SCENE
36: -
BADA
YA SIKU TATU: -
NYUMBANI
KWA KINA MIRIAM: -
(Asubuhi
mpya na njema na ya kumpendeza Mungu na binadamu, jua linawaka kawaida na upepo
mzuri unavuma vizuri na kila mtu anaendelea na shughuli zake. Miriam nae ni
mmoja wa watu wanaoendelea na shughuli zao)
Mary:(anamuona
Miriam) mwanangu
Miriam:
mama…
Mary:
dereva wako yupo hapo nje…
Miriam:(anashangaa)
makubwa amekuja kufanya nini?
Mary:
anasema ametumwa…
Miriam:na
Jeremy?
Mary:
lazima iwe na yeye au kuna mwingine?
(Wanacheka)
Mary:
shoga yangu unapendwa mwayaaa
Ariana:(amesimama
pembeni)
Miriam:
karibia niwe mke wa mtu
Mary:
shoga yangu…niambie huo umbea
Ariana:(anafyonza)
pumbavu (anaondoka kwa hasira anachungulia dirishani anamuona dereva)
lione lile nalo …(anafyonza)
Miriam:(anapita
kuelekea nje)
Ariana:(anamuangalia
Miriam) embu lione yaani simpendi mimi huyu mtoto sijui tu…
Miriam:(anamuona
Ariana) dada Ariana
Ariana:(anajichekesha)
abeee...(anajichekesha)
Miriam:
natoka kidogo…shemeji yako kaniita
Ariana:(anajichekesha)
haina shida we nenda tu uzuri baba na mama wanajua wewe na Jeremy mnapendana...nenda
tu
Miriam:
asante sana dada…okay acha mie niende
Ariana:
msalimie
Miriam:
usijali…. (anamgeukia mama yake mzazi) naenda mama
Mary:
tutaonana mwanangu
Ariana:(anamuangalia
Miriam kwa chuki sana)
Miriam:(anaondoka
kuelekea lilipo gari lake)
Ariana:
hesabu siku zako Miriam mwisho wako umefika… (anacheka kwa kejeli)
Dereva:(anamuangalia
sana Ariana)
Miriam:(anafika
kwenye gari lake anafungua mlango wa gari na kuingia)
Dereva:
enhe mrembo embu niambie za kwako?
Miriam:
nzuri shoga
Dereva: Vanessa
yuko wapi?
Miriam:
yupo tu…
Dereva:
haonekani (anawasha gari) halafu mbona dada yako anakuangalia vibaya
sana?
Miriam:
umeongea sana na Jeremy eti eeh
Dereva:
hapana sijaongea nae kwanza huwa hatuongei
Miriam:
mna mawazo sawa yaani wote mnamuongea vibaya sana dada yangu mna shida gani?
Dereva:
sio kumuongea vibaya ni ukweli usiopingwa wifi yaani anakuangalia vibaya sana
mpaka inaogopesha
Miriam:
wasiwasi wenu tu wenzangu mbona mimi na yeye tunapendana mpaka basi?
Dereva:(anaguna)
labda ndo jinsi anavyoangalia…simjui vizuri mimi huwa namuona tu ila mara
nyingi nikimuona huwa anakuwa ni mtu wa kukasirika sana sijui huwa ana shida gani...?
Miriam:
mnamuwaza tu
Dereva:
labda... (anaendesha gari kuondoka mahali hapo)
Miriam:
tunaenda wapi?
Dereva:
surprise…kuwa mpole utapajua tu shoga re
(Wanacheka)
Miriam:
yaani Jeremy ameshakufundisha ujinga jamani…
Dereva:
usijali jamani sio kwa ubaya jamani
Miriam:
Jeremy yuko wapi?
Dereva:
tulia mwanamke…(anashangaa)mbona una haraka wewe?
Miriam:
jamani…nisije nikawa napelekwa
Dereva:
kwani unadhani naweza kukupeleka mateka…? Jeremy anaweza kunisaka hata mpaka
chini ya bahari…
(Wanacheka)
0 Comments