SCENE 34: -
(Kesho
yake asubuhi Ariana amekaa sebuleni anapata kifungua kinywa huku anatazama
runinga)
Miriam :(
anatokea chumbani anaelekea nje)
Ariana :(
anamuita) Miriam?
Miriam :(
anarudi) abee dada
Ariana:
umenipita bila kunisalimia shida nini?
Miriam:
samahani dada
Ariana:
usijali (anasimama na kumfuata aliposimama) Miriam bado umechukia
niichokufanyia siku ile
Miriam:
usijai dada nimeshasahau...Tugange yajayo
Ariana:
vizuri mdogo wangu…nisamehe tu dada yako nilifanya bila kufikiria…ila kikubwa
naomba usimwambia mama baba wala mama yako...
Miriam:
hata usijali hata Jeremy sijamwambia
Ariana:
Asante Sana mdogo wangu yaani unanipenda mpaka nafurahi (anatabasamu)
Miriam
:( anacheka)
Ariana
:( anakaa) njoo ukae na mimi…
Miriam
:( anakaa pembeni ya Ariana)
Ariana: Mary
ni mama yako
Miriam
:( anakaa kimya)
Ariana:
umelichukuliaje?
Miriam:
sijakaa kuongea nae...
Ariana:
ongea nae usipende kukaa Na kinyongo maisha Ni mafupi Sana kaa na mama yako
huwezi jua unakufa lini? Au utapata tatizo gani? Lini na saa ngapi? Ongea na
mama yako myamalize
Miriam:
Ni kweli dada unachosema…nitaongea Na ma mdogo sorry MAMA
Mary :( anawasikia
anajikuta anatabasamu mara baada ya kusikia Miriam amemuita mama) mwanangu
(anatabasamu)
Miriam:
nikitoka chuoni Mimi na yeye tutaongea Na nitamuita mama Kwa mara ya kwanza
Mary :( akiwa
bado amesimama mbali nao) Asante mwanangu Kwa miaka mingi nimekuwa
nikitamani uniite mama na leo hii nimesikia kwa mara ya kwanza (anafurahi)
Miriam:
anyways…acha niende nitaongea Na mama baadae
Ariana:
haya bwana…msalimie Shem Jeremy
Miriam
:( anacheka) sitaonana nae Leo
Ariana:
kwanini?
Miriam:
ah nataka animisi (anacheka)
Ariana
:( anacheka) anakumisi kila siku na kila saa...Una bahati sana kupata
mwanaume anayekupenda kwa dhati hongera mwaya
Miriam:
ila najisikia vibaya Sana
Ariana:
kwanini?
Miriam:
Jeremy alikuona kwanza wewe
Ariana: oh,
comeon Jeremy hakuniona aliletwa tu...
Miriam:
oh (huku ananyanyuka) jamani acha niende…naenda Kwa Vanessa kwanza
ananisubiri kuna kazi ya chuo nataka tuimalize mapema
Ariana:
msalimie Vanessa
Miriam
:( huku anaondoka) sawa
Mary :( anakuja
alipokaa Ariana) Ariana
Ariana:
abee ma mdogo…
Mary :( anatabasamu)
mlikuwa mnaongea nini na Miriam samahani lakini maana kwa mbali nimesikia
maongezi yenu nikahisi labda naota ndo nikaona nikuulize kupata uhakika Zaidi
Ariana:
amesema ataongea na wewe na atakuita mama kwa mara ya kwanza
Mary :( anafurahi
Sana) kumbe nilisikia vizuri
Ariana:
kabisa
Mary:
nimefurahi Sana
Ariana:
hongera kwa furaha yako…
Mary :( anamuangalia
usoni) hata wewe una furaha?
Ariana:
ndio Nina furaha nimeona tu niendelee na maisha yangu Jeremy ameshapenda
pengine sina budi kukubali
Mary:
vizuri Sana mwanangu…huko ndo kukua sasa ukisikia kukua ndo huko
Ariana
:( anacheka) ma mdogo bwana
Mary:
waache tu wapendane asije kukuumiza zaidi na zaidi unajua Jeremy alikuja hapa
akiwa hana hisia na mtu alitaka tu mke huwezi jua labda ndoa yenu ingejaa
majanga kila kukicha Mungu hutuepusha na mambo mengi
Ariana:
uko sawa kabisa ma mdogo
Mary:
acha niende mwanangu…
Ariana:
haya mama acha mimi ninywe chai niende ofisini kwa baba
Mary:
haya mama (ananyanyuka na kwenda zake)
Ariana
:( anapohakikisha Mary ameondoka kabisa ananyanyuka Kwa hasira) watu
wote wanaona kuwa mimi na Jeremy tusiwe pamoja na mimi nimekubali ila
sijakubali kwa moyo wangu wote nimekubali nikiwa na mipango yangu… (Anacheka)
eti waache wapendane kwani Mimi sitakiwi kupendwa? (Anabonyeza namba za mtu
Fulani)
(Simu
inaita)
Mtu :( anapokea)
Ariana:
ule mpango wetu sasa ufanyie kazi hawa watu wananichezea acha niwafurahishe
Mtu :(
anacheka)
Ariana:
hii itakuwa ni kali ya mwaka
Mtu:
asikuambie mtu
Ariana :(
anacheka)
Mtu: Ni Bomu
la mwaka (anacheka sana)
Ariana:
muache Miriam afurahi nitampa mwezi mmoja wa kufurahi baada ya hapo
kilio…hawezi kunichukulia mpenzi wangu kizembe halafu nikae kizembe mie
Mtu:
nipo tayari kukutumikia Ariana
Ariana: vizuri
sana na Asante…sana
(Wanakata
simu)
Ariana:
Miriam unadhani hata nakupenda? Sikupendi…wazazi wangu wanakupenda wewe kuliko
wanavyonipenda Mimi…nimepata mwanaume wa kunituliza nae umemchukua halafu
unaamini kuwa nimekubali sijakubali Miriam…Your hell begins now Miriam (anacheka)
Mary :(
anakuja ghafla bila kutegemewa) Ariana ndo unachekaje hivyo?
Ariana
:( anashikwa na kigugumizi) ma---mdo---
Mary: ah
utakuwa umechekeshwa kwenye simu siku hizi kuna mambo mengi kwenye simu,
nimeelewa (anacheka)
Ariana
:( anashusha pumzi)
Mary:
naenda sokoni tutaonana baadae
Ariana:
hata Mimi naondoka
Mary:
sawa (anatoka)
Ariana:
yaani pona pona yangu ningekoma leo (anabeba mkoba wake) ngoja niondoke
kabla sijazua balaa…niondoke kabla hata siri yangu haijavumbuka (anaondoka)
(Anaacha
vyombo hapohapo)
Ariana:
atatoa dada wa kazi au Mary mama Miriam... (Anaondoka)
0 Comments