MUNGU MKUU 39

 

SCENE 39: -

JUMAMOSI USIKU: -

(Ariana amekaa chumbani huku nafsi yake inaonekana kuwa imechafuka sana kwa tukio lililotokea asubuhi yake)

Ariana:it is not over untili it is over…huyu Miriam asidhani ameshinda kwamba limeisha…halijaisha na sio kwamba Mungu wake atamsimamia milele kuna kipindi Mungu wake hatakuwepo

(Simu yake inaita)

Ariana:(anaipokea) Colton yaani wewe ni bonge la mshamba…nilikuaminia sana kumbe   wewe ni fala tu (anafyonza)

Colton: nipe nafasi nyingine Ariana nitakuonyesha naweza kufanyia yaliyo mazuri Zaidi ya haya uliyoyategemea

Ariana: sawa naomba unipe ahadi ya kitu Fulani…

Colton: nini tena?

Ariana: wewe ni muigizaji mzuri?

Colton: ndio…sana tu…

Ariana: kuna jambo la kutisha naenda kumfanyia Miriam hakuna atakaye msaidia hata Mungu mwenyewe

Mary:(yupo nyuma yake) unataka kumfayia nini mwanangu?

Ariana:(anashtuka haraka anakata simu)

Mary: unaongea na nani? (anachukua simu ya Ariana) Colton?

Ariana: ndio Colton

Mary: kwahiyo una mawasiliano na Colton? inamaana umekuwa karibu na Colton…labda kutakuwa na ukweli juu ya kile alichokuwa anaongea Jeremy…alituambia kua ni lazima utakuwa umempika Colton…kumbe unamchukia sana Miriam?

Ariana: sana namchukia tangu alivyokuwa mdogo alikuja kupokonya penzi la wazazi wangu, kuanzia hapo nikawa kama mtoto baki...nilivumilia ila sasa imekuwa ni too much nimechumbiwa (anaongea kwa hasira sana) akamchukua mchumba wangu

Mary: Jeremy alimpenda mwenyewe

Ariana: kwanini hakukukataa?

Mary: alijaribu

Ariana: haikutosha…alimtaka tu

Mary:(anakaa kimya)

Ariana: nitamuadhibu Miriam n ukimwambia mtu nitamuua Miriam pamoja na wewe…usinichezee

Mary: wewe sio muuaji

Ariana: wazungu wanasema try me

Mary: Ariana

Ariana:(anamuangalia) umeniletea maziwa?

Mary:(anampa)

Ariana:(hapokei) kampe mwanao maana anaweza kuyakosa haya…mpe anywe kwa wingi

Mary: utamfanyaje mwanangu

Ariana:(anamnong’oneza) siri…(anacheka)unaweza kuondoka nina usingizi sana nataka kulala

Mary: una roho ya nani we binti?

Ariana: embu niondokee hapa

Mary: dhambi ni mbaya sana na unajua hilo

Ariana: toka chumbani kwangu tafadhali

Mary:(anaondoka)

Ariana:(anamfuata) ole wako umwambie mtu…nitamuua mwanao na wewe kwa pamoja

Mary:(anamgeukia anamuanglia kwa unyonge)

Ariana:(anafyonza kisha anabamiza kwa hasira)

Mary:(anaenda chumbani kwa Miriam) hodi mwanangu

Miriam: karibu mama(anamfungulia)karibu mama…

Mary:(anaingia ndani) hujalala?

Miriam: naangaalia tamthilia

Mry:(anakaa pembeni yake) tamthilia gani?

Miriam: law of the heart inaonyeshwa hapa telemundo

Mary: inaonekana nzuri sana…

Miriam: sana

Mary: kama wewe

(Wanacheka)

Mary: nimepita kukuambia kuwa nakupenda sana mwanangu na nitafanya kila kitu kuhakikisha unabaki salama

Miriam: mama una maana gani?

Mary: sina maana yoyote…mwanangu (anacheka) kwani siruhusiwi kukuambia maneno hayo?

Miriam: jamani…nakupenda mama

(Wanakumbatiana)


Post a Comment

0 Comments