SCENE
43: -
KESHO
YAKE ASUBUHI
KITUO
CH POLISI: -
(Ndugu
wa Miriam wakiwa pamoja na Jeremy wanafika kituo cha polisi ili wajue maendeleo
ya kesi ya Miriam sambamba na wao yupo pia mwanasheria mzuri sana mjini hapo)
Afande
1: karibuni
(Wanaitikia)
Afande
1: niwasaidie nini?
Ken:
tumekuja na mwanasheria sisi ni ndugu wa Miriam yule binti…
Afande
2: tunamfahamu huyo binti amekesha anasali tu yaani hajalala…
Jeremy:
(anainamisha kichwa)
Ariana:
(anajisemea moyoni) umekwisha hakuna atakayekuokoa Miriam (anacheka)
Mary:
Mungu wetu ni mkuu…kama alimvusha usiku wa giza na mvua nyingi hakudhulika hata
hili atamvusha…mwanangu atakuwa huru
Keddy:
kabisa atakuwa huru nina Imani
Mwanasheria:
tunaomba tumuone
Afande
2: bila shaka kabisa… (anaenda kumuita na baada ya dakika kadhaa anarudi na
Miriam)
Jeremy: (anamuona)
oh dear (anamuendea na kumkumbatia)
Ken:
yataisha tu kijana wangu…wala usiogope
Ariana:
(anafyonza moyoni) jipeni moyo (anatabasamu)
Jeremy:
umelalaje?
Miriam: (machozi
yanamtoka)
Keddy:
usijali mwanangu haki ya Mungu tena utatoka labda sio Mungu tunayemuabudu
Ariana:
(anajisemea moyoni) hawa watu wanachekesha sana
Mwanasheria:
okay tuanze ili tusipoteze muda maana tuna mambo mengi sana…
(Wanakaa)
Miriam: (anakaa
pembeni ya Jeremy)
Jeremy: (anamshika
mkono Miriam)
Ariana:
(anachukia kuona kitendo kile)
Mwanasheria:
hii kesi ngumu maana kila ushahidi unaonyesha kabisa kuwa Miriam ameua
Ariana:
(anafurahi sana lakini bila kumuonyesha mtu)
Mwanasheria:
lakini kuna tumaini kama mnavyosema Mungu wetu ni mkuu sana na maajabu yake ni
ya pekee hakuna wa kupingana nae anapoamua kutupigania
Mary: (Analia
sana)
Keddy: Mary
acha kulia hili litaisha
Jeremy:
Dah (anakuna kichwa)
Mwanasheria:
sasa (kwa Miriam) embu niambie ilikuwaje siku ile?
Miriam: (anamuangalia
Ariana)
Jeremy: (anagundua)
vipi mbona unamuangalia Ariana?
Miriam: dada
alinipigia simu
Ariana:
relax dogo una wenge najua unayopitia ni mazito tupo hapa kukusaidia ila
usiniingize kwenye huo msala tafadhali
Keddy: Ariana
alikuwepo nyumbani hakutoka kabisa chumbani kwake
Ariana:
(anajisemea moyoni) nilipitia dirishani
Jeremy:
lakini pia Miriam sio mjinga kusema hili mara ya pili
Ariana:
shemeji…
Ken:
haya nyamazeni…
Mwanasheria: enhe sawa alipokuita?
Miriam:
nikaenda ila sikumkuta… nimekaa pale kidogo sijui kilitokea nini ila nilipoamka
nikakuta nina damu na kisu mkononi
Mwanasheria:
sasa kwani mwili wa marehemu uko wapi?
Afande:
(amesimama pembeni yao) umeshazikwa
Mwanasheria:
hauwezi kuzikwa kabla haujafanyiwa vipimo yaani fingerprints na kadhalika
Ariana:
(anaanza kuogopa)
Afande:
ulipimwa…ukakutwa kweli kuna alama ya vidole ya mtuhumiwa
Jeremy:
(anashika kichwa)
Miriam:
I swear Jeremy sikumgusa yule mtu na kwanini nitake kumuua yule kaka hata
simfahamu?
Ariana:
acha uongo Miriam alikuwa bwana wako na alikuja akatuambia labda ulichukia
alipokuja kukusemea ukaona usije ukapoteza danga lingine ambalo lina pesa Zaidi
ukaona umuue una roho mbaya sana
Jeremy: (kwa
Hasira huku anamnyooshea kidogo Ariana) Ariana…one more word na nitasahau kama
wewe ni shemeji yangu kwanini unaongea uongo wa wazi kabisa
Ariana:
kwahiyo mnamuamini sana Miriam?
Ken:
hiyo sio kesi tunataka kupata ufumbuzi juu ya hili suala ili tumtoe mwenzetu
Mwanasheria:
(anakaa kimya huku kuna kitu anafikiria sana)
Jeremy:
something is not right… hapa
Mary: (Anajifuta
machozi)
Afande:
sasa kwasababu ushahidi umeshakusanywa hatuna budi kumpeleka mahakamani
Jeremy:
(anasikitika)
Afande:
na adhabu yake ni kunyongwa hadi kufa
Mary: (analia
sana) onekana Mungu wa majeshi mwanangu sio muuaji mwanangu mimi hajafanya
chochote…Mungu umemvusha kwenye mambo mengi sana mwanangu usiruhusu Mungu
mwanangu afe akiwa mdogo hapana Mungu bado namuhitaji mwanangu nataka
wajukuu…ukimchukua mwanangu nitaishije mimi Mungu (Analia sana) onekana
Mungu wangu jamani baba yangu (analia sana)
Keddy: (anambembeleza
Mary) ataonekana tu
Jeremy:
Mungu onyesha dunia kuwa wewe ni mkuu
Miriam:
(Analia sana)
Ken: (anafuta
machozi)
Ariana:
(anajisemea moyoni) yaani wanalia kabla ya msiba? Wanachekesha
Mwanasheria:
sijawahi kukutana na kesi iliyoshika moyo wangu kama hii…hata mimi naamini
kabisa kuwa hujaua… (kwa afande) naweza kupata nguo alizokuwa amevaa?
Miriam:
hazionekani…
Mwanasheria:
(anashangaa) kuna kitu hakijatulia hapo
Ken:
hata mimi naona
Mwansheria:
sawa haina shida acha sisi twende tutarudi... (kwa Miriam) tutalimaliza
Miriam:
sawa
Jeremy:
(anampa chakula) kula…please jitahidi nitakuja tena baadae
Miriam:
(kwa unyonge) sawa
Jeremy:
I love you
Miriam:
me too
Ariana:
(anajisemea moyoni) jipeni moyo
Afande:
(anamchukua na kumrudisha rumande)
(Ndugu,
mwanasheria pamoja na Jeremy wanaondoka huku wote wakiwa wamejaa uchungu na
huzuni)
0 Comments