SCENE
41: -
BAADA
YA DAKIKA 15: -
JIONI
HIYOHIYO: -
(Miriam
anazinduka kutoka kwenye usingizi mzito aliokuwa amelala baada ya kuleweshwa,
anajishangaa kuona ametapakaa damu)
Miriam:
jamani hii damu vipi...na hiki kisu jamani? (anashangaa)kumetokea nini hapa?
(anaangalia pembeni anamuona Colton) oh God Colton…amekufa? (anajingalia
mkononi) nimemuua?
(Polisi
wanafika)
Miriam:
Mungu wangu polisi?
Polisi:
kaa hivyo hivyo ulivyo dada kama hutaki shida
Miriam:(Analia)
sijafanya chochote mimi…sijafanya chochote…mimi sijui nilikuja kuonana na dada
yangu hapa
Polisi
1:(anamfikia anamfunga pingu kisha anamuamuru kusimama) simama
Miriam:(bila
kugoma anasimama)
(Akiongozwa
na polisi anapanda gari)
Polisi
2: tayari tumeshaita ambulance litakuja kuubeba mwili wa kijana huyu aliyeuliwa
na mwanamke mwenye roho mbaya ona ulivyomuua kikatili
Miriam:
sijafaya chochote naapa nieleweni
Polisi:
twende kituoni huko ndo utaeleza vizuri kinagaubaga
Miriam:(analia
sana) naombeni simu yangu
Polisi
2: ipi?
Miriam:
yangu
Polisi 1:
haipo…
(Gari
la kubeba wagonjwa mahututi linafika mahali hapo, wahusika wanabeba mwili wa
Colton na kuuingiza kwenye gari na kuondoka mahali hapo)
Polisi1:
kwakuwa wameshaondoka na sisi tuondoke
(Wanaondoka)
Miriam:(Analia
sana) naomba niongee na mchumba wangu...
Polisi 1:
tukifika huko…
Miriam:(Analia
kwa uchungu)
(Baada
ya mwendo wa takribani dakika kumi na tano polisi pamoja n miriam wanafika
kituo cha polisi kwa ajili ya mahojiano ya awali)
Miriam:(Analia
sana)
Polisi1:
huachi kulia una shida gani?
Miriam:
sijamuua yule mtu haki ya Mungu kwanini hamniamini?
Polisi2:
umekutwa eneo la tukio na ulikuwa umeshika kisu leo hii unasema hujaua
Miriam:
naapa mbele za Mwenyezi Mungu…. sijamuua (Analia)
Polisi
1: acha kulia sasa…
Miriam:
naomba niongee na mchumba wangu
Polisi 2:
una dakika mbili tu (anampa simu)
Miriam:(anabonyeza
namba za Jeremy kisha anapiga)
(Simu
inaita)
Jeremy:(anapokea)
Miriam: Jeremy
(Analia)
Jeremy:(anashangaa)
Miriam?
Miriam:
ndio Jeremy
Jeremy:
nimekupigia simu sana Miriam
Miriam:
nipo polisi Jeremy…wanasema eti nimeua mtu…
Jeremy: (anashangaa
sana) what?? impossible Miriam sa ngapi?
Miriam:
jioni…hii Jeremy
Jeremy:
jamani...eeh Mungu wangu…ngoja nakuja mke wangu nakuja sasa hivi mama
Miriam:(anakata
simu kisha anendelea kulia)
Jeremy:
Oh God…ngoja niwapigia kina mzee Ken maana hii ni tatizo… (anaonekana
kuchanganyikiwa na habari ile nzito na ya kushtua)
(Simu
inaita)
Ken:(anapokea)
naam baba upo na mwenzio…?
Jeremy:
hapana baba yupo kituo cha polisi
Ken:
what? impossible. kafanya nini? Jamani huyu mtoto mbona ana majanga hivi
kafanyaje? Embu Jeremy niambie mbona unanichanganya?
Jeremy:
hata mimi sijajua baba mimi mtanikuta kituoni (anakata simu)
Ken:(anashangaa)
oh my God… (anabaki ameduwaa)
0 Comments