SCENE
38: -
JUMAMOSI:
-
(Familia
zote mbili zimekusanyika katika jumba safi la mzee Ken kushuhudia utambulisho
wa mchumba wa Ariana, kila mtu anaonekana ana furaha na Amani)
Mary:(anaona
magari mawili ya kifahari) wanakuja jamani tujiandae
Keddy:
naomba kwa Mungu kila kitu kiende vizuri…Ariana yuko wapi?
Ariana:
nipo hapa baba
Jeremy:(amekaa
kimya ila ana wasiwasi wa jambo Fulani)
Miriam:(anamuona
mchumba wake) mume mbona hivyo?
Jeremy: kwani vipi mke?
Miriam:
una wasiwasi...sana shida nini?
Jeremy:
Mungu akulinde tu mke…
Miriam:
kwanini?
Jeremy:
basi tu
(Wageni
wanaingia)
Wenyeji:
jamani karibuni sana
Wageni:
asante sana
(Kuna
furaha na amani inaendelea mahali hapo, familia ya mchumba wa Ariana na familia
ya kina Ariana wanapokeana vizuri sana)
Miriam:(ananyanyuka
na kuelekea jikoni)
Jeremy:(anataka
kumfuata)
David:(anamuona)
baba embu saidia wenzio
Jeremy:
sawa baba
Miriam:(anaenda
jikoni)
(Vinywaji
vinaleta na mmoja wa watu wanaoleta vinywaji ni Ariana)
Ken: Ariana
mama... (anamuonyesha ishara ya kumuomba aondoke)
Mzee:
muache tu aisee anaonekana ana adabu sana…ni mke mzuri sana kijana wetu amejua
kuchagua
(Wanacheka)
Jeremy:(anamuangalia
sana Ariana)
Ken:(kwa
mchumba) kijana unaitwa nani baba?
Mchumba:
(kwa heshima) naitwa Colton
Ken:
jina zuri sana kijana…
Colton:
asante sana baba
Ariana:(anamwagia
kinywaji Colton kwa bahati mbaya)
Colton:
oh shit…
Ariana:(anamnong’oneza
Colton) kazi yetu inaanza sasa hivi…
Ken:
pole baba ni bahati mbaya pita nenda bafuni ukajisafishe… (kwa Jeremy)
kwanini usikimbie nyumbani ukamletee nguo mwenzio
Jeremy:(kwa
heshima) sawa baba… (ananyanyuka anapiga hatua kisha anajisemea moyoni)
nimemuona Ariana anamwagia kinywani Colton kwa makusudi kabisa (anaguna)je
kuna mpango wowote unaendelea? Colton anaenda bafuni na Miriam yupo jikoni… (anataka
kurudi)
David:
baba nenda ukamletee mwenzio nguo
Jeremy:
sawa baba(anaondoka)
Colton:(anaenda
jikoni badala ya bafuni)
Miriam:(anamuona
Colton) wewe ndo shemeji yangu?
Colton:
ndio (anamuangalia kwa matamanio sana) napenda matako yako (anamshika
matako)
Miriam:(anamsukuma
na kumpiga kibao) unikome…tena ukome uwe na adabu
Colton:
nimesikia kuwa una mtindo wa kuchukua shemeji zako…
Miriam:(kwa
hasira) nani amekuambia?
Colton:
kila mtu anasema
Miriam:
hapana mimi na Jeremy tumependana Sana na familia zetu zilikaa na kuongeaa
tukakubaliana na sasa mambo yapo sawa
Colton:(ghafla
anamkumbatia) mpenzi jamani umeniacha na kwenda kwa Jeremy kisa sina hela
kama yeye?
Miriam:(anahangaika
kumsukuma)
Colton:(anamg’ang’ania)
nakupenda Miriam mpenzi wangu
(Familia
zote mbili zimesimama zinashuhudia tukio hilo)
David:
nini hiki Miriam?
Ariana:(anacheka
chinichini)
Miriam:(anashangaa)
Colton:
naomba niongee jamani…mimi na Miriam ni wapenzi muda mrefu sana alinisaliti
nikaamua kumchumbia dada yake...
Ariana:(anajiliza)
nina nini mimi kwanini Miriam ananifanyia hivi…?
Miriam:
dada…
Ariana:(kwa
Colton) kwanini hukuniambia kuwa wewe na Miriam mna mahusiano? kwa mara
nyingine nimeumia…mara ya kwanza ilikuwa Jeremy na sasa ni Colton…kwanini
lakini?
Ken:
siwaelewi…kwamba nini?
Keddy:(amekaa
kimya)
Colton:(kwa
Ken) mimi na Miriam ni wapenzi…wa muda mrefu...amenisaliti na kuwa ana
Jeremy…kisa Jeremy ana pesa…nimeumia sana ndo maana nikaamua kuwa na dada yake
Ariana:(anajiliza)
Ken:
kijana…kwanini unasema uongo
Miriam:(Analia
sana)
Ken:
yaani eti kisa Miriam kakuacha ndo uje umchukue dada yake?
David:
inawezekana ndio… labda amefanya kwa hasira
Mama Jeremy:
baba Jeremy
David:
wewe binti ni mhuni kumbe ee
Ken:(kwa
David) mzee mwenzangu…embu ngoja… (kwa Colton) kwa heshima chukua
wazazi wako uondoke hapa…sitakuruhusu umuoe mwanangu mana huna msimamo na pia
ni muongo
Colton:(anaondoka
yeye pamoja na wazee wake)
David:
mwanangu hatoweza kumuoa mwanamke anayechanganya wanaume
Keddy:
nimemlea Miriam na ninamfahamu…hakuwa na mahusiano na mwanaume mwingine yaani
Jeremy ni mwanaume wake wa kwanza…
Ariana:(anakasirika
sana)
David:
kuna mambo mengine wazazi hatuyafahamu…kuhusu watoto wetu
Mary:
tunamjua Miriam sana na sana na hata siku moja hajawahi kufanya jambo la aibu
David:(amekaa
kimya)
Jeremy:(anarudi)
kuna nini…jamani?
David:
tumemkamata mchumba wako na mwanaume mwingine
Jeremy:
nilijua tu kuna kitu Ariana anapanga
Ariana:
mimi tena?
Jeremy:
usidhani mimi mjinga umepanga yule kaka sio mchumba wako umempika tu…
Araina:
kwa kuniona siwezi kupendwa au?
Jeremy:
muogope Mungu utakufa vibaya sana Ariana… (anamkumbatia mpenzi wake)
David:ni
muda wa kuondoka na hatutarudi tena hapa
Jeremy:
basi sahau kuwa mimi ni mwanao
Mama Jeremy:
jamani nyie
Miriam:(Analia
sana)
Ken:(anamkumbatia
Miriam) acha kulia tafadhali
Ariana:(anakasirika)
David:
mnamuamini sana Miriam ee
Keddy:
shemeji ni kwasababu tunamjua Miriam vizuri
David:(anakaa
kimya)
Ken:(kwa
David) tumshukuru Mungu kwamba kwa pamoja tumemjua na tumejua hila za huyu
kijana hakuwa na nia nzuri kwa familia yetu
Jeremy:
unadhani ni kwa ajili gani?
Ariana:(anajiliza)
Ken:
acha kulia Ariana na umshukuru Mungu kwa kukuepushia hili pia…
Jeremy:(bado
amemshika Miriam)
David:(anashusha
pumzi) sijui niamini nini…
Mama
Jeremy: baba Jeremy…wewe hujaona Miriam alivyokuwa najitahidi kumsukuma? na
pia, hata kama walikuwa wapenzi tayari wameachana na Miriam ameamua kumchagua
Jeremy…huyo kijan ameingia kuharibu maisha ya hii familia…ni hila za huyo
kijana na bahati nzuri tumemjua... (kwa Ariana) pole mwanangu kwa kuwa
mhanga wa huyo kijana usijali tumeshamjua…
David:
basi sawa tufanye ilikuwa hivyo
Jeremy:(anamuangalia
Ariana kwa jicho baya sana)
Ariana:(anajiliza)
David:
pole sana mwanangu Ariana na pia Miriam nisamehe mwanangu
Ariana:
usijali baba
David:
haya tuendelee na mambo mengine
Jeremy:(anamfuta
machozi Miriam) pole yameisha mpenzi
Miriam:(anashusha
pumzi) asante sana
Ken:
jamani nawashukuru sana tulisahau hili jamani
Keddy:
kabisa
(Wanarudi
sebuleni na kuendelea na shughuli zingine)

0 Comments