MUNGU MKUU 44


 

SCENE 44: -

OFISINI KWA JEREMY: -

(Jeremy yupo ofisini kwake amesimama anaanngalia nje kupitia dirisha lake kubwa liliopo ofisini kwake, anaonekana ana mawazo mengi sana, anajikuta machozi yanamtoka)

Anita: (anaingia) samahani boss

Jeremy: (anafuta machozi kisha anageuka) naam

Anita: (anamuangalia kwa umakini) ulikuwa unalia boss?

Jeremy: hapana acha tu

Anita: shida nini?

Jeremy: kipenzi changu amewekwa ndani Anita

Anita: Mungu wangu amefanya nini?

Jeremy: acha tu… (anabadilisha mada) enhe nambie nini shida?

Anita: kuna watu wawili nadhani mmoja ni rafiki yake wifi na mwingine

Jeremy: oh, waambie waingie nilikuwa nawasubiri sana

Anita: sawa (anatoka)

Jeremy: (anakaa kwenye kiti kuwasubiri waingie)

(Mwanasheria na Vanessa wanaingia)

Vanessa: shemeji

Jeremy: naam shemeji yangu

Vanessa: shikamoo

Jeremy: marahaba karibuni

Mwanasheria: (anampa mkono) habari yako bwana Jeremy

Jeremy: ah nipo nipo tu nimepoteza furaha kabisa…mpenzi wangu yupo jela

Vanessa: sijaenda kumuona naona uchungu

Jeremy: acha tu shemeji

Mwanasheria: wameshamuamishia jela ni vigumu kuomba dhamana

Jeremy: (Analia) ningejua ningemtorosha tukaenda kuishi mbali mimi ningekuwa nakuja tu jioni narudi huko mbali

Mwanasheria: usikate tamaa na naomba ujikaze halafu ukiwa unaenda usiwe unalia ukilia yeye atakosa hata nguvu ya kuendelea kuishi she needs us more than ever…

Jeremy:  yes, sure hata hivyo nimekuwa nikijikaza sana kila nikiwa mbele yake

Mwanasheria: unafanya vyema sana

Jeremy: (anashusha pumzi) anyways advocate embu niambie kitu hapa kesi imekaaje?

Mwanasheria: ina utata

Vanessa: sijaelewa hapo…ina utata kivipi?

Jeremy: mwili wa marehemu umezikwa kabla ya uchunguzi wowote

Jeremy: lakini walisema wamefanya uchunguzi

Mwanasheria: sidhani na kitu kingine nguo alizokuwa amevaa Miriam…zimepotea ghafla

Jeremy: hata mimi niliona kuna utata hapa kwakweli

Mwansheria: na kitu kingine ni statement ya Miriam

Jeremy: ile ya kusema alipigiwa simu na Ariana…

Mwansheria: tungepata simu ya Miriam

Jeremy: simu yake imepotea

Mwanasheria: tunaweza kuomba statement ya simu zake kwa siku hiyo

Jeremy: yes, tujaribu hapo tukipata tutapata uhakika kuhusu Miriam kuwasiliana na Ariana

Mwanasheria: exactly…

Vanessa: Ariana atakuwa amehusika sana kumpeleka Miriam jela

Jeremy: wewe umenena shemeji yangu

Mwanasheria: kwanini mnasema hivyo?

Jeremy: (anaguna) ni muhimu nikuambie…unajua nilikuwa ni kijana niliyejitosheleza nilikuwa nina biashara za kutosha sio nilikuwa mpaka leo nina biashara nyingi tu ila sasa sikuwa na mwanamke wa kuniliwaza kwa kifupi mke…

Mwanasheria: (anasikiliza kwa makini)

Jeremy: kila nikiangalia nikawa sioni nikaona niombe msaada kwa wazazi wangu wanisaidie kutafuta mke…ndipo walipoenda katika familia ya mze Ken yaani baba yao kina Miriam wakaomba uchumba na Ariana…siku naenda kutambulishwa rasmi nikamuona Miriam…I swear nikampenda sana…sikuchelewa kumueleza hisia zangu na kwa uoga akawa kigeugeu mara akubali mara akatae…mwisho akakubali tukaanza mahusiano…mara Ariana akajua...akajifanya ameridhia kumbe ana lake jambo..akawa anafanya vituko bila sisi kujua mara amteke Miriam mara sijui afanye nini yaani chuki tu

Mwanasheria: nimeielewa vyema stori yako kwa maana nyingine Ariana ametengeneza uadui na Miriam kisa wewe Jeremy

Vanessa: hapana Miriam sio mtoto wa mzee Ken ila walimchukua na kumlea kama mtoto wao kabisa sasa hilo hakikumpendeza Ariana hivyo sasa alikuwa anamchukia Miriam tangu enzi za zamani sio tu kwasababu ya Jeremy kwa maana nyingine Ariana anaona Miriam anamuibia vitu vyake hivyo anamuona adui

Mwanasheria: I see

Jeremy: ndo hivyo…everything makes sense

Mwanasheria: exactly…sasa (kwa Vanessa) kwa maana nyingine naomba usimame mahakamani kuwaambia haya unayoniambia sasa hivi…

Vanessa: sawa mwanasheria nitafanya kila kitu kwa ajili ya rafiki yangu

Mwanasheria: safi…ni lazima niinue mjadala kuwa Ariana aliwasiliana na Miriam kabla ya tukio na ana sababu za kutosha za kutaka kumuingiza Miriam kwenye shida ilia pate upendo anaohisi Miriam kamuibia…

Jeremy: yes…

Mwansheria: kila kitu kitaenda sawa lakini Zaidi tunauhitaji ukuu wa Mungu uonekane

Vanessa: kabisa

Mwanasheria: huwa mnasali?

Vanessa: sana

Jeremy: Miriam amenifundisha kusali mtoto anasali yule kwakweli mahusiano yake na Mungu ni ya karibu sana

Mwansheria: ndo maana anampigania nimesikia historia yake kwa kipande kipande lakini nimeelewa kuwa ni mbarikiwa.

Jeremy: hata hili litapita ingawa (anaguna)

Mwansheria: nini?

Jeremy: inanisumbua sana yaani sijui tu

Mwanasheria: acha tusubiri

Vanessa: mnaenda lini tena?

Jeremy: yaani mimi naenda kila saa…asubuhi naenda mchana naenda na usiku naenda

Vanessa: ukiwa unaenda niambie twende wote

Jeremy: haina shida shemeji yangu

Mwanasheria: okay acha niende nikajiandae na kesi mahakamani itakuwa ngumu lakini najua tutafanya kitu

Jeremy: nakutegemea sana

Mwanasheria: sawa (ananyanyuka anampa mkono Jeremy) basi nikuache uendelee na ujenzi wa taifa

Jeremy; siwezi bila kipenzi changu

Mwanasheria: yataisha tujipe moyo

Jeremy: kwakweli

Vanessa: (ananyanyuka) na mimi naondoka ila ukiwa unaenda naomba unipigie ili twende wote

Jeremy: bila shaka kabisa

(Wanaondoka huku Jeremy anabaki akiendelea na kazi zake)

Post a Comment

0 Comments