SCENE
40: -
BAADA
YA SIKU TATU: -
(Majira
ya saa kumi na mbili jioni, miriam anatoka chuoni baada ya kumaliza kipindi cha
mwisho cha siku hiyo, anaongea na simu)
Miriam:
leo nimechoka sana unajua…kwahiyo hatutaonana…
Jeremy:
poa nitamtuma dereva wako aje akuchukue au unaonaje?
Miriam:
afanye haraka…asiniweke
Jeremy:
dakika moja tu
Miriam:
okay namsubiri
Jeremy:
I love you so much my love
Miriam:
I love you too…baby
(Wanakata
simu)
Miriam:(anasimama
akiwa na lengo la kusubiri gari lake lije kumchukua na kumpeleka nyumbani)
(Simu
yae inaita)
Miriam:(anapokea)
dada Ariana vipi?
Ariana:
chukua boda mara moja uje hapa mara moja nina shida naomba msaada wako
Miriam:
wapi?
Ariana:(anamuelekeza)
Miriam:
haya dada nakuja…
Ariana:
fanya haraka mdogo wangu
Miriam:(anaita
pikipiki anamuelekeza na mara moja anaondoka mahali hapo)
(Baada
ya mwendo wa takribani dakika tatu, hatimaye anafika mahali ambapo ameelekezwa
na Ariana)
Miriam:(anashuka
kwenye pikipiki anamlipa kisha anamruhusu kuondoka)
Dereva
pikipiki:(anaondoka)
Miriam:
mbona simuoni tena… (anachukua simu yake kisha anampigia)
(Simu
inaita)
Ariana:(anapokea)
nakuona
Miriam:
njoo basi naona giza linaingia
Ariana:
una haraka sana?
Miriam:
wewe unanijua kuwa sipendi kukaa nje kwa muda mrefu
Ariana:
sasa hivi utapata nilichokuitia
Mtu:(anakuja
nyuma ya Miriam na kumziba pua na mdomo kwa dawa ya usingizi)
Miriam:(analegea
na kuanguka chini)
Mtu:(ni
Colton)
Ariana:(anatokea
kutoka kwenye maficho) leo ndo mwisho wako Miriam nitakachokufanyia sijui
nani atamuokoa (anacheka)
Colton:(anajimwagia
rangi inayofanana na damu, anachukua kisu anakipaka rangi hiyo kisha
anamhikisha Miriam, anampaka rangi hiyo kwenye nguo zake)
Ariana:
perfect
Colton:(anajilaza
pembeni ya Miriam)
Ariana:
Miriam ataamka baada ya muda gani?
Colton:
kama dakika 15...hivi
Ariana:
polisi watakuwa wapo hapa
Colton:
nenda sasa
Ariana: this
time, naomba usiniangushe hata kidogo sawa ee
Colton:
usijali haya nenda…
Ariana:
nawapigia simu jifanye umekufa …baada ya hapa tutaonana tena nitakupeleka mbali
nitakupa pesa nyingi sana Colton hutaamini macho yako
Colton:
asante sana
Ariana:
poa usiniangushe…(anaondoka)
Colton:(anajilaza
na kujifanya kuwa mfu)
Ariana:(anachukua
simu nyingine tofauti na yake na kupiga simu polisi) hello kituo cha
polisi?
sauti:
ndio karibu tukusaidie…
Ariana:
kuna mauaji yametokea(anawaelekeza)mwanamke Fulani amemuua mtu hapa
sijuini kwanini njooni haraka kwenye eneo la tukio nimeshawaelekeza
Sauti:
asante kwa taarifa...tunakuja muda sio mrefu
Ariana:
asante… (anakata simu anamgeukia Miriam)
Miriam:(bado
yupo kwenye usingizi mzito sana)
Ariana:
umekwisha Miriam (anacheka kisha anaondoka zake)
Colton:(amejikausha
kama mtu aliyekufa kweli)

0 Comments