SCENE
32: -
KESHO
YAKE ASUBUHI: -
(Ariana anaingia chumba alichopo Miriam,
anamkuta bado kalala)
Ariana:
lione…limelala kwa amani wakati mimi sina hata raha sina hata hamu ya kula
Miriam :(
anaamka)
Ariana:
sijui huwa unampa nini Mungu maana hii ni mara ya tatu unanusurika…
Miriam
:( kimya maana hana uwezo wa kuongea kwasababu ya maumivu ya koo)
Ariana:
unanitolea macho...ndio mara tatu mara ya kwanza nilikutupa wakati upo mdogo
wakakutafuta ukapatikana, mara ya pili ajali iliyoua wanafunzi wengi
ukanusurika ukawa haupo na mara ya tatu ni hii...Mara zote nimefanya mimi
kasoro hiyo ya gari ila niliiombea
Miriam
:( anamuangalia akiwa bado kimya)
Ariana:
I hate you so much wewe Ni sababu ya huzuni yangu…nakuchukia Miriam nakuchukia
Sana wewe na mama yako nawachukia wote
Miriam
:( anamuangalia kimya)
Ariana: anyways,
usifurahi kuwa sasa limepita Hilo…bado ndo kwanza mwanzo huu…welcome to hell my
stupid sister (anacheka Kwa kejeli)
Jeremy
:( anakuja ghafla)
Ariana
:( anajifanya kumuweka vizuri Miriam) Shem
Jeremy:
nilikuwa nakutafuta
Ariana:
Mimi?
Jeremy:
ndio…wewe Shem
Ariana:
Mimi hapa sasa umenikuta
Jeremy:
najua kuwa wewe ndo ulikuwa na Miriam mara ya mwisho
Ariana
:( anashangaa Kwa kutoa macho mithili ya mjusi amebanwa na mlango)
Jeremy:
unashangaa? Kumbe wewe ni mnafki ee unajifanya unampenda Miriam kumbe ndo adui
yake mkubwa…kweli kikulacho ki nguoni mwako…sikutegemea
Ariana:
nani amekuambia?
Jeremy:
unataka kubisha?
Ariana:
naweza kuwa ni wa mwisho kuonana nae ila nisiwe ndo niliyemdhuru
Jeremy: oh,
comeon Ariana…mara ya kwanza nilikuwa nahisi naona vibaya maana sio kwa
kumuangalia vibaya vile mdogo wako…nilihisi humpendi ila sasa nina uhakika kuwa
humpendi na utafanya kila uwezalo kumdhuru
Ariana:
sisi ni watoto tunaofatana ni kawaida kukasirikiana kila mara
Jeremy:
najua ukweli juu ya familia yako nimewasikia wazazi wako wanaongelea…Miriam ni
mtoto wa ma mdogo
Mary
Ariana:
kweli? Hata sikujua
Jeremy:
ona unavyodanganya najua wewe ndo umewaambia maana nimewasikia wanamgombeza ma
mdogo kuwa kwanini hakuwaambia zamani mpaka wewe ukawaambia
Ariana: (anashusha
pumzi kisha anajichekesha) sawa nakubali yote nisamehe sasa
Jeremy:
ulichomfanyia Miriam sio kizuri hata kidogo natamani kukusamehe nashindwa
Ariana:
nisamehe na ninaomba usimuambie mtu yeyote kuwa mimi na Miriam tulikuwa pamoja
ule usiku
Jeremy:
nitakusamehe ila naomba uniambie kwa mdomo wako kuwa wewe ndo umesababisha haya
kwa mdogo wako
Ariana
:( anashusha pumzi) unanirekodi
Jeremy:
sina hiyo tabia na pia nakupa neno langu kuwa sitamwambia mtu chochote hii
itakuwa ni siri yetu sisi watatu
Ariana:
sikwambii kitu Jeremy
Jeremy:
hata usiniponiambia najua kuwa ilikuwa ni wewe ila sijui ni kwanini
Ariana
:( kimya)
(Ken
na polisi wanaingia)
Ken :( kwa
Miriam) mama unaendeleaje mwanangu?
Miriam :(
anatabasamu)
Mmoja wa
polisi: huyu yuko poa mpaka anatabasamu (anacheka)
(Wote
waliopo wanacheka kidogo)
Ken:
najua bado koo linauma nimekuja na karatasi utuambie watu waliokufanyia unyama
huo waandike kwenye karatasi
Ariana
:( anaanza kuogopa)
Jeremy
:( anamuangalia Ariana)
Polisi 2:
uliwaona waliokupiga?
Miriam
:( Kwa kuhangaika anaandika ndio)
Ken:
unawajua?
Miriam
:( anaandika hapana)
Polisi1
:( anashusha pumzi) duh kazi basi sawa wewe pumzika tutaendelea
kuwasiliana… (Kwa Ken) mzee acha sie twende tutakuja tena
Ken:
haya ngoja nikutoe…
(Wanatoka)
Jeremy :(
Kwa Ariana) mdogo wako ana kupenda Sana
Ariana
:( anafyonza moyoni)
Jeremy:
Ariana please acha hizo Kama ni umechukia kuhusu huu uhusiano tulikuuliza
mapema ukaonekana kuridhika sasa mbona inaonekana kuwa inakuumiza sana
Ariana:
nani amekuambia ni kwasababu ya wewe?
Jeremy
:( anamuangalia usoni bila kumwambia chochote)
Ariana:
who do you think you are?
Jeremy:
unapaniki
Ariana:
wewe ndo umeanza so chukua hiyo
Jeremy
:( anatikisa kichwa Kama kusikitika)
Ariana:
usijipandishe kijana
Jeremy:
sawa...Nadhani Kama ni hivyo sitasikia tena kuwa umemfanyia chochote mpenzi
wangu
Ariana:
mtajua wenyewe kwanza mnaendana wote hamna akili
Jeremy:
sawa…nafurahi kuona na kusikia kuwa umetutema sasa tutakuwa vizuri hakuna
shida…naombea tu hicho kikao cha dharula kitatupa ruhusa ya kupendana kwa amani
bila kujificha
Ariana:
mtajua wenyewe
Jeremy:
unajifanya una majibu…huku una msala
Ariana:
unataka nikutetemekee?
Jeremy:
nitawaambia kila kitu
Ariana:
nenda kawaambie wote wapo pale
Jeremy:
Do not be stupid Ariana
Ariana:
wewe ndo usiwe mjinga
Jeremy:
una maana gani? Je natakiwa kuwa makini kwamba unaweza kumuua mpenzi wangu
wakati wowote?
Ariana:
nimuue wa nini na nani amekuambia kuwa nilimpiga mimi usichukulie kunyamaza
kwangu ndo nimekubali?
Jeremy:
iam watching you Ariana
Ariana
:( anaondoka Kwa hasira) nimefanya nini kwanini nimegombana na Jeremy
huku natakiwa kupatana nae ili siku wakiachana na huyu Malaya nitapata nafasi
nzuri ya kuwa nae…nitamuomba msamaha
Jeremy
:( Kwa Miriam) dada yako ni mtu hatari sana…tuwe makini sana
Miriam
:( hajibu kitu)
0 Comments