SCENE
35: -
(Jioni
nyingine iliyo tulivu mbele ya macho ya viumbe vyote vile vinavyoonekana na visivyoonekana,
Miriam na mpenzi wake (Jeremy) wamekaa sehemu tulivu wakijivinjari na kutuliza
akili zao)
Miriam:(anakunywa
kinywaji chake)
Jeremy:(anakunywa
juisi yake huku macho yake yakimuangalia mpenzi wake)
Miriam:(anaweka
glasi chini baada ya kunywa kinywaji chake)
Jeremy:(anaweka
glasi mezani pia) aah
Miriam:
nini tena?
Jeremy:
wala… (anaangaza macho yake katika eneo hilo zuri na la kuvutia)
napapenda hapa…ni pazuri na pia ni pazuri Zaidi ukiwepo hapa
Miriam:(anacheka
kidogo)
Jeremy:
asante Miriam kwa kuja maishani mwangu…
Miriam:
ilikuwa ni mtihani lakini nashukuru Mungu dada Ariana amekubaliana na sisi
Jeremy:
ila mimi nina mashaka nae
Miriam: oh,
comeon Jeremy…dada Ariana amekubali kuwa mimi na wewe tunapendana na hawezi
kubadilisha hilo...hata mimi nilikuwa na mashaka nae ila tumezungumza basi
nimeona kumbe hana shida dada wa watu
Jeremy:
sijui lakini ila Ariana sio mtu mzuri hata kidogo yuko tofauti na wewe unajua?
Miriam:
watu tunatofautiana lakini unajua?
Jeremy:
nyie mmetofautiana sana…
Miriam:
anyways, acha tuachane na hayo tuangalie mambo yetu
Jeremy:
sijui kwanini lakini nafsi yangu inaniambia ni lazima nikuonye uwe makini sana
na Ariana
Miriam:
dada yangu anaweza kuwa ni mtu mwenye hasira sana ila nakuhakikishia kuwa
hawezi kunifanyia mimi kitu kibaya
Jeremy:
usijifanye umesahau Miriam…Ariana alikuteka na kukutesa sana nimekukuta nusu
mfu nusu mzima
Miriam: (anakaa
kimya)
Jeremy:
usimuamini Ariana she is very evil
Miriam:
sawa nakubali kuwa aliniteka na kunitesa sana…ila ameshabadilika
sana…amebadilika na ametukubali pia
Jeremy:
sio kweli. can’t you see baby…anavyotuangalia kila mara akituona pamoja ni kama
kuna kitu anapanga na kibaya sana...
Miriam:
hapana Jeremy dada yangu sio mbaya hivyo bwana
Jeremy:(anamuangalia
usoni) nikuambieje ili uamini kuwa dada yako sio mtu mzuri na wala
hakupendi hata kidogo?
Miriam:
naomba nikuulize kitu Jeremy
Jeremy:
go ahead…
Miriam:
kwanini unamchukia sana dada Ariana?
Jeremy:
simchukii…ila simuamini…na sidhani kama hata wewe unatakiwa kumuamini…kwa macho
yangu mawili nilimuona anavunja kioo cha gari nililokununulia
Miriam:
Jeremy tutagombana naona sasa unataka kunigombanisha na Ariana…Ariana ni dada
yangu hata kama hatujazaliwa tumbo moja tumekuwa wote Jeremy…
Jeremy:(anatikisa
kichwa ishara ya kusikitika)
Miriam:
mimi na Ariana tumekuwa pamoja na baba huwa anatusisitiza kupendana
Jeremy:
wewe unampenda ila mwenzio hakupendi…
Miriam: (kwa
hasira) enough Jeremy...naona maongezi yetu yataishia kugombana…
Jeremy:
utakuwa umependa wewe…ila kwa upande wangu mimi sitaki na wala sitamani
kugombana na wewe
Miriam:
basi usimseme vibaya dada yangu
Jeremy:
Miriam
Miriam:
Jeremy please don’t … (anamuonyesha ishara ya kumkatiza) tumekuja
kuenjoi na sio kukerana
Jeremy:(ananyamaza
huku anamuangalia Miriam kwa huruma)
Miriam:(anabadilisha
mada) enhe nambie…tutaenda tulipopanga?
Jeremy:(anaitikia
kwa unyonge)
Miriam:
jamani ndo unaitika kama hutaki??
Jeremy:
hamna kawaida…tu nipo poa mbona?
Miriam:(anakunywa
kinywaji chake huku anamuangalia mpenzi wake)
Jeremy: anyways,
tutaenda tulipopanga…
Miriam:
cheka basi jamani
Jeremy:
sijisikii kucheka Miriam
Miriam:
kwasababu sijakusikiliza au?
Jeremy:
hapana…huo ni uamuzi wako na wala sitaruhusu hili litie doa penzi letu…kuwa na
Amani Miriam…ila nataka utambue kuwa sijui kwanini ila nahisi Ariana anapanga
jambo baya sana…
Miriam:(anakaa
kimya)
Jeremy:
my queen naomba unisikilize kesho nitakuhamisha hapo nyumbani uke mbali nae...na
pia akikuita sehemu usiende peke yako kama siku ile
Miriam:(anacheka
kidogo) Jeremy hivi unadhani kunitoa nyumbani ni jambo rahisi?
Jeremy:
najua sio jambo rahisi…okay nitakuoa…nitafunga ndoa na wewe Miriam…
Miriam:
Jeremy, mimi nasoma bado
Jeremy:
hiyo haina shida Miriam yaani haina shida utaona tu mimi nakuja kutoa mahari
siku sio nyingi mpenzi wangu na pia baada ya hapo, tutafunga ndoa haraka iwezekanavyo
ili utoke karibu na Ariana
Miriam:(anatikisa
kichwa) hata sijui cha kufanya Jeremy…sijui nikumbieje ili ujue kuwa mimi
na dada Ariana tumekuwa ni marafiki wakubwa sana...okay nimejaribu kukutoa
kimaongezi ila naona hata hubadiliki
Jeremy:
kwa vyovyote vile Ariana akikuita sehemu usiende hata kwa nini…nitamuomba
dereva wako pia asikupeleke sehemu ambayo Ariana yupo...
Miriam:
Jeremy…
Jeremy:
nimemaliza…na mama yako ma mdogo Mary nimeshamwambia pia
Miriam:
umemwambia wa nini?
Jeremy:
kwa ajili ya usalama tu na sio vinginevyo
Miriam:
yaani Jeremy…sijui Ariana alikufanya nini?
Jeremy:
kwanini?
Miriam:
humpendi na sidhani kama hata ana mawazo mabaya juu yangu ila tu kwasababu
humpendi ndo unaamua kusema hayo maneno jamani sio vizuri
Jeremy:one
day utaniambia kuwa Jeremy ulikuwa unaniambia ukweli
Miriam:(anatabasamu)
yaani unaongea uko serious utasema polisi jamani
Jeremy:
Miriam sikutanii niamini kuwa dada yako ndo adui wako wa kwanza Zaidi hapo
kwenu
Miriam:
okay sitaki kukuudhi hivyo nitafanya kama unavyotaka ili nisikuudhi
Jeremy:
asante mke wangu…nitamwambia baba na mama kuwa ninataka nikuoe…najua watakubali
maana hata wao wanakupenda sana (anacheka kidogo) jamani huwezi kuamini
walikuwa wananiambia bora ningekuchumbia wewe
Miriam:
waliponiona?
Jeremy:
ndio…
Miriam:(anacheka)
Jeremy:
unacheka nini?
Miriam:si
unanidanganya
(Wanacheka)
Jeremy:
nakwambia ukweli Miriam...nakupenda sana lakini wazazi wangu wanakupenda Zaidi
(Wanacheka
sana)
Jeremy:
kunywa juisi tuondoke bwana usije ukachelewa nyumbani bure
0 Comments