SCENE
37: -
BAADA
YA DAKIKA AROBAINI: -
KWENYE
NYUMBA MPYA: -
(Baada
ya dakika arobaini Miriam na dereva wanafika katika nyumba moja kubwa na mpya
na pia ni ya kifahari sana)
Miriam:(huku
anashuka kwenye gari) shoga yangu mbona nyumba inatamanisha hii ni ya nani?
(nafunga mlango wa gari)
Dereva:(anashuka
kwenye gari kisha anafunga mlango) ndo usubiri sasa shoga yangu
Miriam:
usiniambie hi indo surprise uliyokuwa unaniambia
Jeremy:(amesimama
nyuma yao) exactly my love
Miriam:(anashangaa
sana) how come? (kwa madeko kidogo) jamani Jeremy sio vizuri
Jeremy:(huku
anacheka) do you like it?
Miriam:
oh My God iam so happy so very happy… (anajikuta anamkumbatia kwa upendo na
furaha)
Jeremy:(anamkumbatia
pia) nafurahi kuwa umeifurahia nyumba hii.
Miriam:
baada ya harusi tutaishi hapa?
Jeremy:
ukiniruhusu sasa hapa mimi sitakuwa baba mwenye nyumba nitakuwa naishi
kwako…utaishi na mimi kwenye nyumba yangu ili niwe baba mwenye nyumba
(Wanacheka)
Dereva:
unaogopa kuwa chini ya mwanamke?
Jeremy:
vibaya sana
Dereva:(anabaki
anacheka)
Miriam:(bado
naishangaa nyumba ile ya kifahari) oh My God… (anacheka) this is crazy
wallahi
Jeremy:(kwa
Miriam) naona unashangaa sana unaonaje tukaingia ndani? tuione kwa karibu
Miriam:
hapo sasa ndo umenena baba
(Wanaingia
ndani)
Miriam:
oh my God …hii ni paradiso au?
Dereva:
una bahati shoga yangu ndo maana dada yako anakuchukia
Jeremy:
(anaguna)
Miriam:
jamani embu tusiongelee hayo maana sipendi kusikia dada yangu anasemwa vibaya
(Jeremy
na dereva wanaangaliana)
Miriam:(kwa
Jeremy) baby asante kwa zawadi hii...
Jeremy:(anakaa
kimya)
Miriam:(naendelea
kuangaza macho yake kwenye nyumba ile ya kifahari iliyojaa samani za thamani)
sasa hapa jikoni ni wapi (anageuka alipo Jeremy)
Jeremy:(amepiga
goti moja ameshika kiboksi Fulani mkononi)
Miriam:(anashangaa)
Jeremy…mbona umepiga goti? una shida gani?
Jeremy:
will you marry me?
Dereva:
wow…jamani finally…
Vanessa:(anatokea
nje)
Miriam:
(amesimama kama sanamu iliyogandishwa)
Vanessa:
wewe jibu sio umeganda kama sanamu
Miriam:(analengwa
na machozi) lakini …baby mimi sikujua kama utakuwa unamaanisha ulichokuwa unasema,
mi nilijua tu unajisemea
Jeremy:
ndo nakuomba
(Wazazi
wa pande mbili akiwemo Ariana na Mary wanafika mahali hapo)
Miriam:(anawaona
anajikuta Analia kwa furaha) jamani mbona mpo hapa? Mmefikaje hapa si
nimewaacha nyumbani?
Mary:
kuna njia fupi ndo tumetumia
David:
hukutaka au?
(Wanacheka)
Ken:
jibu basi mwenzio anaumia… (anamsogelea Jeremy)
Miriam:
yes…I will marry you my love
(Vigelegele
n vifijo vinaendelea mahali hapo)
Ken:(anamsaidia
Jeremy kunyanyuka) hongera sana umekuwa mume wa mtu mtarajiwa
Ariana:(anafura
na hasira ila anajichekesha akigundua kuwa kuna mtu anamuangalia)
Keddy:(kwa
Ariana) dada wa bibi harusi (anacheka)
(Wanacheka)
Ariana:(anamkumbatia Miriam) hongera
mdogo wangu nakuombea kwa Mungu awafikishe kwenye kusudi lako na mpenzi wako
Miriam:(anaangalia
pete yake ya thamani)
Ariana:(anaangalia
pete ile na roho inamuuma sana)
Miriam:
asante sana dada yangu kwa maombi yako
Ariana:
usijali mdogo wangu kwetu tupo wawili tu nitakusimamia mpaka siku ya harusi
yako
(Vanessa,
dereva pamoja na Jeremy wanaangaliana chinichini)
Ariana:
(kwa Jeremy) shemeji harusi lini?
Jeremy:
kesho…
Araina:(anashangaa)
what?
Jeremy:
what nini? Hutaki au?
Mma
Jeremy:(anacheka) anakutania…
Ariana:
nimejua tu kuwa ananitania haiwezi kuwa kesho
Jeremy:
kwanini?
Ariana:
hatujajiandaa
Jeremy:(anacheka
kwa kejeli)
Mary:(kwa
Miriam) hongera sana mwanangu umependeza na pete yako mwenyewe jamani Mungu
awasaidie mama
Jeremy:
amina mama na ninaombea Mungu awapige wale wote watakaokuwa kinyume na sisi na
mipango yetu (anamuangalia Ariana chinichini)
Miriam:
Jeremy kila mtu ni mwema kwetu hapa mipango yetu itaenda vizuri kwa jina la
Yesu…
David:
amina
Mama
Jeremy:(kwa Jeremy) tuonyesheni basi jikoni
(Wanacheka)
Miriam:
asanteni sana jamani nimefurahi sana utasema ni kumbukizi ya siku yangu ya
kuzaliwa
Keddy: you deserve the best my love
Ariana:
:(anakasirishwa sana na maneno ya mama yake)
Mary:(anamuangalia
Ariana)
Ken:
tangazo…jamani mwanagu mkubwa pia amepata mchumba bado hatujamuona ila
tunatarajia kumuona hivi karibuni...
(Watu
wanafurahia sana)
David:
habari njema sana naona tupange harusi siku moja itakuwa nzuri sana
Ken:
wazo zuri sana mzee mwenzangu jamani
(Familia
zote mbili zinabaki kuwa na Amani na furaha kwa habari ya uchumba wa binti wote
wawili)
0 Comments