SCENE
33: -
BAADA
YA SIKU TATU
NYUMBANI
KWA KINA MIRIAM
(SIKU
YA KIKAO CHA DHARULA)
(Miriam yupo nyumbani na hali yake inaonekana
kuwa nzuri na afya yake inaendelea kuimarika, amezungukwa na wazazi wa pande
zote mbili yaani upande wake na upande wa Jeremy, Jeremy na Vanessa wapo pia)
David:
unaendeleaje mama
Miriam :(
bado anahangaika kuongea) naendelea—vizuri kiasi baba
Mama
Jeremy: vizuri mama…
Miriam
:( anatabasamu)
Ken: nadhani Leo itakuwa siku nzuri ya sisi
kuzungumza mambo mawili ambayo yalikuwa siri ila sasa yanajulikana moja ni
kuhusu…ingawa natamani sana nisizungumzie ila nimeona nizungumze ili watu
wasibaki gizani (anatulia kidogo) jambo la kwanza ni kuhusu ukweli
kuhusu kuzaliwa kwa Miriam…
(Watu
wanasikiliza Kwa makini sana)
Ken:
Miriam ni mwanangu pamoja na yote…
Keddy :(
anainamisha kichwa)
Ken: (anamuangalia
Miriam) Miriam mwanangu, Kwa moyo mzito Leo naomba nikuambie ukweli wa
jinsi ulivyozaliwa
Miriam :(
anamsikiliza Kwa makini)
Ken :( anashusha
pumzi halafu kwa sauti ya chini anasema ukweli) Miriam sio mtoto wetu wa
kuzaa…tulimpata kwa njia ya ajabu
(David
na mkewe wanashangaa sana)
Ariana
:( anacheka chinichini baada ya kuona wazazi wa Jeremy wameshtuka)
Miriam Jeremy kwaheri kwenye uhusiano (anacheka chinichini)
David:
aisee yaani hatukujua na wala msingetuambia wala tusingehisi...Kabisa hongereni
mmejua kukaa na kitu na kukichukulia vizuri
Mama:
nyinyi ni wazazi wazuri sana…hongereni sana
Mary :( anafurahi)
Ken:
mama mzazi wa Miriam ni Mary…
David:
what? Na mlikuwa mnajua?
Ken:
hapana ndo tumejua siku ile Miriam amepotea
Mama
Jeremy: oh, Mary hongera kwa kuzaa mtoto mzuri kama Miriam
Ariana:(anachukia
sana huku anajisemea moyoni) sasa inakuja ile pointi muhimu ya Jeremy na
Miriam tuone kama watakubali(anaguna)pole sana Jeremy na Miriam mmejiona
wajanja tuone kama penzi lenu litakubaliwa
Ken:
Miriam mbona hujashangaa…? Ulikuwa unajua kuwa Mary ni mama yako? Yaani umepoa
hushangai hufanyi chochote vipi mama?
Miriam
:( anaongea kwa shida) hamna baba nilikuwa najiuliza kwanini mimi na ma
mdogo tunafanana
Keddy:
kwahiyo ukahisi kuwa anaweza kuwa mama yako?
Miriam:
ndio
Jeremy
:( anajisemea moyoni) najua unamzibia Ariana, najua uliambiwa na Ariana
Miriam
:( anatabasamu)
Ken:
pamoja na hayo ulitakiwa uonyeshe hata kushtuka lakini pia anyways tuachane na
hayo baada ya kujua Mary ni mama yako unajisikiaje? Samahani kukuambia hivi
wakati huu lakini Miriam sitaki kuendelea kukuficha umeshakuwa mkubwa
Miriam:
usijali baba…nakuelewa na kuhusu kujua Mary ni mama yangu sijui cha
kufikiria…nikitulia nitakuja na jibu
Mary :( anamshika
Miriam kwa upendo)
Jeremy :(
amesimama nyuma ya Miriam)
Ken:
sawa ingawa nimebaki na maswali naamini hilo tumemaliza la pili…ni kuna kitu
hapa sikielewi na wala sikipendi
David:
kitu gani?
Ken :( anavuta
pumzi) mzee mwenzangu
David:
naam…
Ken:
mlikuja na posa kumposa Ariana
Ariana
:( anajisemea moyoni) enhe…muulize huyu mzee anayejifanya mlokole tena
mzee wa kanisa
David:ni
kweli kabisa mzee mwenzangu
Ken:
sasa mbona leo hii nasikia Jeremy kamgeukia Miriam mnawachezea binti zangu?
Jeremy :(
anaingilia) hapana baba...Nampenda Sana Miriam
David:
Jeremy acha niongee (Kwa Ken) najua tulikuja na posa ya Ariana lakini
njiani mambo yalibadilika
Ken:
yalibadilika?
David:
ndio…hata sisi tulimwambia Jeremy kuwa hii sio vizuri (anatabasamu kidogo)
si unajua mambo ya moyo mzee mwenzangu tulitaka mpaka kumpoteza mtoto
wetu…wanapendana sana na kwa niaba ya familia yangu ninaomba msamaha mzee mwenzangu,
tusamehe sana
Ariana:(anajisemea
moyoni) are you kidding me? yaani ni kosa lakini linachukuliwa kawaida
Mama Jeremy:
tuwape nafasi watoto halafu isitoshe Ariana alikuwa sio kwamba kampenda mtoto
wetu kumbukeni tulikuwa tunawalazimisha watoto na Mungu ameona hilo ndo maana
hajaruhusu Jeremy na Ariana kuendelea
Ariana:(anajisemea
moyoni) duh...aisee siamini masikio yangu
David:
tuwaache wapendane
Ken:
vipi kuhusu mwanangu Ariana
David:
hakumpenda Jeremy sio jinsi Miriam anamvyompenda Jeremy
Ken :( Kwa
Ariana) eti Ariana unalichukuliaje?
Jeremy
:( anaingilia tena) alisema yupo sawa tu haina shida
Ken: eeh
kumbe alikuwa anajua
Jeremy:
ndio
Ken:
vipi kuhusu wewe Miriam Ni kweli unampenda Jeremy
Jeremy
:( anamshika mkono) usiogope huu sio wakati wa kuficha kitu mwambie
ukweli usiogope
Miriam:
ndio baba nampenda Jeremy
Ariana
:( anainamisha kichwa) aisee
Ken :(
kimya kidogo)
David :(
kimya huku anamuangalia Ken chinichini)
Ken:
kiukweli sijui nini cha kusema... (Kwa Ariana)
Ariana :(
amechukia Sana lakini anapoangaliwa na baba yake anajichekesha)
Ken :( anatabasamu)
unasemaje mwanangu
Ariana:
Mimi sina shida baba wamependana haw ana kama wanapendana basi hatuna budi
kukubaliana na haya yote
Keddy:
are you all right Ariana?
Ariana:
yeah
(Miriam
na Jeremy wanashangaa)
Ariana
:( anacheka) jamani mbona mnanishangaa kwani hamjui hata Mimi Nina moyo
mzuri?
Mary:
hakuna aliyekuhukumu Ariana
Ariana:
ila nini? (anacheka kidogo) mbona watu wote wananishangaa
Keddy:
tusamehe ila tunafurahi kama umekuwa mtu mzima kukubaliana na hili...
Ariana:
sawa mama
Ken:
basi sawa kikao chetu kimeisha kwa Amani
(Watu
wanashikana mikono kuonyesha Amani na upendo kati ya familia zote mbili. Miriam
na Jeremy upande mwingine wanaonekana hawana raha na wanamshangaa Ariana, Ariana
anaonyesha furaha na wala chuki)
Miriam
:( anajisemea moyoni) nina wasiwasi na dada
0 Comments