MUNGU MKUU 42


 

SCENE 42: -

USIKU HUO HUO

NYUMBANI KWA MZEE KEN: -

(Mzee Ken anagonga mlango wa Ariana, anaonekana kuchanganyikiwa kwa habari ile ya kushangaza na kusikitisha)

Ken:(anagonga mlango)

Ariana:(anajifanya kutoka kwenye usingizi mzito)

Ken: umelala mapema sana leo kwanini?

Ariana: nilikuwa najisikia vibaya sana…nimelala tangu saa kumi…

Ken: anyways tuna tatizo

Ariana:(anajisemea moyoni) kumekucha (anajichekea moyoni)

Ken: mdogo wako yupo kituo…cha polisi sijui amefanya nini…

Ariana: nani amekuambia?

Ken: Jeremy

Ariana: aisee…atakuwa amefanya nini?

Ken: sijui…nimeshawaambia mama yako na mama yako mdogo wananisubiri nje kwenye gari nimekuja kukuamsha tuondoke mdogo wako anatuhitaji

Ariana: sawa baba…ngoja nivae

Ken: usichelewe

Ariana:(anaingia ndani) mambo yamekuwa mambo…(anafyonza)alidhani ameniweza kumbe kajiweza mwenyewe mjinga huyu…na ataozea jela mshenzi yule (anavaa)

Ken:(akiwa nje ya chumba kile) Ariana bado…

Ariana: nakuja dad… (anatoka nje) haya twende

(Wanatoka nje walipo Keddy na Mary)

Ken: haya jamani tunaweza kwenda (anapanda kwenye gari kisha anawasha gari)

Mary:(anasali moyoni) Mungu mwanangu namuweka mikononi mwako wewe ni Mungu mkuu tenda miujiza tangu kale umekuwa ukimtetea mwanangu naomba tena utende miujiza tena baba…onyesha ukuu wako mfalme naomba mwanangu apone kwenye janga hili sina cha kuongeza Zaidi

(Safari inaendelea)

Ariana:(anajisemea moyoni) maskini wamechanganyikiwa wengine si cha ajabu wanaombea akombolewe (anamuangalia Mary)

Mary:(anaendelea kuongea moyoni) najua Ariana ndo kafanya haya ila naamini ukuu wa Mungu ni wa ajabu na kila kitu kitakuwa sawa kwa jina la Yesu

(Hatimaye wanafika)

Ken: tumefika jamani…tuombe sana

Keddy: yaani hata sielewi amefanya nini...kwani Jeremy kasemaje?

Ken: ndo tuingie tukasikie

Mary:(anavuta pumzi ndefu)

Ken: tulieni kila kitu kitakuwa sawa

(Wanaingia ndani ya kituo)

Jeremy:(ameshafika amemkumbatia mpenzi wake)

Ken:(anawafikia) nambie…za hapa…mama (anamuangalia Miriam)

Miriam:(Macho yamemvimba kwa kulia sana)

Ken: pole mama…nambie nini shida kwanini wamekuleta na hizi damu imekuwaje embu niambie

Miriam: baba sijaua mimi…

Mary: kwanini unaongelea kuhusu mauaji...?

Miriam:(kwa Mary) Colton amekufa…

(Wanashangaa)

Miriam: dada Ariana aliniita

Ariana: loh acha uongo…mimi nimerudi nyumbani hata ma mdogo anajua

Keddy: hata mimi nilimuona na hakutoka

Ariana:(kwa Miriam) utakuwa unaota

Miriam: labda, ila kuna mtu alinipigia nimefika pale sijui ikawaje nakuja kuamka nakuta nimeshika kisu na maiti ya Colton pembeni yangu

Ken: aisee…mbona moja kwa moja inaonekana ni mchezo?

Miriam: ndo najaribu kuwaaambia hapa hakuna anayeniamini wameniambia nitalala hapa

Jeremy:(anasikitika sana)

Miriam: nafungwa maana nimeambiwa kila ushahidi unaonyesha kuwa mimi ndo nimeua…

Jeremy: yaani hata sijui nitafanyaje…sijui naanzia wapi kukusaidia yaani hata sielewi na wewe nakwambiaga usiwe unaenda sehemu peke yako

Miriam:(Analia sana)

Ken: basi sio muda wa kulaumiana kwa chochote kwa sasa embu tufikirie tunafanyaje kwa hili ili tutatue hili tatizo

Jeremy: tuanzie wapi?

Ken: tutafute mwanasheria nitampigia kesho family lawyer wetu ili tuanzie hapo tujue tunafanya nini

Jeremy: wamekata kumuachia wamesema kuwa atalala hapa na kesi itasikilizwa haraka iwezekanavyo

Mary: Mungu wangu

Miriam:(Analia sana)

Jeremy: Miriam acha kulia jamani

Miriam: sijaua mimi jamani nashindwa kuelewa imekuwaje

Polisi 1: muda umeisha naomba muondoke na mtuhumiwa anatakiwa aingie selo

Miriam:(anavua pete na kumkabidhi Jeremy) nishikie…

Jeremy:(Analia) Miriam

Miriam:(anaondoka)

Jeremy: jamani Miriam (anaweka mfukoni pete ile)

Miriam:(anavua viatu anapewa nguo nyingine)

(Ndugu zake pamoja na mchumba wake wanabaki wanasikitika)

Mary:(Anazimia)

Miriam:(anageuka kuwachungulia Analia sana)

Jeremy:(Analia sana) Miriam mpenzi wangu…kipenzi changu…

Ariana:(anacheka chini chini huku anajisemea moyoni) kutesa kwa zamu wakati nalia wao walicheka sasa mimi nacheka wao wanalia haya Maisha bwana (anacheka sana)

(Ken na mkewe wanamsaidia Mary aliyezimia)

Jeremy: Mungu naomba uonekane kwenye hili nina uhakika kua mke wangu hajatenda hili…

Ariana:(anajisemea moyoni) umerudishiwa hiyo pete nitafanya juu chini niivae mimi…

Jeremy:(Analia sana)

Ken: twendeni tutarudi kesho…tutarudi na mwanasheria…

Jeremy: mimi nalala hapa…

Ariana:(anamshika Jeremy) shemeji…

Jeremy: embu niache mimi(anamsukuma)

Mary:(anazinduka baada ya kupepewa na Keddy kwa muda mrefu)

Ken: twendeni nyumbani

Jeremy:(anajisemea moyoni) nitalala chini mpaka siku unatoka Miriam (wanaondoka)

Post a Comment

0 Comments