SCENE
31: -
(Ken, keddy, ariana na Mary wanafika
hospitalini wanamkuta Jeremy amejiinamia huku anaonekana kuwa na mawazo mengi
sana macho yake yamevimba sana kwasababu ya usingizi na kulia)
Mary:
Jeremy
Jeremy :(
anamkumbatia) ma mdogo (analia)
Mary:
basi usilie tena, umeshalia Sana
Ariana: (anachukia
kuona Jeremy Analia)
Ken:(anamkumbatia
Jeremy) nisamehe mwanangu…nilichukia sana ingawa bado tunatakiwa kuwa na
mazungumzo
Keddy:
baba Ariana haya sio ya kuongea sasa hivi
Ken:
najua
Mary:
ilikuwaje umemkuta wapi?
Jeremy:
kwenye jumba Fulani (anamuangalia Ariana) bovu…
Keddy:
Mungu wangu natumaini hawajamfanya vitu vya ajabu mwanangu
Ariana :(
anachukia Sana huku anajisemea moyoni) eti mwanangu (anafyonza)
ovyooo (anaendelea kujisemea moyoni) sijui amepataje bahati ya kupona si
angekufa tu mshenzi huyu yaani namchukia kuliko hata dunia inavyojua
Jeremy
:( Kwa Keddy) uzuri amepigwa Tu... Ameumia tumboni na amepata majereha
mengi sana kichwani
Mary :(
Analia)
Ken :( Kwa
Mary) usilie Mungu ni mkuu ameumia kidogo tu
Keddy:
kwani madaktari wanasemaje?
Jeremy:
hawajatoka
Ariana:
pole unaonekana umeumia Sana
Jeremy:
wewe hujaumia?
Ariana
:( anajichekesha) unaonekana umeumia kuliko sisi ndugu zake
Keddy:
huu sio wakati wa kutupiana vijembe
Ariana:
simtupii mtu yeyote kijembe
Ken:
acheni bwana sipendi kelele
Mary :( Kwa
Jeremy) upo peke yako?
Jeremy:
nilikuwa na mlinzi wangu akaondoka sasa nipo na wazazi wangu
Ken:
wako wapi?
Jeremy:
wapo nje...
Ken: oh,
jamani wana moyo mzuri Sana…
Keddy:
nataka kujua Miriam anaendeleaje
Jeremy:
haturuhusiwi kwenda…nimeomba mara nyingi Sana ila wanasema nitulie tu
Ken: oh
(Wanakaa)
Ariana
:( anamuangalia Jeremy Kwa hasira)
Mary:
umesema ulimpataje?
Jeremy
:( anajisemea moyoni) nikisema walienda kuonana na Ariana itakuwa msala kwa Ariana
sasa nisemeje?
Keddy:
baba, Mary anakuuliza kitu
Jeremy:
(anashikwa na kigugumizi)
Keddy:
vipi?
Jeremy:
baba alipokuja Jana usiku akaniambia kuwa Miriam haonekani…kama ilivyojulikana
mimi na Miriam tuna…
Ken:
tunaelewa...Acha stori nyingi endelea kusema ulimpata wapi?
Ariana
:( anajisemea moyoni) eti tunaelewa...Yaani hapa Mimi hawanifikirii
kabisa Jeremy alikuwa mchumba wangu amechukuliwa na Miriam kila mtu anaelewa? (Anasikitika)
huu ni ujinga hawa watu wananizingua tu nitaondoka muda sio mrefu
Mary:
wewe Jeremy…endelea
Jeremy:
nikampigia Vanessa akasema kuwa walienda kuangalia kazi Fulani naona huko ndo
yakampata hayo makubwa
Keddy:
dah…maana Jana akili ilikuwa haitulii kabisa…namfahamu sana mwanangu hana tabia
za ajabu za kunitia aibu
Jeremy:
namjua pia
Ariana
:( anajisemea moyoni) huu ni upuuzi kila mtu anamsifu Miriam utasema ni
malaika
(Wazazi
wa Jeremy wanakuja walipo)
Ken :( Kwa
baba Jeremy) oh David
David: Kennedy
(Wanakumbatiana)
Ken:
pole bwana
David:
pole pia
Ken: ila
Mungu amedhihirisha ukuu wake naona mambo sio mabaya sana
David:ni
kweli…daktari amesema kuwa hali aliyonayo sasa hivi sio hali aliyokuja nayo
Mary :( ananyanyua
mikono juu) Asante Jehovah
Mama
Jeremy :( kwa Keddy) mama Ariana
Keddy:
Mama Jeremy…za siku nyingi?
Mama
Jeremy: nzuri
(Wanakumbatiana)
Mama
Jeremy :( anamuangalia Ariana)
Ariana: shikamoo
mama, (Kwa baba Jeremy) shikamoo baba
(Wanaitikia)
Ken:
tuna mazungumzo ngoja hili lipite
David: Ken
nini tena?
Ken:
tutaongea
Jeremy
:( anamuangalia baba yake chinichini)
David :(
anajisemea moyoni) nimeshajua…tatizo nini
Ken: Kwa
sasa tujikite kujua hali ya Miriam
David:
kabisa
Ken: ILA
tusisahau kuwa tutakuwa na kikao cha dharula baada ya hili
David:
haina shida ndugu yangu
Jacob :(
anatoka chumba alichokuwepo Miriam)
Jeremy:
dokta…
Jacob :(
anamshika Jeremy bega) relax my friend...Mgonjwa amefumbua macho Kwa
mara ya kwanza tangu amefikishwa mahali hapa (anatulia kidogo) naweza kusema
huyu binti ana Mungu wake pamoja na kunyongwa sana…ameweza kuwa sawa
Ariana
:( anachukia Sana)
Mary:
Mungu ni mkuu jamani
(Wazee
waliopo hapo wanakumbatiana kwa furaha)
Ariana
:( anaonekana kukasirishwa na yote haya)
Jeremy :(
anafurahi Sana) tunaomba tumuone
Daktari:
anahitaji kulala maana pamoja ana kwamba alikuwa amefumba macho alikuwa
hajalala amechoka, mtamuona kesho asubuhi (anatabasamu kisha anaondoka)
(Wanabaki wanamshukuru Mungu kwa muujiza huo)
Ariana:(anakasirishwa
na ujumbe ule)
0 Comments