MUNGU MKUU 58


 

SCENE 58: -

BAADA YA MIEZI MIWILI

HARUSI YA COLTON NA VANESSA: -

(hayawi hayawi mbona yamekuwa walisema haolewi mbona kaolewa, ndugu, jamaa na marafiki wa Vanessa na Colton wamekusanyika pamoja katika kanisa la Tanzania Assembly of God kushuhudia muungano wa wawili hao)

Miriam: (yupo ndani ya gari lililopambwa kwa ajili ya bibi harusi) wow rafiki yangu hatimaye umekuwa wifi yangu

Vanessa: nani alidhani kuwa mimi na wewe tungekuja kuwa ndugu kabisa… (anacheka kidogo) nani alijua kuwa mimi na wewe tungekuja kuwa karibu Zaidi

Miriam: nakupenda sana Vanessa na Zaidi nashukuru kwa kuja katika maisha ya kaka yangu

Vanessa: oh, Miriam my dear friend

Miriam: sio friend ni wifi

(wanacheka kisha wanakumbatiana)

Miriam: tutoke dear wasije wakapaniki wakidhani tumegoma kushuka kwenye gari

(wanacheka)

Vanessa: tushuke shoga yangu asije Colton akaanza kupaniki na hivi anajua kuchanganyikiwa

(wanacheka)

Miriam: (anashusha pumzi) it is time

Vanessa: (anashuka amependeza kuliko kawaida) Miriam watu wako wapi?

Miriam: (anacheka) wapo ndani wifi wewe ndo malkia unaingia wa mwisho na utakapoingia kila mmoja atasimama

Vanessa: my dream came true dear

Miriam: absolutely (anamsindikiza mpaka mlangoni kisha anamuacha)

Vanessa: mbona unaniacha?

Miriam: tulia halafu tabasamu mlango unafunguliwa mlango muda sio mrefu

Vanessa: (anashusha pumzi)

(mlango unafunguliwa)

Colton: (anamuona mkewe mtarajiwa) wow… she is so beautiful

Vanessa: (anagongesha macho na mumewe mtarajiwa anatabasamu)

Colton: (anatabasamu)

(watu wananyanyuka)

Vanessa: (anaanza kupiga hatua kuelekea alipo mumewe mtarajiwa)

Colton: (anamsubiri kwa hamu kubwa)

Watu: (wamesimama wengine wanampiga picha)

Ariana: (anamuangalia Vanessa) jamani kamependeza kweli yaani

Mary: wow…amenoga...jamani mtoto

Miriam: (amekaa pembeni ya baba mtoto wake) wow jamani karafiki kangu kamependeza sana

Colton: (anajiweka vizuri kisha anatabasamu)

Vanessa: (anakaribia kufika alipo mumewe mtarajiwa)

Colton: I can’t believe she is going to be my wife in few minutes

Ariana: eeh Mungu hata mimi natamani sana kuolewa natamani sasa na mimi nipate wangu…najua nilikukejeli ilikuwa ni ujinga tu sasa nakiri ukuu wako naomba unionyeshe kweli na mimi natamani kuolewa

Vanessa: (anafika alipo Colton anatabasamu kisha anamshika mkono)

Colton: (anapanda nae alipo mchungaji)

Vincent: (anatabasamu) mwanangu

Colton: (anaongea kwa kunong’ona) umependeza mpenzi wangu

Vanessa: (anamuangalia kwa aibu) asante

Colton: (anatabasamu)

Mchungaji: (kwa utani) kama mmeshamaliza kuchekeana tuendelee na ratiba nyingine

(watu wanacheka sana)

Colton: (anacheka pia)

Mchungaji: embu mfunue isije ukawa unamchekea mke wa mtu mwingine

(wanacheka)

Colton: (anamfunua) wow

Vanessa: (anacheka)

Mchungaji: wow ee (anacheka huku anatikisa Kichwa) mrembo eeh

Colton: (anacheka) ndio

Mchungaji: ndo yeye??

Colton: hakika

Miriam: (anacheka)

Mchungaji: basi sawa... (kwa watu) bwana Yesu asifiwe kanisa

Watu: amina...

Mchungaji: ndugu zangu leo tumekusanyika hapa kushuhudia muungano kati ya Colton Vincent Mshana na mwenzake Vanessa Emmanuel Mpejiwa

Watu: (wanasikiliza kwa makini)

Mchungaji: (kimya kidogo)

Colton: (anatabasamu)

Mchungaji: (kwa Colton) Colton je unamchukua Vanessa Emmanuel Mpejiwa kuwa mke wako wa ndoa na kwamba utamlinda, kumheshimu na kumpenda siku zako zote za maisha mpaka pale kifo kitakapowatenganisha?

Colton: ndio

(watu wanashangilia)

Mchungaji: (kwa Vanessa) Vanessa je upo tayari kumchukua Colton Vincent Mshana kuwa mume wako wa maisha kwamba utamheshimu, na kumpenda siku zote za maisha yenu mpaka pale kifo kitakapowatenganisha?

Vanessa: ndio

(watu wanashangilia)

Mchungaji: basi kwa ukiri wenu kifuatacho ni zoezi la pete

(watoto wawili wanaleta pete mmoja anampa Colton na mwingine anampa Vanessa)

Vanessa: (anaipokea na kukaa nayo)

Colton: (anafanya hivyo pia)

Mchungaji: naomba mgeukiane…

(wanafanya hivyo)

Mchungaji: nitakuwa nasema maneno unayafatisha…naanza na mwananume…mshike mkono mwenzio na kusema maneno haya…mwenzangu pokea pete hii

Colton: (anafata)

Mchungaji: iwe ishara ya mapendo na uaminifu wangu kwako…

Colton: (anafata)

Mchungaji: kwa jina la baba, na la mwana na la roho mtakatifu

Colton: (anafata huku anamvalisha pete)

Watu: (wanashangilia baada ya kuona Colton amemvalisha pete kwa ukamilifu)

Mchungaji: (kwa Vanessa) utafanya kama alivyofanya mwenzio

Vanessa: (anaitikia)

Mchungaji: mwenzangu pokea pete hii

Vanessa: (anarudia maneno yale)

Mchungaji: iwe ishara ya mapendo na uaminifu wangu kwako…

Vanessa: (anarudia)

Mchungaji: kwa jina la baba na la mwana na la roho mtakatifu…

Vanessa: (anarudia huku anamvalisha pete)

Mchungaji: safi sasa… alichokiunganisha Mungu mwanadamu asiweze kukitenganisha

(watu wanashangilia)

Vanessa: (anamgeukia Miriam kisha anatabasamu)

Miriam: (anatabasamu) hongereni sana

Mchungaji: basi ndugu zangu nawatangazia kwenu bwana na Bibi Colton Mshana

(kanisa linalipuka kwa shangwe na nderemo)

Mchungaji: (kwa maharusi) naomba mje mnisainie vyeti vya ndoa…hongereni sana

Colton: (anamkumbatia mkewe)

Mchungaji: oh, samahanini sikuwaambia mpongezane

(watu wanacheka)

Vanessa: (anamkumbatia mumewe)

Miriam: (anafurahi sana)

Vanessa: (anatabasamu)

(maharusi pamojana washenga wao wanasaini vyeti vya ndoa)

Mchungaji: basi sawa mmekuwa mume na mke kamili

(maharusi wanawaonyesha watu vyeti vyao vya ndoa)

Watu: (wanafurahi sana)

Jeremy: oh, hatimaye wametimiza lengo lao

Miriam: na sisi Mungu atufanikishie…

Jeremy: ni miezi miwili tu imebaki mimi na wewe tufunge ndoa mpenzi wangu…

Miriam: oh, Jeremy wangu baba G wangu nakupenda sana

Jeremy: mimi Zaidi

(watu wanaendelea kuwapongeza maharusi kwa kufunga ndoa takatifu, maharusi wana furahi sana, picha nyingi za ukumbusho zinapigwa na kila mtu anaonekana kuwa na furaha kubwa sana)

Post a Comment

0 Comments