ya mpenzi wangu ni mbaya sana eeh Mungu naomba usimchukue bado namtaka ndo kwanza hata ndoa hatujafunga…naomba Mungu wangu unisaidie usimchukue kipenzi changu

(Miriam bado amelala)

Jeremy :( amechanganyikiwa Sana)

Mlinzi: taratibu boss…

(Gari linaenda kasi Sana na baada ya kutembea kwa muda hatimaye wanafika hospitali)

Jeremy :( anashuka kwenye gari anambeba miriam anaingia nae ndani ya hospitali)

(Manesi wamepitiwa na usingizi)

Jeremy :( anapayauka) jamani naomba mnisaidie Nina dharula jamani nisaidieni

Mlinzi :( Kwa manesi) nyie…

(Manesi wanashtuka)

Mlinzi: tuna mgonjwa hapa Ana hali mbaya sana tunaomba msaada wenu

Manesi :( wanaamka kwa kujivuta)

Jeremy: (anashikwa na hasira) inamaana hamuoni nawaita kuwa mpenzi wangu anaumwa sana? mbona mnajivuta kazi yenu ni nini? nitairipoti hii kwa mabosi wenu

Mia:(mmoja wa manesi) tusamehee kaka...ngoja niandae chumba naomba unifuate…

Jeremy:(akiwa bado kambeba Miriam anamfuata Mia kwenye chumba cha wagonjwa mahututi)

Mia: muweke hapa kaka ngoja nikawaite madaktari…

Jeremy:(anamlaza Miriam kitandani)

Mia: tusamehe kaka(anaondoka)

Jeremy:(anamshika Miriam) usijali mpenzi utapona mama usikate tamaa kila kitu kitakuwa sawa mama…naomba tu usikate tamaa nifikirie mimi na maisha ambayo tumepanga pamoja baby naomba usikate tamaa Miriam

Miriam :( bado hatikisiki wala kuongea wala kufumbua macho hali yake bado ni mbaya sana)

Jeremy :( anashikwa na hasira sana) hawa madaktari wako wapi utasema tumekuja kuomba msaada…

(Madaktari na manesi wanaingia)

Jacob:(daktari mkuu) ngoja nimuone mgonjwa (anamuangalia Miriam) oh mgonjwa hali yake sio nzuri… (kwa manesi na madaktari) naomba tumhamishe haraka sana (kwa Jeremy) kijana naomba utoke tufanye kazi yetu

Jeremy :( anamuangalia Miriam) sawa dokta naomba mmuokoe mpenzi wangu akipatwa chochote sitaweza kuishi

Jacob: usijali tutajitahidi kufanya kazi yetu…na Mungu atusaidie

Jeremy: najua Mungu ni mkuu atatenda miujiza yake… (Anatoka nje na kuwaacha madaktari na manesi wafanye kazi yao)

Mlinzi :( anamjia) boss vipi?

Jeremy :( anatikisa kichwa) sijui tu…ngoja nimpigie mama na baba yangu simu sina mtu yeyote wa kumwambia shida yangu hii… (Anachukua simu anabonyeza namba ya baba yake)

(Simu inaita)

Baba :( anashtuka kutoka usingizini) nani tena usiku wa manane?

Mama :( anashtuka anakaa maana alikuwa amelala) labda Jeremy…embu pokea...

Baba :( anaangalia kwenya kioo cha simu) hata hivyo ni yeye (anapokea) baba yangu nini usiku baba

Jeremy :( Analia) baba

Baba :( anapatwa na wasiwasi) nini wewe?

Jeremy: nipo hospitali...

Baba: kwanini? Una shida gani?

Jeremy: Miriam amepigwa sana ameumia sana hafungui macho haongei wala nini...Yaani hali yake ni mbaya sana baba

Baba: Mimi na mama yako tunakuja tuambie ni hospitali gani mwanangu halafu wapigie wazazi wa Miriam

Jeremy :( anawaelekeza)

Baba: nimepaelewa…tunakuja baba usijali tupo pamoja mwanangu

(Wanakata simu)

Jeremy :( anabonyeza namba za Mary)

(Simu inaita)

Mary :( anashtuka) nani tena? (Anaangalia kioo cha simu yake) Jeremy ananipigia usiku huu kuna nini? (Anapokea) baba?

Jeremy: ma mdogo…Miriam

Mary :( anashtuka) mwanangu amefanya nini mbona unalia

Jeremy: ana hali mbaya Sana yupo hospitali

Mary: amefanyaje embu ngoja nakuja nielekeze nakuja sasa hivi

Jeremy :( anamuelekeza)

Mary: nakuja ngoja niwaamshe tunakuja usijali baba subiri hapohapo tunakuja… (Anakata simu, anavaa nguo kisha anatoka anaelekea sebuleni) inabidi niwaamshe najua muda umeenda Sana ila sina budi (anaangalia saa ukutani) karibia saa kumi alfajiri (anaenda kugonga mlango wa Ariana)

Ariana :( anaamka) ah nani ananisumbua (Anafyonza)

Mary :( anagonga mlango wa Ken na mkewe)

Keddy :( anatoka) nini shida?

Mary: Miriam amepatikana

Ken :( anasikia anakuja haraka) yuko wapi?

Mary: hospitali

Ken: twendeni si mnapajua?

Ariana :( anatoka) kuna nini?

Ken: twendeni hospitali

(Wanaondoka)

Post a Comment

0 Comments