SCENE 18: -
(Asubuhi ya siku ya pili yake Miriam
anajiandaa kuondoka nyumbani)
Miriam
:( anaonekana ana haraka Sana)
Ariana
:( amekaa mezani anapata kifungua kinywa)
upo busy Sana ndugu yangu siku hizi sikuelewi
Miriam
:( anasimama na kumsikiliza)
Ariana:
upo Kama kuna shemeji…
Miriam
:( anacheka kidogo) hapana dada shikamoo
Ariana:
marahaba… (Anapaka siagi kwenye mkate kwa
kutumia kisu kidogo) kama una shemeji niambie jua mimi ni dada yako kwahiyo
mambo mengi ni mimi ndo natakiwa kujua wewe ni mdada umeshaakuwa kwahiyo kuwa
katika mahusiano ni jambo la kawaida
Miriam:
najua dada ila bado sijapata boyfriend…
Ariana:
usinitanie bwana…ulivyo mzuri tena mwenye bahati unakosa mwanaume?
Miriam:
kabisa dada
Ariana:na
yule aliyekuleta jana?
Miriam:ni
boyfriend wa Vanessa yule
Ariana:
kweli ee
Miriam:
yes dada…
Ariana:
nina shida…unajua Miriam
Miriam:
shida gani dada, please talk to me
Ariana:
Jeremy
Miriam:(anashtuka kidogo)
Ariana:(anamuangalia) Jeremy ameniandikia meseji
amesema kuwa anaomba tusitishe uchumba wetu kwamba hataki kabisa mahusiano na
mimi
Miriam:(anaguna) mama na baba wanajua?
Ariana:
hapana hawajui nataka nimbembeleze Jeremy ili aendelee na mipango ya harusi
Miriam:(anaguna) mbona mtihani
Ariana:
sio mdogo mdogo wangu, ni mtihani tena mkubwa sana
Miriam:
mpigie simu uombe uongee nae jamani
Ariana:
hapokei simu zangu nampigia mpaka nimesajili namba mpya nampigia ila naona
haisaidii chochote maana hapokei
Miriam:
ukimuuliza shida nini anasemaje?
Ariana:
ana mwanamke anayempenda Kwa dhati, yaani wanaume wana majanga jamani
Miriam
:( anaguna) yaani mbona majanga?
Ariana:
tuombeane tu shoga yangu…naomba tu na wewe uwe makini maana wanaume wana mambo
mengi sana
Miriam:
sawa dada…nimekuelewa
Ariana:
sasa naomba unisaidie jambo Fulani...
Miriam:
nitakusaidia Kwa lolote utakaloniomba, likiwa ndani ya uwezo wangu kweli kabisa
nitakusaidia dada
Ariana:
ongea na Jeremy mwambie Mimi nampenda sana tena sana natamani tufunge ndoa,
tutimize malengo ya wazazi wetu...Niombee mdogo wangu ongea nae sawa ee
Miriam
:( kimya kidogo huku anamuangalia Sana
dada yake)
Ariana:
nambie utanisaidia au?
Miriam:
nitakusaidia dada…
Ariana:
Asante Sana mama…. (Anaendelea kunywa
chai)
Miriam:(anajisemea moyoni) ni lazima niache huu
ujinga naoufanya Jeremy ni mchumba wa dada yangu na dada yangu anampenda
sana…ni lazima niachane na Jeremy mara moja
Ariana:
mbona huendi sasa maana ulikuwa unajifanya una haraka
Miriam
:( anashtuka kutoka kwenye mawazo)
unasema?
Ariana:
nenda bwana utachelewa huko ulipokuwa unaenda
Miriam:
sawa baadae basi
Ariana:
haya poa ila na wewe nitambulishe shemeji
Miriam:
sina mtu dada...nipo tu…
Ariana:
haya bwana wewe jifanye unanificha, mtakuja kusema tu
Miriam
:( anacheka kisha anatoka nje) Ni
lazima niachane na Jeremy
(Gari la Jeremy linaegeshwa mbele
ya Miriam)
Jeremy:
mrembo wangu uko poa?
Miriam:
Jeremy hutakiwi kuwepo hapa
Jeremy:
nimebadili gari hawatajua kuwa ni mimi…twende nikupeleke chuoni halafu baadae
naomba tutoke dinner
Miriam
:( anashusha pumzi) Jeremy
Jeremy
:( anamfungulia mlango) comeon panda kwenye gari twende basi
Miriam
:( anapanda)
Jeremy
:( anamuangalia) are you okay?
Miriam:
no
Jeremy:
what happened? Unaumwa? (Anamgusa kwenye
paji la uso) mbona joto ni la kawaida?
Miriam:
siumwi…Jeremy
Jeremy:
ila?
Miriam:
tuachane Jeremy
Jeremy:(anashtuka) what?
Miriam:
umenisikia vyema Jeremy…wewe ni mchumba wa dada yangu na dada yangu amesema
anakupenda na anataka umuoe
Jeremy:
what are you talking about?
Miriam:
hatuna sababu ya kuwa wapenzi kwanza mimi ni mtoto mdogo sana
Jeremy:
lakini nakupenda sana ni wewe baby ndo nataka nikuoe (anafungua mlango) naenda kuwaambia wazazi wako kuwa nataka kukuoa
wewe
Miriam:
ukitaka kuniudhi fanya hivyo…nitajirusha ghorofani nijiue…
Jeremy
:( anafunga mlango) embu twende
sehemu baby tukaongee naona umepaniki sana
Miriam:
hakuna cha kuongea mimi na wewe sijui unanielewa…dada yangu anaomba sana kuwa
na wewe, wewe unadhani atafanyaje siku akijua kuwa mimi na wewe ni wapenzi,
ataona usaliti na hatawahi kunisamehe, nakupenda Jeremy ila nampenda dada yangu
Zaidi
Jeremy:
then let us fight for this love my love,
Miriam:
sina hizo nguvu Jeremy
Jeremy:
unazikosaje hizo nguvu jamani? Ok hold on...Nakupenda Sana Miriam tulia
tutatoka tu kwenye huu usiri na ninakuhakikishia kila kitu kitakuwa sawa
Miriam:
no Jeremy...no…please Kama humtaki dada yangu ni bora ukapende mtu mwingine na
sio mimi…mimi ni mdogo wa Ariana na kwa ugumu mkubwa nimeyatengeneza mahusiano
yangu na yeye
Jeremy:
tafadhali usijifunge…
Miriam:
naachaje…please try to understand jamani tusijifikirie wenyewe…tufikirie na
wengine jamani
Jeremy
:( Analia) that is not fair Miriam
Miriam:
iam so sorry ila dada yangu ndo kila kitu kwangu siwezi kumdanganya dada
yangu…siwezi kumsaliti
Jeremy:
sitaki kuwa na mtu yeyote Zaidi yako Miriam
Miriam:
jaribu kuwa muelewa basi jamani Jeremy…
Jeremy:
No siwezi kukuelewa Miriam…nakupenda Sana…you are the woman of my life honey ni
wewe ndo nataka uwe mama wa familia yangu…sio Ariana...Nimeshakuambia nilikuwa
naona nimekuwa na pia umri unaenda ndo nikawaambia baba na mama wanaifanyie
mpango wa kutafuta mchumba sikujua kama ningekutana na wewe baby...
Miriam:
tuondoke tutaongea mbele huko
(Jeremy anawasha gari kisha
analiondoa mahali hapo)
1 Comments
Mambo n 🔥🔥
ReplyDelete