SCENE 1: -
(Ni usiku mmoja mtulivu sana,
mwezi angani unang’aa vizuri na kila kitu kina kinaonekena kipo katika utulivu,
katika nyumba iliyo na giza kuna mtu anaonekana anaingia ndani kwa mwanaume
mmoja ambae anaonekana amelala usingizi fofofo, lakini ghafla yule mtu
aliyeingia anamchoma kisu mara kadhaa mwanaume yule aliyekuwa amelala)
Mwanaume
:( anashtuka na anajihisi maumivu makali sana)
jamani… (Kwakuwa ni giza haoni) we
nani?
Mtu
:( anaendelea kumchoma kisu)
Mwanaume:(anaishiwa nguvu na kupoteza maisha hapo
hapo)
Mtu:(ananyanyuka maana alikuwa amekaa)
pumbavu… (anachukua dumu lililokuwa
limejaa mafuta ya taa kisha anaanza kuyamwaga sehemu mbalimbali za nyumba ile
anafanya hivyo kwa muda na mwisho anawasha kiberiti kisha anatupia halafu yeye
anakimbia)
(Nyumba inawaka moto ambao unawashtua
majirani waliokuwa bado wako nje)
Mmoja
wa majirani: jamani oneni nyumba ya Robert inawaka moto jamani…
Mama
mmoja: eeh maskini wa Mungu halafu alikuwa amelala ndani
Jirani
mwingine: twendeni tukasaidie kuuzima pengine tunaweza kumuokoa Robert
(Haraka majirani wanakimbilia kwa
bwana Robert ili wamuokoe maisha, na kuuzima moto ule)
Mama:
kwanini tusiwaite zima moto jamani hivi tutaweza kweli?
Mmoja
wa majirani: mama Mgata upo sawa kabisa
Mwingine:
tatizo huwa wanachelewa sana embu tujaribu
(Wanaendelea kumwaga maji wengine
wanamwaga mchanga na wengine wanapiga simu kwa ajili ya msaada wa zima moto na
wengine wanaita majirani wengine)
Mama:
sijui kama Robert atakuwa mzima humo ndani huu moto ni mkubwa sana sijui
umesababishwa na nini
Jirani:
labda umeme…
(Wakati wanaendelea kuhangaika kuuzima moto huo,
gari la zima moto linakuja na haraka askari wa zima moto wanaanza kazi yao,
wanauzima moto huo kwa muda na hatimaye wanafanikiwa kuuzima. haraka wanaingia
ndani kuangalia mtu aliyekuwepo ndani wanatoa mwili uliokuwa tayari umeungua
vibaya sana na mtu yule alikuwa ameshafariki dunia)
Mmoja
wa askari wa zima moto: tunasikitika kusema huyu mtu ameshafariki dunia…cha
kufanya ni nyinyi kutoa taarifa polisi kuwa mtu huyu ameshafariki dunia
(Majirani wanasikitika sana)
Askari
zima moto: cha msingi ngoja niite ambulance iupeleke mwili mochwari iili
uhifadhiwe huko na kusubiri taratibu nyingine
Mama:
yaani tunasikitika sana baba wa watu hakuwa na makuu na mtu alikuwa ni mtu wa
watu
Askari:ni
mpango wa Mungu
Mama:(Analia sana)
Askari:
familia yake iko wapi?
Mama:
wapo nchi za nje mke na watoto wake
Askari:(anapiga simu, inaita na hatimaye inapokelewa)
ndio kuna mwili wa mtu mmoja umekutwa kwenye tukio la ajali ya moto…tafadhali
naomba mje muuchukue ili uhifadhiwe katika chumba cha kuhifadhia maiti
Sauti:
sawa nielekeze tunakuja baada ya muda
Askari:
nakuandikia meseji sasa hivi
Sauti:
sawa na asante sana kwa taarifa
Askari:(anakata simu kisha anaandika meseji)
sasa ni muhimu familia yake ikajua ili ipango ya mazishi ianze
Mama:
sawa
Askari:
hivyo vingine vitafanywa na mapolisi…sisi kazi yetu tumemaliza...
(Baada ya dakika kama kumi na tano,
ambulance inafika mahali pale, haraka wafanyakazi wa hospitali ile wanashuka)
Kijana:
jamani habari zenu
Majirani:
salama…
Kijana:
poleni kwa msiba huu…
Majirani:
asante
(Yule kijana pamoja na wenzake
wanachukua machela kisha wanabeba mwili wa bwana Robert na kuuweka kwenye
ambulance kisha wanaondoka eneo hilo la tukio)
Askari:
basi sawa sisi…ngoja na sisi tuondoke poleni sana kwa tukio hili la kutisha
Majirani:
asante sana
(Askari wa zima moto na wenzake
wanaondoka mahali pale, huku wakiwaacha majirani wakiongea mambo tofauti
tofauti)
Mama:
yaani nimesikitika sana kifo cha huyu mtu...
Jirani:
acha tu mama Neema…embu yafikirie mateso aliyoyapata huyu bwana kabla
hajafa…yaani ameungua sana…vidonda mwili mzima…
Mama
Neema: yaani acha tu halafu jumba lake limeungua lote lilikuwa bonge la jumba…yaani
Hassani nimesikitika mwenzio
Hassan:
hunizidi hata kidogo
Jirani
mwingine: ndo hivyo kila mmoja wetu ataonja mauti…njia yetu sote hivyo
tusikitike jamani
(Wakati huo anakuja binti mmoja mwenye umri
kati ya 23 au 24 ni mjamzito kati ya miezi mitano au mine nay eye anaonekana
anaishi jirani hapo)
Binti:
jamani kuna nini…nimesikia ving’ora vingi sana kuna nini?
Mama
Neema: acha tu mdogo wangu…Bw. Robert kafariki kwenye ajali ya moto
Binti:
maskini…inauma sana
Mama
neema: sasa wewe umekuja juzi tu…sisi tuliyomuona kuanzia ndo anaanza kujenga
nyumba yake yaani tumeumia sana
Binti:
maskini…hatuna budi kumshukuru Mungu…
Mama
Neema: kweli…hivi nimekuona hii ni wiki ya pili si umepanga chumba kimoja humo
kwetu…nakuonaga unatoka na kuingia hata sikufahamu jina lako
Binti:
naitwa Josephine au Liliana….
Mama
Neema: ah!!sawa hilo la kwanza gumu ngoja nikuite Liliana au we unasemaje?
Liliana:
sawa tu, ingawa jina nililozaliwa nalo ni Liliana au niite JO...
Mama
Neema: sawa...haina shida…
Liliana:
sawa najisikia vibaya na ishakuwa usiku sana ngoja nikalale tutaonana kesho
asubuhi
Mama:
sawa Jo
Liliana:(anaondoka zake)
Mama
Neema: jamani mnaonaje na sisi tukapumzike tutaonana kesho asubuhi
(Majirani wanakubaliana na kila
mmoja wao anaenda nyumbani kwake maana imeshakuwa usiku sana…wanapoondoka anakuja
yule mwanamke aliyemuua Robert na kuchoma nyumba yake, haonekani sura na wala
hatambuliki kirahisi ila tu ni mwanamke)
Mwanamke: sasa nafsi yangu
imeridhika…wanaume wamekuwa ni watu wa baya sana kwangu… huyu alinichkulia kitu
nilichokithamini sana katika Maisha yangu,hicho kitu ni cha thamani sana kwangu
kisa mapenzi nilishindwa kumsamehe kabisa huyu alinichukulia dhaifu…
alinidharau na kunikejeli nilishindwa kumsamehe Mungu wangu naomba unisamehe
kwa hili najua nimekosea sana ila ilibidi nifanye maana alinisumbua sana
huyu mwanaume nimemkomesha (anacheka kidogo) apumzike kwa amani (bila
kuonekana uso anaondoka zake)
1 Comments
Hello my friends and family,thank you for your love and support,story ya kwanza imeisha nimeanza story mpya tafadhali naomba muendelee kuniunga mkono asanteni na ninawapenda sana
ReplyDelete