SCENE 59: -
BAADA YA MIEZI MIWILI: -
HARUSI YA RAPHAEL NA LILIANA: -
(Ni siku nzuri tena iliyopambwa
vyema Kwa hali ya hewa nzuri yenye upepo mwanana kutoka bahari ya Hindi,
Liliana amekaa katika chumba kidogo cha kubadilishia nguo amevaa gauni la
maandalizi (robes) amekaa anaonekana ana mawazo sana lakini Zaidi ana furaha
sana)
Liliana:
maisha yangu yote nimekaa naiwazia hii siku…siku hii ni ya muhimu sana
kwangu…finally naenda kufunga pingu za maisha
Bianca:
(anaingia) mama
Liliana:
(anamnyanyua na kumuweka kwenye paja
lake) mwanangu… (Anambusu) umependeza
sana mama yangu
Bianca:
(anatabasamu) wewe ndo umependeza
Liliana:
muongo mimi hata sijavaa gauni langu
Anna:
(anaingia akitokea nje) binamu
Liliana:
yes binamu
Anna:
hujajiandaa tu yaani huko mumeo anapiga simu kila mara
Liliana:
(anacheka) na yeye akae Kwa kutulia
jamani
Anna:
lazima awe na wasiwasi
Liliana:
asijali bwana
Anna:
(anakaa kimya huku anamuangalia)
Liliana:
(anatabasamu) nini binamu
Anna:
historia ya maisha yako ni historia nzuri sna yenye mafunzo mengi
Liliana:
oh binamu
Anna:
umepitia mengi sana Liliana lakini pamoja na hayo hukuwahi kukata tamaa
umesimama na Imani yako mpaka mwisho
Liliana:
oh binamu
Anna:
leo unaolewa kipenzi yaani nina furaha sana
Liliana:
(ananyanyuka na kumkumbatia)
Anna:
natamani shangazi na mjomba wangekuwepo au mama na baba yangu au aunt Bianca
Liliana:
(machozi yanamtoka)
Anna:
usilie Liliana yameisha si umeshasamehe? Yameisha mama
Liliana:
yes, yameisha binamu
Bella:
(anaingia) jamani bibi harusi hata
hajavaa? Na mama mkwe wako anakuja
Liliana:
acha aje tu
Lydia:
(anasukuma mlango kidogo kasha
anachungulia) jamani tunachelewa kanisani (anamuita Bianca) twende tutangulie
Bianca:
(anamfuata Lydia na kuondoka nae)
Lydia:
fanyeni haraka (anaondoka na Bianca)
Liliana:
haya nivalisheni
(Anna na Bella wanamvalisha gauni lile kubwa
lenye nakshi kila mahali ama hakika ni gauni la kifahari, baada ya kuhangaika
kwa muda wanamaliza kumvalisha)
Anna:
haya twendeni
(Wanatoka nje wanakutana na kundi
kubwa la kina mama wanaowapokea kwa vifijo na nderemo nyingi)
Liliana:
oh My God (anatabasamu)
Anna:
kila mtu anaifurahia hii siku Liliana
Liliana:
hata Mimi naona
(Wanatembea mpaka katika gari
lililopambwa vizuri kabisa maalumu kwa ajili ya siku hii muhimu, wanapanda huku
ngoma na tarumbeta zinawafata kwa nyuma)
Liliana:
Leo ni siku kubwa sana yaani siamini (anageuka
nyuma) ona magari
Bella:
usijali hiki ni kidogo mpenzi kanisani ndo kuna raha yote
Liliana:
kwanini?
Bella:
si ndo alipo mumeo?
Liliana:
(anatabasamu kidogo)
(Safari ya kuelekea kanisani kwa
ajili ya kushuhudia muungano kati ya Liliana na Raphael)
Liliana:
(moyoni) leo ni siku yangu muhimu
sana yaani hata sijui nifurahi au nilie natamani wazazi wangu wangekuwepo na
Zaidi mwanamke aliyenilea kwa upendo mkubwa kama vile mimi ni mwanae hata yeye
natamani angekuwepo angalau akae pembeni yangu ashuhudie umati wa watu
ulivyofurahi na mimi (anaguna) ila
maisha yamenipitisha (anacheka kidogo)
kuanzia kupoteza wazazi wangu mpaka kumpata mama yangu Bianca maisha ya
kifahari niliyoish baada ya kuteseka mikononi mwa shangazi yangu mpaka kufikia
kumuua hawara yangu baba mzazi wa mume wangu mtarajiwa aisee (anacheka kidogo) kila mtu kuna hadithi
mwenyezi Mungu kamuandikia ni jukumu let utu kuipokea kwa Imani kwamba kesho
itakuwa sawa au asubuhi itafika halafu mambo yawe sawa
Bella:
(anamshtua Liliana) unawaza nini
cousin?
Anna:
tumefika kanisani
Liliana:
(mapigo ya moyo yanamuenda kasi Sana)
Anna:
relax hakuna kitakachoharibika not today my cousin
(Mlio wa harusi wa kiitaliano
unasikika na watu wanaingia kanisani wakijiandaa kumpokea malkia wa siku hiyo)
Liliana:
naona watu wamekaa kunisubiri…
Anna:
relax acha sisi tuingie kanisani
Liliana:
okay nawakuta huko
Bella:
bye all the best
Gabriel:
(anakuja) hujambo?
Liliana:
sijambo shemeji shikamoo?
Gabriel:
marahaba Mimi ndo nimekuja kukuchukua nitakusindikiza mpaka altareni
Liliana:
(machozi yanamtoka) Asante Sana
shemeji
Gabriel:
usijali (anampa mkono) haya taratibu
Anza kutembea
Liliana:
(anaanza kupiga hatua taratibu)
Gabriel:
hongera Sana
Liliana:
Asante Sana shemeji
(Mlango unafunguliwa na kila mtu
anasimama kumkaribisha malkia wa siku hiyo, malkia ni malkia kweli amependeza
sio utani yaani gauni limekaa mahali pake na kila mtu anaushangaa urembo na
umbo zuri alilojaaliwa Liliana)
Liliana:
(hatua kwa hatua kwa madaha na tabasamu
ang’avu anaisogelea altare alipo mchumba wake mpenzi Raphael)
Raphael:
(anamuangalia kwa mapenzi makubwa)
wow oh my God
Liliana:
(anatabasamu akimuangalia mume wake
mtarajiwa)
Raphael:
beautiful
Liliana: (baada ya hatua kadhaa hatimaye anafika
kwa mumewe mtarajiwa)
(Wapendanao hao wanashikana
mikono kasha kwa upendo mkubwa wanaangaliana usoni, kisha wananagalia mbele
kusikiliza maelekezo ya mchungaji)
Mchungaji:
pandeni hapa altareni
Maharusi:
(wanapanda)
Mchungaji:
(anatoa neno kidogo)
Wageni:
(wanaonekana kuwa na furaha sana mwenye
kupiga picha tukio lile mwenye kuchukua video yaani kila mmoja na jinsi
alivyopenda kuishangilia siku ile ya Liliana na Raphael)
Raphael:
(anamng’oneza mkewe mtarajiwa)
umependeza sana mke wangu
Liliana:
(anatabasamu)
Raphael:
Mungu amejua kuumba wewe ni mwanamke mzuri sana
Liliana:
(anatabasamu)
Raphael:
Mimi ni mwanaume mwenye bahati sana
Liliana:
hata Mimi ni mwanamke mwenye bahati sana my love yaani najivunia kuwa wako
Raphael
Raphael:
(anaibusu mikono ya Liliana)
Mchungaji:
(anatania) Kama mmemaliza
kunong’onezana tunaweza kuendelea
(Watu wanacheka)
Liliana:
(anacheka Kwa aibu)
Mchungaji:
(anaanza ibada ya ndoa, baada ya kuongea
maneno machache anaziita Pete)
Bianca:
(akiwa amependeza Sana analeta Pete za
ndoa na kumkabidhi mchungaji)
Mchungaji:
Asante mtoto mzuri
Bianca:
(anarudi kukaa alipo mama Raphael na
Michael)
Mchungaji:
(anampa Pete moja Liliana na nyingine
Raphael)
(Maharusi wanapokea Pete hizo na
kuzishikilia mkononi kusikiliza maelekezo ya mchungaji)
Mchungaji:
(Kwa Raphael) nyanyua mkono (Kwa Liliana) haya fatisha maneno haya
Liliana:
(anakaa tayari)
Mchungaji:
mwenzangu pokea Pete hii
Liliana:
(anafatisha)
(Zoezi la kuvalisha Pete
linaendela na hatimaye linafika mwisho, watu wanashangilia sana na kulifurahia
tukio lile takatifu)
Mchungaji:
basi baada yahaya yote nawatangaza kuwa me na mue halali na alichokiunganisha
Mungu mwanadamu asikitenganishe
(Nderemo, vifijo vinalipuka
kanisani humo, watu wanawapongeza kwa hatua mpya maishani mwao, maharusi wanasaini
vyeti vyao, picha zinapigwa kwa fujo, ngoma zinasikika kila kitu kinaonekana
kuwa vizuri)
Liliana:
(anajisemea moyoni) oh mama zangu
natamani mngekuwepo muone furaha yangu leo
(Kwenye umati wa watu anaonekana
mama yake mzazi Liliana pamoja na Bianca)
Liliana:
(anatabasamu anapoona) kumbe mpo
nawapenda Sana asanteni Kwa kuwepo hapa furaha yangu imekamilika
Mizimu:
(inatabasamu kisha inatoweka)
Liliana:
(anaendelea kufurahia pamoja na mume na
ndugu, jamaa na marafiki)
Raphael:
finally baby we are happy (anambeba mkewe
Kwa upendo)
1 Comments
Get ready for story number 3
ReplyDelete