SCENE 7: -
(Asubuhi nzuri na ya kupendeza
tena ya siku nyingine na siku ya kwanza ya juma yaani Jumamosi, Ken na mkewe
Keddy wanausubiri kwa hamu ugeni wa mchumba wa kupangiwa na wazazi wa Ariana)
Keddy:
yaani nimefurahi jamani hii siku imefika mwanangu nae aolewe jamani…
Ken:
kweli kabisa mke wangu na njia za Mungu hazichunguziki hata kidogo…Jeremy ni
kijana mcha Mungu sana…baba yake aliponiambia kuwa kijana wake amemaliza masomo
na kwa sasa anatafuta mke nikamtaja mwanangu na hapohapo baba yake Jeremy
akaniunga mkono na kusema kuwa watafaa kuwa wanandoa na wataishi vizuri pia
Mary:
kumbe watoto hawajawahi kuonana?
Keddy:
ndio…baba Ariana na baba wa huyu kijana wanajuana na wanasali kanisa moja na
wote ni wazee wa kanisa
Mary:
sawasawa…
(Miriam anakuja walipo Ken, Keddy na Mary)
Mary:
vipi wewe?
Miriam:
wageni wanakuja
Ken:
sawa… (kwa Mary) kaandae vinywaji na
chakula Miriam atakusaidia…kwa Ariana asitoke kwanza...
Mary:(huku anatabasamu) sawa shem...
(Kengele ya mlangoni inalia)
Keddy:(haraka anafungua mlango) karibuni jamani
(Wageni ni pamoja na kijana mmoja
mrefu, mtanashati tena anaonekana ni mstaraabu sana, kuna mzee na bila shaka ni
baba wa kijana huyu mtanashati lakini pia kuna kijana mwingine ni mrefu ila wa
wastani)
Mzee:(huku anaongoza njia) asante sana…na
Amani iwe juu ya nyumba yenu
Ken:
amina karibuni sana
(Wageni wanakaa)
Miriam:(anatokea akiwa amebeba vinywaji na
anaonyesha tabasamu wakati wote)
Jeremy:(anamuangalia Miriam kwa umakini mkubwa sana)
wow… (anamnong’oneza baba yake) baba
je huyu ni mwanamke nayetarajia kumuoa?
Baba:
hapana mwanangu, mkeo mtarajiwa hapa hayupo utamuona baadae mara baada ya
kusikilizana pande zote mbili wewe tulia tu kila kitu kitakuwa sawa
Jeremy:(kimya huku anajisemea moyoni) huyu
mwanamke ni mrembo sana…na nimetokea kumpenda sana…
Miriam:(hana habari anatabasamu tu)
Jeremy:(anapokea kinywaji kutoka kwa Miriam)
unaitwa nani?
Miriam:
naitwa Miriam…na ni mdogo wake Ariana…shemeji karibu kwenye familia
Jeremy:(anajisemea moyoni) nitakaribia kwa ajili
yako…nimekupenda sana Miriam na nitakuoa wewe na sio Ariana sijui nimefanya
nini kumkubali mwanamke ambae sikuwahi kumuona hata mara moja
Mzee:(kwa Miriam) unaonekana una heshima
sana…unasoma au unafanya nini?
(Keddy na Ken wanatabasamu)
Miriam:(anajibu kwa ujasiri) nasoma chuo nipo
mwaka wa kwanza…nasomea sheria…
Mzee:
safi sana unataka kuwa muamuzi kama Debora?
Miriam:
hapana baba nataka kuwa wakili
Mzee:
safi sana…
(Wakati huo Ariana anawachungulia
na hafurahishwi na jinsi watu wanavyomfurahia Miriam)
Ariana:
yaani huyu mwanamke kila sehemu anataka kujionyesha yeye ndo mzuri…(anafyonza)ananikera kweli yaani (anamchungulia Jeremy) ila mwanamme
mzuri huyu…anafaa kuwa mume wangu…he is so handsome
(Huku sebuleni, furaha na Amani
zinaendelea kutawala)
Mzee:
basi sawa… (anamuangalia Miriam)
nimekufurahia sijui kwanini?
(Wanacheka sana)
Jeremy:(anajisemea moyoni) hunizidi
mimi…nimemfurahia sana na hata kama unasoma nitakusubiri tu sina haraka ya kuoa
sasa…nimempata mwanamke wa maisha yangu na sina mpango wa kukuacha…Miriam my
love…
Miriam:(anaendelea kutabasamu kisha anaondoka na
kwenda zake jikoni)
Jeremy:(kwa baba yake) dad… (anamnong’oneza baba yake) kwani leo ndo tunatoa mahari?
Mzee:
hapana mwanangu au unaonaje?
Jeremy:
isiwe leo lakini pia mi naona mtupe muda kidogo mimi na Ariana tujuane tuzoeana
na Zaidi tuwe marafiki…
Mzee:
sawa haina shida mwanagu sisi tunakusikiliza wewe na huyo mwenzio…
Jeremy:
asante baba
Ken:(anaangalia mezani) oh naona chakula
tayari lakini kabla ya hapo naomba nimlete kwenu binti yangu mkubwa mpendwa
sana
Mzee:
bila shaka…
Ken:
mama Ariana nenda kamlete binti yetu mpenzi…
(Wageni wanaonyesha furaha)
Keddy:(ananyanyuka na kuingia ndani alipo Ariana na
baada ya muda anatoka akiwa na Ariana)
Ariana:(anaonyesha tabasamu na aibu pia)
Mzee:(anaonyesha kumfurahia pia)
Ariana:(anamsalimia baba Jeremy kwa heshima zote)
Mzee:
marahaba mama…
Ariana:(anamsalimia kaka aliyekuja na Jeremy kama
mshenga wake)
Mshenga:(anaitikia na anaonekana ni kijana mwenye
aibu sana)
Ariana:(anamsalimia Jeremy)
Jeremy:(anamuitikia na kuonyesha tabasamu ila
anamuangalia Miriam)
Miriam:(hana kinyongo wala nini na anaonekana ana
furaha kuliko mtu yeyote hapo)
Ken:
basi baada ya hayo…tujongee mezani...
Mzee:
asante sana
(Wenyeji wanawaongoza wageni na kwenda mezani
kupata chakula cha mchana pamoja)
Jeremy:(anamuangalia sana Miriam)
Ariana:(anamuona Jeremy anavyomuangalia Miriam)
Miriam:(anakula na wala hana hata muda na mtu)
(Familia zote mbili wanaendelea
kula huku kila mmoja wao anafurahia chakula kile, baada ya kula kwa muda mrefu
kidogo hatimae wanamaliza kula)
Mzee:(ananyanyuka na kwenda kunawa) chakula
kitamu sana
(Keddy na Mary wanafurahi)
Ariana
:( anachukia Sana maana anajua kuwa
aliyepika chakula kile ni Miriam)
(Wageni wengine nao wananawa na
wao wanakisifu chakula)
Miriam
:( anatoa vyombo na kuvipeleka jikoni)
Jeremy
:( anamuangalia Ariana)
Ariana
:( anaona aibu na kuanza kumsaidia kutoa
vyombo)
(Wageni pamoja wenyeji wanarudi
sebuleni kukaa kidogo kabla hawajaaga, wanakaa kwa muda kidogo kisha wanaaga)
Mzee:
jamani tunashukuru Sana kwa kila kitu…tumefurahi sana
Keddy:
tumefurahi pia karibuni Sana
Mzee:
tutakuwa ni wakwe wazuri sana
Keddy:
kabisa
Ariana
:( anacheka)
Jeremy
:( anamuangalia Miriam)
(Wageni wananyanyuka na kuondoka
zao, wakisindikizwa na wenyeji)
Jeremy
:( anamuaga Miriam) bye Miriam (anaondoka yeye na mzee pamoja na mshenga
aliyekuja nae)
1 Comments
Love story is about to begin...what will happen next...don't go anywhere
ReplyDelete